Vyombo vya Habari Tanzania imarisheni 'Maslahi' kwa Waandishi wenu ili wasiwe wanang'ang'ania ziara za Wakubwa zinazowauwa kwa ajili ya Posho

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,548
108,860
Ukweli ni lazima usemwe hata kama ni Mchungu na bahati nzuri pia naisemea Tasnia ambayo naijua, naiishi na nimebobea nayo.

Waandishi wa Habari ( hasa mlio Newsroom ) mtakubaliana nami kuwa sasa ni kawaida kwa Waandishi wa Habari Kupenda kutumwa katika Ziara za Wakubwa ( Viongozi na Wanasiasa ) ili wapate Posho na 'Bakshishi' kadha wa kadha.

Na haiishii hapa tu bali kuna Wengine ( Waandishi wa Habari ) ama Wanarogana au wanachomeana Utambi kwa Wamiliki na Mabosi ili Wapendwe na Waaminiwe Wao na Ziara za Matukio ya Viongozi Wakubwa wa Mikoa, Kichama n Kitaifa wawe Wanawekwa ( wanatumwa ) Wao tu.

Nina uhakika kuwa Vyombo vingi vya Habari nchini Tanzania vingekuwa 'Stable Economically' basi Waandishi wa Habari wasingekuwa Wanagombana kuwepo katika Ziara za Kimatukio za Wakubwa ili wapate Posho bali wangskuwa Wanajipanga n Kujiratibu vyema na Kiuweledi ili Kutelekeza Majukumu yao ya Kitasnia.

Kwa mfano Ajali ya Jana Waandishi wa Habari wangdkuwa katika Magari yao ya Ofisini ( Kampuni zao ) huenda wangejipanga vyema Kiratiba na hata Kiitifaki kuwahi walikokuwa wakienda Ziarani ila Wote waliomba Lifti katika Gari la Dereva wa Land Cruiser la Serikali ambalo lilikuwa linawahi Msafara na Kuvuka hivyo hata Dereva nae hakuwa na Utulivu huo ukichanganya na Viburi vyao Madereva wa Magari ya Serikali nchini na hatimaye akawauwa Waandishi na hata Yeye nae Kufa papo hapo.

GENTAMYCINE najua kuwa Ajali zingine hazikwepeki na hazizuiliki kutokana na Uhalisia wake ila najua kukiwa na Udhibiti na Umakini mkubwa hasa kwa wana Habari kuacha Kupenda Kitonga ( vya Bwerere ) hasa vya Kudandia Lifti za Wakubwa ( Viongozi ) na Tamaa za kupata Posho na kuacha utaratibu wa Kimaadili kwa Tasnia yetu hii husika hakika tutakufa ( watakufa ) mno tu.

Nina uhakika Waandishi wa Habari wa Tanzania huu Moyo wa Kuzipenda hizi Ziara za Viongozi Wakubwa ili mdake Posho na wengine humo humo mnaomba 'Connections' za Uteuzi ( Kuteuliwa ) huko Serikalini mngehamishia katika Kutafuta Habari za maana, zenye Tija, za kuibua Masuala, Kukosoa na Kulielimisha Taifa letu na Kizazi chetu mngekuwa mmefanya la maana ila Wengi wenu Kipaumbele chenu ni Tanaa za Posho, Uteuzi na Kujipendekeza.

Poleni mnoWatanzania kwa Msiba huu.
 
Majeneza yaliyobeba miili ya waandishi wa habari watano waliofariki katika ajali wakiwa kwenye ziara ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel yakiwa yamewasili katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza kwa ajili ya shughuli ya kuagwa na ndugu, jamaa na marafiki. Picha na Mgongo Kaitira

17C7A337-5E49-46C0-9E66-356545F4A762.jpeg
 
Wapumzike mahalii wanapostahili....ilaa mkuu njaaa n mbayaaa sanaa asikwambie mtuu.......posho,connection,na uteuzi una uwakikaaa ndio zimechukua roho zao au n ajali km ajali tu imetokea
 
Majeneza yaliyobeba miili ya waandishi wa habari watano waliofariki katika ajali wakiwa kwenye ziara ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel yakiwa yamewasili katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza kwa ajili ya shughuli ya kuagwa na ndugu, jamaa na marafiki. Picha na Mgongo Kaitira

View attachment 2077987
Unajua jinsi ziara na matukio ya RS yanashirikisha waandishi wa habari au unajilopokea tu?
 
Ajabu ni kwamba tunasikia waandishi wakipewa msaada wa kupumzishwa katika udongo. Ila wananchi wengine hatujui kama serikali imelibeba jukumu au wameachwa.

Vyombo vya habari pia viongeze vigo wa ripota itasaidia kukuza ajira.
 
Wapumzike mahalii wanapostahili....ilaa mkuu njaaa n mbayaaa sanaa asikwambie mtuu.......posho,connection,na uteuzi una uwakikaaa ndio zimechukua roho zao au n ajali km ajali tu imetokea
Nakuunga mkono mkuu,hatuongei kwa ubaya..
Nilikuwa nafanya kazi kama fundi wa kituo fulani cha redio kinachomilikiwa na chuo kikuu fulani hapa mkoani kwetu..

