Vyombo vya habari Tanzania na hatma yetu

Mwana wa Marium,
Sasa wewe unaona ni bora kwa taifa changa kuanza kuangalia namna ya kuwa na idadi ndogo za watu? No- and big no! Tunahitaji watoto- nadhani sehemu zingine Tz ni pori tu kwa kuwa watu ni wachache sana! Tz tuna vyanzo vingi vya maji hata kuliko Nigeria- angalia mito na maziwa kila mahali!

Your definition of usomi- is intersting! Well taabu yangu na wasomi kama ulivyosema huchelewa sana kuolewa/kuoa wakati wanasoma. Ila kumbuka pia hata akiolewa na miaka 27 bado mwanamke msomi Tz atazaa only 2 childern! Hili ndo kwangu ni issue. Hata mwanamme msomi at 30 anaoa mwal. at 24 wanazaa tu watoto wawili!

Yet wamachinga ndo tunawacha wanazaa watoto wengi- it is my view that kwa kufanya hivi we dont do justice for the welfare of future of our nation!

MzalendoHalisi:

Kizazi kinachokuja kinategemea zaidi misingi ya maisha utakayo waachia kuliko idadi yao. Vile-vile mapori unayoyaona wewe si mapori yaliokaa bure. Na utakuwa hutoi hukumu nzuri kwa kizazi kijacho, iwapo utataka idadi iongezeke kwa sababu kuna mapori.

Mapori yaliopo sasa ni kiini cha ENEGY ya sehemu kubwa wananchi wa Tanzania. Mapishi ya chakula Tanzania yanategemea sana mapori ambayo wewe unaona yanakaa bure. Miaka 20 iliyopita, kuni zilikuwa zinapatikana katika umbali wa mita 100 lakini sasa zaidi ya kilometa 2.

Vile vile mapori hayo ni yanategemewa na wanyama na wafugaji. Na vile vile ni vyanzo vya mito tuliyonayo. Na unanitia mashaka na wasiwasi mkubwa kutoelewa mchango wa mapori yetu. Machafuko kama ya Darfur chanzo chake ni ukosefu wa mapori.

Kinachoweza kuturudisha nyuma sana sio wasomi kuwa na watoto wachache bali ni kuwa na uwezo wa kuwapa watoto wao elimu ya kutosha kupambana na maisha ya kisasa. Na wamachinga kuwa na watoto wengi wasio na elimu. Na hali hiyo inajionyesha sasa na wala hakuna sababu ya kusubiri vizazi vinavyokuja. Machafuko ya kitabaka yanaweza kutokea.

Na vilevile siungi mkono sera za uzazi wa majira. Sera hizo hazina manufaa iwapo milango ya kazi na elimu itaendelea kuwa umefungwa kama sasa. Toka tumepata uhuru tunaendesha nchi kama jeshi. Jeshini unakuwa na makamanda wachache na wapiganaji wengi. Mawazo ya Nyerere na viongozi wengine yalikuwa kuwa na wasomi wachache na kundi kubwa la wenye elimu ya msingi linalopokea amri. Kosa la wasomi wa Tanzania ni kutaka kuendelea kuwa makamanda na wengine wapiganaji (wamachinga).
 
Hii ni kawaida yetu kuwa tuangalia sana matokeo ya maendeleo ya vitu bila kutazama kiini cha maendeleo.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa uwiano wa idadi ya watoto wapya wa kike na wa kiume katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Tabora ni sawa. Na kuna uwezekano mkubwa kuwa uwiano huo unapotea pale watoto hao wanapofikia umri fulani kwa sababu ambazo hatutaki kuzitafutia ukweli wake.

Kwa mfano; Wanaume wengi wa Botswana walikuwa wanafanya kazi katika migodi ya dhahabu huko Afrika Kusini. Hali hii ilifanya vijiji kukosa vijana wa kiume na kazi za kijamii kama mazishi zilibidi zifanywe na wanawake.

Vile vile watu wanahama kuelekea mijini na magonjwa tuliyo sasa yanaweza kueleza uwiano huo. .
Yote hapo juu mumble jumble!! I hurriedly shout out “Prima-facie!!!!”
But hii hapa chini Lo!

I hope Maryam hakusoma hii maanake utaweza kukosa umwana! LOL…;)
Do you have any scientific explanation for your insight onto this presumption? And I quote you again...
“Kwa mfano uwiano wa wajaluo na makabila mengine unaonyesha kuwa wajaluo wanapungua na sababu kubwa inatokana na mila yao ya kuto-tahiri.” Yaani hii kali ehhh Kwa sababu ya kuto-tahiri?

Au kuna kigezo hapa?:confused:
 
Yote hapo juu mumble jumble!! I hurriedly shout out “Prima-facie!!!!”
But hii hapa chini Lo!

I hope Maryam hakusoma hii maanake utaweza kukosa umwana! LOL…;)
Do you have any scientific explanation for your insight onto this presumption? And I quote you again...
“Kwa mfano uwiano wa wajaluo na makabila mengine unaonyesha kuwa wajaluo wanapungua na sababu kubwa inatokana na mila yao ya kuto-tahiri.” Yaani hii kali ehhh Kwa sababu ya kuto-tahiri?

Au kuna kigezo hapa?:confused:


Umenasa kwenye mtego. Sikuimalizia hiyo stori ili wenye fikra kama za waandishi wetu wa habari wanase. Mjomba umekurupuka.

Kutahiri kunaongeza ugumu wa ngozi ya kichwa cha uume na kupunguza uambukiza wa magonjwa ya zinaa. Kwa mfano mtu alitahiriwa ataambukizwa kwa kupitia njia mkojo tu na yule asiye atambukizwa kwa kupitia kwenye njia ya mkojo na ngozi laini ya kichwa cha uume wake (scientific fact).

Tukija kwenye statistics. Makabilya yasiotahiri yameathirika zaidi na ugonjwa wa ukimwi kuliko yale yenye mila za kutahiri. Mfano ni wajaluo wa kando ya Ziwa Victoria zaidi kuliko makabila mengine.

Kutokana na hoja hii kuna uwezekano mkubwa kuwa wahaya wameathirika zaidi sio kwa kupenda ngono hila tohara.

Tukija kwenye sera za kukinga kukinga ukimwi, serikali ya afrika kusini imeanzisha kampeni ya kutahiri kwa taifa zima.

Habari kama hizi zitachukua muda kufikia IPPMEDIA au Guardian lakini zina zaidi ya nusu mwaka.
 
Presumptious as it sounds Mimi naamini huyu Maryam alitaka kusema Wajaluo wanapungua na sababu kubwa ni wao kufa na Ukimwi! Duh, umejituta hapo! na Atanaye naye kakurupuka sasa hapa sijui itakuwaje?
 
"Mwana Wa Maryam;Umenasa kwenye mtego. Sikuimalizia hiyo stori ili wenye fikra kama za waandishi wetu wa habari wanase. Mjomba umekurupuka."
Sijanasa kokote na kukurupuka huko ni kwa sababu sikuwa nataka kuichambua hii post yako bali kupata jibu nililokuuliza! Na kama hujasoma vizuri nilikuelewesha kwa nini nimekurupuka " I hurriedly shout out “Prima-facie!!!!”
But hii hapa chini Lo!"


Umenasa wewe hapa!!

Do you have any scientific explanation, news articles, UN report or something to prove that wajaluo wanapungua sana kwa kuathirika na Ukimwi?

"Kutahiri kunaongeza ugumu wa ngozi ya kichwa cha uume na kupunguza uambukiza wa magonjwa ya zinaa. Kwa mfano mtu alitahiriwa ataambukizwa kwa kupitia njia mkojo tu na yule asiye atambukizwa kwa kupitia kwenye njia ya mkojo na ngozi laini ya kichwa cha uume wake (scientific fact)."

Ndio hii inaweza kuwa scientific fact kwa watoto kuanzia miaka 6-14! Wajaluo wangapi wamefanyiwa hii scientific study kuona kwamba kutokutairiwa kwao kemechangia UTI STD na hata HIV na kama hizo hapo juu zimewafanya wajaluo wasizaliane?

"Kwa mfano uwiano wa wajaluo na makabila mengine unaonyesha kuwa wajaluo wanapungua na sababu kubwa inatokana na mila yao ya kuto-tahiri.”
Yaani hii kali ehhh Kwa sababu ya kuto-tahiri? ehh?

Again! Hujanionyesha huwo uwiano, na makabila hayo mengine hujayataja!

"Kutokana na hoja hii kuna uwezekano mkubwa kuwa wahaya wameathirika zaidi sio kwa kupenda ngono hila tohara."

Huna hoja hapa ila mumble jumble! Wewe una visa na wajaluo?

"Tukija kwenye sera za kukinga kukinga ukimwi, serikali ya afrika kusini imeanzisha kampeni ya kutahiri kwa taifa zima."

mumble jumble...wapi takwimu zako?

"Habari kama hizi zitachukua muda kufikia IPPMEDIA au Guardian lakini zina zaidi ya nusu mwaka."

Kulaleki!!

Huna hata aibu kusema haya weka facts hapa! Wewe Umezitoa wapi?
Mdahalo ndio huu
 

Utafiti ulifanyika Kenya kwenye vijiji vya wajaluo wanaoishi kando ya ziwa. Na wakalinganisha na makabila mengine yanayoishi huko na imeonyesha wanaume wa kijaluo wameathirika sana.

Kwa taarifa ni imani ya wajaluo kuwa kutahiri kunapunguza nguvu za kiume. Na kabla ya ugonjwa wa ukimwa, ongezeko la watu katika jamii za kijaluo lilikuwa kubwa kuliko makabila mengine ya Kenya.


Ku-support nayosema hapa naomba soma kipande hiki. Kutoka kamati ya umoja wa mataifa inayoshungulikia tatizo hilo http://www.who.int/hiv/topics/malecircumcision/en/index.html. Na vile vile kabla ya taarifa hiyo uchunguzi ulifanyika naomba soma taarifa kutoka The Boston Globe http://www.boston.com/news/world/canada/articles/2006/08/16/circumcision_touted_as_hiv_defense/.


Male circumcision in HIV preventionWHO, the UNAIDS Secretariat and their partners are working to develop specific policy recommendations for expanding and promoting male circumcision as a method of HIV prevention. The UN agencies have noted with considerable interest the announcement made by the US National Institutes of Health (NIH) in December 2006 on the results of two trials which showed an approximate halving of risk of HIV infections among men who were circumcised. The trials carried out in Kenya and Uganda, support results from earlier South Africa Orange Farm Intervention Trial in 2005, which demonstrated at least a 60% reduction in HIV infection among circumcised men.

The UN agencies emphasize that male circumcision does not provide complete protection against HIV infection. It should never replace other known effective prevention methods and should always be considered as part of a comprehensive prevention package, which includes correct and consistent use of male or female condoms, reduction in the number of sexual partners, delaying the onset of sexual relations, and HIV testing and counselling.

WHO and the UNAIDS Secretariat have convened technical consultations on trial findings and developed policy recommendations for countries. The groups will be working cooperatively to identify the best means of increasing the delivery of safe circumcision services in countries that choose to scale up male circumcision as a way of HIV prevention.
 
Shida nzima ya hiki tunachojadiliana hapa ilianza na mtaalamu Thomas Robert Malthus (1766-1834), mchumi na mtaalamu wa demografia (sifahamu tafsiri yake sahihi ya kiswahili).
Huyu bwana 'aliitishia' dunia kwa utafiti wake kwa kusema kuwa uzalishaji wa chakula hauendani na ongezeko la watu duniani (kwa wakati huo), kwa hiyo kuna wakati huenda dunia ikakumbwa na baa kubwa la njaa na kufikia mwisho wake, kama hazitafanyika juhudi zozote za makusudi za kuzuia ongezeko hili la idadi ya watu. Alidai kwamba ongezeko la watu hukua ki-nambamraba kwa wastani wa 2,4,,8,16....> wakati uzalishaji wa chakula huenda kwa wastani wa kiarithmetiki yaani 1,2,3,4....>. Sasa suala hili ndilo lililoshikiwa bango na mataifa makubwa kuwa lazima kuwe na mabadiliko katika uzazi, kwamba lazime kuwe na uzazi wa mpango.
Kwa hapa kwetu Tanzania, huduma hizi za uzazi wa mpango zilianza miaka ya '60, lakina zilikuwa hazina umaarufu sana kama ilivyo sasa. Kwa hiyo, UMATI (Chama Cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania) ilikuwepo tangu enzi hizo, wote hawa ni katika kutekeleza somo la Bw Malthus.
Kwa mujibu wa Bw Malthus, vitu vya asili ambavyo vingepunguza idadi hii ya watu bila juhudi za mwanadamu ni kama magonjwa, vita, njaa na vitu kama milipuko ya volkano na ukame mkali. Akaendelea kudai kwamba iwapo mwanadamu atataka kupunguza idadi ya wtu kwa juhudi zake mwenyewe, basi inabidi atumie mbinu kama kuua mimba, kufunga uzazi, kukaa useja ama ukapela, mauaji ya makusudi, kujiua, kutumia dawa za kuzuia mimba na ngono za jinsia moja.
Tangu miaka hiyo, yaani karne ya 18 na 19 hadi leo bado nchi tajiri nyingi zinafuata maelekezo haya katika kuzuia ongezeko la watu duniani. Na sasa nchi masikini ndio zinaiga mkumbo, sijui hatima ya yote itakuwa ni nini.
Tuendelee kuchambua hoja, angalau nimetoa chanzo cha nadharia hii ya kupunguza idadi ya watu.
 
Kimsingi madai (sio takwimu) ya Mwambalaswa kuwa Tabora ina wanaume wengi kuliko wanawake sio kweli kabisa. Ukianzia ngazi ya taifa, wanawake ni asilimia 51 na wanaume ni asilimia 49.
Nimefuatilia takwimu sahihi za serikali na matokeo ni haya hapa:

Tabora (sensa ya mwaka 2002)
Jumla ya watu wote ni 1,717,908
Wanaume ni 846,196
Wanawake ni 871,712

Kiwilaya, idadi ya watu ni hii.
Nzega
Population 417,097
Male 203,371
Female 213,726

Igunga
Population 325,547
Male 159,667
Female 165,880

Uyui
Population 282,272
Male 139,998
Female 142,274

Urambo
Population 370,796
Male 183,229
Female 187,567

Sikonge
Population 133,388
Male 66,569
Female 66,819

Tabora Urban
Population 188,808
Male 93,362
Female 95,446

Nikiangalia matokeo ya wilaya zote za mkoa huu, wanaume ni wachache kuliko wanawake, kwa hiyo mpaka hapa namgalagaza Mwambalaswa vibaya sana. Labda tuangalie katika jimbo lake kukoje.

Sensa ya Mwaka 2002
Chunya
Population 206,615
Male 103,762
Female 102,853

Hapa Bw Mwambalaswa huenda ana pointi, kwani kwa jimbo lake wanaume ni wengi kuliko wanawake. Na hii bila shaka inatokana na migodi ya dhahabu kule Chunya, kwani wanaume wengi wanakimbilia Chunya kuchimba dhahabu, kama ilivyo kwa Botswana. Sasa suala la kusema apewe sababu za hali hii nadhani hiyo niliyotoa hapo juu ni mojawapo, kwa hiyo asitafute mchawi. Kwa hiyo kilichoongeza idadi ya wanaume hapo jimboni kwake ni uhamiaji (immigration)ya wachimba madini.
 
