Vyombo vya habari punguzeni kuandika habari za uhalifu, mnauchochea

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
14,981
9,873
Kuna tatizo la vyombo vingi vya habari kuandika kwa sehemu kubwa habari za kihalifu na jinai kuliko habari za maendeleo, kiukweli watu wakiwa wanasoma hizo habari mara kwa mara kunaleta adiction fulani watu kuanza kuutekeleza uhalifu ule au kuanza kujenga hofu kwenye jamii.

Kwa muda sasa tumeona magazeti mengi yakiandika ukatili dhidi ya wanawake. Sasa tumeanza kuona wanaume nao wanaanza kukumbwa na kadhia za ukatili wa kijinsia ikiwemo kuchomewa moto ndani ya nyumba.

Ifike wakati hizi habari za kihalifu ziachwe kwa jeshi la polisi wao ndio wapewe jukumu la kuziwakilisha kwa umma na kwa namna gani, wapo watu wanazua fujo ili wapate umaarufu wa kisiasa bila kujali wanatengeneza taharuki zisizo za lazima kwa jamii.

Kuna vyombo viliandika kuwa Mbowe alikamatwa kwenye hotel ya taifive kwa polisi kukanyaga mlango wakati si kweli Mbowe alikamatwa katika hotel ya Freedom na sio kwa kukanyagiwa mlango.

Magazeti mengi yanahusisha kukamatwa kwake na harakati zake za kisiasa kumbe kakamatwa kwa makosa ya kihalifu tu, Mkuu wa Mkoa anazuia mikusanyiko kuwakinga watu na korona wengine wanahusisha na mikutano ya kisiasa na magazeti nayo yanashadadia
 
Kiswahili cha wapi hiki!?
 
Mleta mada hujui nini na mipaka ya mwandishi wa habari.

Anapotoa habari anaushahidi wa chanzo,kama hana ushahidi hawezi Fanya hivyo.

Pili, Polisi na Mwandishi wa habari wanategemeana.
 
Waanaandika kwa kuwa uhalifu wa kuratibiwa tena ule wa kudhulumu haki za msingi unafanywa kwa uwazi tena kwa ukiukwaji wa katiba wa wazi wazi.
 
Mleta mada hujui nini na mipaka ya mwandishi wa habari.

Anapotoa habari anaushahidi wa chanzo,kama hana ushahidi hawezi Fanya hivyo.

Pili, Polisi na Mwandishi wa habari wanategemeana.
tunapoandika habari za kihalifu nini objective ya hizo habari, mbona CCN hawaandiki habari za ubakaji marekani, mbona aljazeera waandiki habari za ukiukwaji wa haki za watu nchini saud arabia, mbona wanapokata watu vichwa na mikono hawatangazi aljazeera, sie hata watu wakinyimana unyumba kesho magazeti yote yameandika, kwanini msiongelee uzalishaji wa mbolea minjingu, kwanini msiandike habari za shabiby kununua buses mpya, kwanini tusiandike habari za bhakresa kununua fleet za scania toleo jipya, ila tukisikia bhakresa kamtishia mtu bastola magazeti yote yataandika. Hebu tujitahidi kuwa positive na nchi yetu.

Sasa hivi kuna mkakati wa trade harmonization katika bara la Africa na kuweka common tariff hamna hata mmoja anayezungumzia, benki tatu za serikali zimeungana hamna hata gazeti moja limeandika. Kuna hili Gazeti moja lenyewe nikuandika habari za mauaji tu utafikiri lina milikiwa na shetani
 
Wataalamu wa mambo ya fedha wamekaa kujadili kuwa na 15% ya kodi kwa nchi zote za dunia mpaka juzi ni Nchi 130 zilizolubali na kuweka saini Tanzania hatupo huku tupo kwenye kuongeza kodi badala ya kupunguza...
 
Kuna tatizo la vyombo vingi vya habari kuandika kwa sehemu kubwa habari za kihalifu na jinai kuliko habari za maendeleo, kiukweli watu wakiwa wanasoma hizo habari mara kwa mara kunaleta adiction fulani watu kuanza kuutekeleza uhalifu ule au kuanza kujenga hofu kwenye jamii.

Kwa muda sasa tumeona magazeti mengi yakiandika ukatili dhidi ya wanawake. Sasa tumeanza kuona wanaume nao wanaanza kukumbwa na kadhia za ukatili wa kijinsia ikiwemo kuchomewa moto ndani ya nyumba.

Ifike wakati hizi habari za kihalifu ziachwe kwa jeshi la polisi wao ndio wapewe jukumu la kuziwakilisha kwa umma na kwa namna gani, wapo watu wanazua fujo ili wapate umaarufu wa kisiasa bila kujali wanatengeneza taharuki zisizo za lazima kwa jamii.

Kuna vyombo viliandika kuwa Mbowe alikamatwa kwenye hotel ya taifive kwa polisi kukanyaga mlango wakati si kweli Mbowe alikamatwa katika hotel ya Freedom na sio kwa kukanyagiwa mlango.

Magazeti mengi yanahusisha kukamatwa kwake na harakati zake za kisiasa kumbe kakamatwa kwa makosa ya kihalifu tu, Mkuu wa Mkoa anazuia mikusanyiko kuwakinga watu na korona wengine wanahusisha na mikutano ya kisiasa na magazeti nayo yanashadadia
UNATUMIWA NA "WAKOLONI WEUSI". Hayo makosa ya Mbowe ya kihalifu yapi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom