Vyombo vya habari kwanini mnawakimbia CHADEMA na ACT Wazalendo?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Leo CHADEMA wameanza mchakato wa kumpata Mgombea Urais ila vyombo vya habari vikubwa nchini havikuripoti live tukio ilo.

Kura zimepigwa bado hawakutaka kuripoti, hata ITV ambao Wana breaking news hawakuwa habari yoyote kuonyesha Kuna Jambo linaendelea.

Mgombea amepitishwa bado vipo kimya, hata pale mwanahabari mwenzao Salum Mwalim alipewa ridhaa ya mgombea mwenza hawakutaka kuupa umma habari hii

Kateuliwa mgombea Zanzibar baro TBC, Star Tv na ITV wapo kimya

Nyarandu kapongeza na kusema anamuunga mkono Tundu but bado wapo kimya

BBC wametangaza na taarifa kuanza kusambaa mitandaoni ndipo wanaanza kuandika kidogokidogo.

Wapi nafasi ya vyombo vya habari Tanzania?

Leo naona CHADEMA wamejifunza, wamejiwekea mkakati wakurekodi matukio kwa simu na kuyarusha WhatsApp yasambae kila Kona hii ikiwa nikukabuiliana na mgomo wa vyombo vyetu vya habari .

ACT pia kupitia blogs na WhatsApp watarekodi na kurusha ninyi endeleeni kutumia Tv ambazo hazina tena waangaliaji tuone
 
Nilikuwepo cafe fulani napata kikombe cha black tea, ilitokezea.kuwa wameweka TBC (which I never watch by design) wakasema tu for 5 seconds kama CDM wamempitisha Lissu kuwa mgombea wa kiti cha Uraisi.

Nikamwambia yule niliyekaa naye meza moja hii ni sawa na Azam kugoma kuonesha fainali ya FA ikiwa inacheza kati ya Yanga na Simba wakati chanels nyengine zinaonesha!

TBC wanajipunguzia viewers kwa upumbavu wao wenyewe. Na matokeo yake watu husubiri habari za BBC na DW kusikiliza local news. Its unbelievable. Kama ingelikuwa TBC wana coverage nzuri basi BBC na DW zisingepata washabiki wengi wa kusikiliza local.news. Matokeo yake rating ya TBC inaanguka na kukosa mapato kwenye matangazo ya biashara.
 
Wangekuwa matapeli mngehangaika kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwahujumu kuwadhoofisha kuwafanyia unyanyasaji wa kila aina?
Matapeli ndiyo yanakamatwa kila kukicha mdanganyeni ndugu yenu tutamuadhibu kupitia sanduku la kura bila aibu na hatarudia
 
Matapeli ndiyo yanakamatwa kila kukicha mdanganyeni ndugu yenu tutamuadhibu kupitia sanduku la kura bila aibu na hatarudia
Chadema ndiyo walitapeli vyeti vya Daud Bashite? Chadema ndiyo walinunua kivuko feki cha Dsm Bagamoyo cha 1975 kwa bilion 8 ? Chadema ndiyo walitafuna trilion 1.5 wakamtoa CAG kafara kuficha aibu?
 
Kwa kadiri vyombo vya habari vinavyozidi kukosa ujasiri kuripoti baadhi ya matukio maarufu hapa nchini, ndivyo ambavyo vinavyozidi kupoteza umaarufu wake kwa wananchi. Habari hutofautina hadhi zake mbele ya walaji, katika hali ya kawaida haitegemewi kuripoti taarifa za kuzaliwa kwa panya juu ya dali ya nyumba yako, katika siku ambayo ng'ombe wako naye kazaa ktk zizi lako.

Kuna baadhi habari ni motomoto, na tena ambazo wafuatilaji wa mambo hutarajia ndizo zitapamba vichwa vya habari. Lakini badala yake inaonyesha kuna woga fulani umetamalaki wa kutenda kutokana na weledi na taaluma. Pengine hii ni kutokana na kukosa uhuru wa kufanya maamuzi sahihi kwa wakati.
 
Ww unzaota kabisa Tundu akipata 5% ya kura atakuwa amejitahidi sana
Unaleta mambo ya ushabiki wa Simba na Yanga katika mambo muhimu ya nchi? Funguo macho ya akili yako uone na uelimike kisha uache mizaha hiyo. Au unafikiri watz wa leo ni wale wa mwaka 47? Subiri.
 
Back
Top Bottom