IDIMI,
Nimependa sana Kiswahili ulichotumia ndugu yangu- Kinambamraba- Geometric Exponential yaani unanikumbusha wakati tukiwa darasa la 5 primary- Kula 5!
 
@Mzalendo,
Nilikuwa najikumbusha enzi hizo za shule ya msingi, mamboya kivimbe (volume), vipeo na vipeuo (exponents) nk. Kama una nafasi tafadhali pitia pale "Jukwaa La Elimu", ujikumbushe kidogo kuhusu mada fulani ya shule za msingi, kuna wachangiaji mahiri sana pale utakutana nao, Kama Gamba La nyoka nk.

@Mwana Wa Mariamu,
Nimeshangaa sana kuona takwimu za Wajaluo, sikufukiria kuwa kuna watu wamefanya utafiti kuhusu tohara na maambikizi ya ukimwi. Ni hivi majuzi tu nilipokuwa naangalia taarifa ya habari BBC, niliposhangaa kuwa, wanaume waliotahiriwa wana nafasi kubwa ya kutoambukizwa virusi visababishavyo ukimwi kuliko wale wasiotahiriwa.
Amazing!
Je Tanzania tuna programu yoyote ya uhamasishaji tohara kwa wanaume?
Sio tukazanie kupiga vita ukeketaji tu, tuwashauri na wanaume waende sunna, hasa ile mikoa ambayo haina utaratibu huo.
 
Nimekuwa nikipata wakati mgumu kuelewa kama kweli tanzania tunavyombo vya habari vinavyofanya kazi ya kutafuta habari badala ya kuripoti habari kama wanavyo ipokea kutoka kwenye vyanzo vya habari.

Ninachotaka kusema hapa ni kuwa waandishi wetu wameshindwa kuoji kauli za watendaji wa serikali na wamebaki kuripoti kile ambacho wanakisema hata kama kina walakini ndani yake.

Kilichonisukuma kuanzisha hii mada ni hii kauli ya waziri mkuu kutaka apelekewe majina ya wala rushwa,wauza unga,na aina nyingine ya uchafu au huozo wowote,wakati raisi wake alishatamka kitambo kuwa na orodha ya hao wahusika. je hizo orodha ambazo zipo kwa mweshimiwa raisi ni nini utekelezaji wake au zilifikia wapi ?

Kuna swala la muhimbil,hatujaona hapa wahusika hasa mkuu wa kitengo cha MOI akiwekwa kitimoto ilikutoa ufafanuzi kitugani kilitokea.

Au sheria za waandishi wetu haziwaruhusu kufanya hivyo kama wa nchi za magharibi.waandishi wa kimangharibi kama kitu kimetokea hospitali basi kambi ya kazi yao itakuwa hospitali au sehemu yoyote ya tukio.

Kwa mwenye kuelewa kwa nini waandishi wetu wapo nyuma au ni sheria zetu haziruhusu basi tuelimishane juu ya hili
 
KT,

Tatizo unaloliona si kwa waandishi tu. Ni tatizo la wawekezaji ktk vyombo hivyo kutaka high returns bila kuinvest accordingly. Hawataki kuajiri competent journalists kwa kuwa hawataki kuwalipa vizuri.

Hili ni tatizo pia kwa sekta nyingine...hata entertainment, ambako kununua bia lazima "ubembeleze sana bar maid akuuzie."
Hata hivyo wanajitahidi kwa mazingira magumu waliyomo kaka. Mabaya machache yasifanye tusahau mazuri yao.
 
Nafikiri tatizo ni kubwa kuliko linavyoonekana. Nafikiri there is something wrong somewhere in our education system. Our education system producers rote learners devoid of inquisitive mind. Halafu pia mfumo wetu wa elimu unafundisha watu kukubali na kuheshimu chochote kinachotoka kwa mkubwa. Hii sio tu kwa viongozi, it begins rightn from the family. Baba akisema kitu hata kama ni upuuzi mnatakiwa nyumba nzima mkubali hivyohivyo. Kwa hiyo mimi nafikiri tunayoyaona kwa waandishi wa habari ni reflection of a bigger problem in the society. I am afraid changing this sort of attitude will have to involve multiple players rather than a single entity such as a givernment.