Asee njaa mbaya, ikitokea kuna ugeni wa kiongozi fulani au professor fulani anapresent thesis yake ambapo waandishi wa habari inabidi waripoti ndipo majanga yanapoanza, majungu, kujipendekeza sometimes mpaka kushikana mashati.

Imagine hyo ni ndani ya taasisi kubwa tena ya wasomi, vipi huku changanyikeni!!!!!.
 
Upuuzi mtupu,kwamba waandishi wanakwenda kwenye ziara za kiserikali kwa sababu ya njaa ili walipwe posho?,ujinga ni pale unapokuwa hujui unachokizungumzia
 
Majeneza yaliyobeba miili ya waandishi wa habari watano waliofariki katika ajali wakiwa kwenye ziara ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel yakiwa yamewasili katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza kwa ajili ya shughuli ya kuagwa na ndugu, jamaa na marafiki. Picha na Mgongo Kaitira

View attachment 2077987
Kuna jeneza limewekewa bendera ya polisi au muandishi alikua mpelelezi
 
Ukweli ni lazima usemwe hata kama ni Mchungu na bahati nzuri pia naisemea Tasnia ambayo naijua, naiishi na nimebobea nayo.

Waandishi wa Habari ( hasa mlio Newsroom ) mtakubaliana nami kuwa sasa ni kawaida kwa Waandishi wa Habari Kupenda kutumwa katika Ziara za Wakubwa ( Viongozi na Wanasiasa ) ili wapate Posho na 'Bakshishi' kadha wa kadha.

Na haiishii hapa tu bali kuna Wengine ( Waandishi wa Habari ) ama Wanarogana au wanachomeana Utambi kwa Wamiliki na Mabosi ili Wapendwe na Waaminiwe Wao na Ziara za Matukio ya Viongozi Wakubwa wa Mikoa, Kichama n Kitaifa wawe Wanawekwa ( wanatumwa ) Wao tu.

Nina uhakika kuwa Vyombo vingi vya Habari nchini Tanzania vingekuwa 'Stable Economically' basi Waandishi wa Habari wasingekuwa Wanagombana kuwepo katika Ziara za Kimatukio za Wakubwa ili wapate Posho bali wangskuwa Wanajipanga n Kujiratibu vyema na Kiuweledi ili Kutelekeza Majukumu yao ya Kitasnia.

Kwa mfano Ajali ya Jana Waandishi wa Habari wangdkuwa katika Magari yao ya Ofisini ( Kampuni zao ) huenda wangejipanga vyema Kiratiba na hata Kiitifaki kuwahi walikokuwa wakienda Ziarani ila Wote waliomba Lifti katika Gari la Dereva wa Land Cruiser la Serikali ambalo lilikuwa linawahi Msafara na Kuvuka hivyo hata Dereva nae hakuwa na Utulivu huo ukichanganya na Viburi vyao Madereva wa Magari ya Serikali nchini na hatimaye akawauwa Waandishi na hata Yeye nae Kufa papo hapo.

GENTAMYCINE najua kuwa Ajali zingine hazikwepeki na hazizuiliki kutokana na Uhalisia wake ila najua kukiwa na Udhibiti na Umakini mkubwa hasa kwa wana Habari kuacha Kupenda Kitonga ( vya Bwerere ) hasa vya Kudandia Lifti za Wakubwa ( Viongozi ) na Tamaa za kupata Posho na kuacha utaratibu wa Kimaadili kwa Tasnia yetu hii husika hakika tutakufa ( watakufa ) mno tu.

Nina uhakika Waandishi wa Habari wa Tanzania huu Moyo wa Kuzipenda hizi Ziara za Viongozi Wakubwa ili mdake Posho na wengine humo humo mnaomba 'Connections' za Uteuzi ( Kuteuliwa ) huko Serikalini mngehamishia katika Kutafuta Habari za maana, zenye Tija, za kuibua Masuala, Kukosoa na Kulielimisha Taifa letu na Kizazi chetu mngekuwa mmefanya la maana ila Wengi wenu Kipaumbele chenu ni Tanaa za Posho, Uteuzi na Kujipendekeza.

Poleni mnoWatanzania kwa Msiba huu.
Kuna bahasha za khaki mzee ndio wanazikimbilia na ndio wanarusha habari zipo very biased.

Hii ni laana inawatafuna maana wanafanya kazi kinyume na miiko ya kazi yao.

Jiulize kwenye waandishi wa vyombo binafsi vya habari walikuwaje kwenye landcruiser ya serikali???? Wale wanapewa allowance za safari kama hizi ila tunajua ziara kama hizi huwa kuna fungu maalum la waandishi ili mkuu wa mkoa wampambe aonekane jembe.
 
Mkuu nayajua yote haya na hata na mengineyo kwani nimeshapita huko ( humo ) miaka ya nyuma na ndiyo maana leo nimeamua niwaambie ( niwachane ) huu Ukweli ili tubadilike ( wabadilike )
 
Back
Top Bottom