Wewe kama umewahi kuhudhuria international conferences, watz wangapi huongea ukilinganisha na mataifa mengine? Mara nyingi tunajuaje wakati wa chai! Inauma lakini angalau kwa sasa ndivyo tulivyo!
 
Tatizo ninaloliona ni ukondoo amabao umetanda katika nyanja zote za maisha ya watanzania. Tu wapole sana, tunakubali kirahisi mno, we are not aggressive. hata kama ni haki yako still badala ya kudai utaomba na kubembeleza. Kuanzia siasa, viongozi wamebweteka, vyombo vya habari bado nafikiri habari zinachujwa na waliojuu kama siafu kabla ya kuandikwa au kurushwa hewani. sio competence bali kutokujiamini na woga wa kupoteza kibarua. mhhhhh
 
Ninachotaka kusema hivi waandishi kumi wakifika tuseme wizara ya afya na kuomba kuongea na waziri au naibu wake juu ya jambo fulani je wahusika watatoka au itakuwaje ?
 
Suala la corruption, maslahi na u-bias limewafumba macho baadhi ya waandishi wa habari. Wanasahau hata yale yaliyotamkwa kabla na wakayanukuu kwenye magazeti yao. Ndiyo maana mwendo wetu wa maendeleo ni wa Kinyonga.
 
Wakuu, nakubaliana na hoja zote ikiwa ni pamoja na our traditional system ambayo imetulea kwa namna tulivyo. Tunashindwa kushindana kwenye dunia ya ushindani kwa kuwa tu wazito mno. Hatubadiliki mind set zetu. Tunaogopa changes. Waandishi wa habari ni sehemu ya jamii yetu, na inareflect jamii yote ilivyo pia.

Achilia mbali michango yetu kwenye mikutano, lakini hebu angalia hata kwenye international TV and radio programs kama Straight Talk Africa, BBC's Have Your Say, au hata vipindi vya local TV stations...wanaopiga simu ni mataifa mengine jirani, kama Kenya, Malawi, Zambia, South Africa nk.

Unaongelea waandishi? hata namna ya public inavyopokea issues mbali mbali umeona? umesikia comments za wanaohojiwa juu ya mambo kadhaa yanayowahusa? Watu wamekulia ktk utamaduni wa kulalamikia tumboni. Waandishi wa habari, na ili tuwe sahihi tuseme ni tatizo la media industry...ni kati ya jamii hiyo ambayo ina wawekezaji wanaoona hali hiyo ni kawaida...sekta zote mkuu. Hakuna anayejali ku attain perfection kwenye kazi yake...kuanzia fundi rangi hadi waziri. kila kitu analenga kukamilisha kwa at least 50 per cent, wala si 100 per cent!
 
Ninachotaka kusema hivi waandishi kumi wakifika tuseme wizara ya afya na kuomba kuongea na waziri au naibu wake juu ya jambo fulani je wahusika watatoka au itakuwaje ?

Mkuu, ni haki ya kikatiba kila mwananchi kudai na kupatiwa habari. Hiyo ni article 18 kama sikosei, ya katiba yetu. Kwa waandishi, hili ni rahisi zaidi. Kwa hiyo hao waandishi wataruhusiwa kwanza katibu mkuu, ambaye msemaji wa wizara, au waziri mwenyewe.

Lakini kwa utamaduni tulio nao, hawa watu wanaweza kuomba waandikiwe maswali, halafu yatajibiwa at a later date! Kuna kasumba mbaya. Je, akipigiwa simu na BBC? Atajieleza safi sana, halafu hao hao wanasema vyombo vya ndani havina uzalendo...
 
Back
Top Bottom