Vyombo vya habari kuweni makini mnapowaita watu kuja kutoa ufafanuzi wa jambo fulani

Malunkwi

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
339
79
Hiva majuzi kulikuwa na kipindi kilichorushwa katika ktuo cha televisheni cha Clouds kilichohusu Ukweli kuhusu Freemasons, kwa kifupi wageni waalikwa ktk kipindi kile hakuna chochote walichofafanua wakaeleweka zaidi ya kububuja maneno tu na inavyoonekana ni kama waganga wa kienyeji wamekwenda kujitangazia soko,
Jana kituo cha EATV nacho kilirusha hewani kipindi kinachohusiana na mambo hayohayo kadhalika yule Mganga wa jadi anayejiita Profesa sikuona alichofafanua hadi mtu akaelewa haswa Freemason ni nini zaidi ya kueleza habari zake za majini na kwenda kuzimu.

my take: Media kuweni makini mnapowaita wageni kutoa ufafanuzi wa mambo yenye utata katika Jamii
 
Naunga mkono hoja.

Pia TBC Taifa nao wangalie sana. Kila Jumamosi wanarusha kipindi cha afya kwa jamii kuanzia saa 3-4 asubuhi. Hapo wanaalika eti 'madaktari' wa tiba mbadala kuelezea magonjwa mbalimbali ya binadamu na jinsi wanavyoyatibu. Ukiwasikiliza 'madaktari' hawa, unagundua kuwa wamedandia fani na ni hatari sana kwa afya za Watanzania.
 
kinachonitatiza ni hizi media both TV na Radio kuwa na program zinazofanana in 24 hrs..sasa sijui program manager wao ni mmoja?au ni kuigana kusiko na tija?..au ni vilaza?yaani kuna vipindi vingine mtu mpaka unazima radio jinsi vinavyoboa kusikiliza...coz havielimishi wala haviburudishi chochote kwa msikilizaji!..aaaagggrrr
 
Uhuni mkubwa!
Hiva majuzi kulikuwa na kipindi kilichorushwa katika ktuo cha televisheni cha Clouds kilichohusu Ukweli kuhusu Freemasons, kwa kifupi wageni waalikwa ktk kipindi kile hakuna chochote walichofafanua wakaeleweka zaidi ya kububuja maneno tu na inavyoonekana ni kama waganga wa kienyeji wamekwenda kujitangazia soko,
Jana kituo cha EATV nacho kilirusha hewani kipindi kinachohusiana na mambo hayohayo kadhalika yule Mganga wa jadi anayejiita Profesa sikuona alichofafanua hadi mtu akaelewa haswa Freemason ni nini zaidi ya kueleza habari zake za majini na kwenda kuzimu.

my take: Media kuweni makini mnapowaita wageni kutoa ufafanuzi wa mambo yenye utata katika Jamii
 
Naunga mkono hoja.

Pia TBC Taifa nao wangalie sana. Kila Jumamosi wanarusha kipindi cha afya kwa jamii kuanzia saa 3-4 asubuhi. Hapo wanaalika eti 'madaktari' wa tiba mbadala kuelezea magonjwa mbalimbali ya binadamu na jinsi wanavyoyatibu. Ukiwasikiliza 'madaktari' hawa, unagundua kuwa wamedandia fani na ni hatari sana kwa afya za Watanzania.

umeona mkuu... yaani wanahatarisha hatma ya wanajamii wa taifa hili coz asilimia kubwa ya watu wetu hawana maarifa ni rahisi kwa wao kuamini kila jambo especially wanapoona limeoneshwa kwenye vyombo vya habari.
 
wanajali kuongeza wigo la wasikilizaji,bila kujali vipi wanaliathiri taifa kwa kupandikiza mawazo yasiyo ya kweli!
 
...Freemasons sasa imekuwa ni Habari ya kuuzia magazeti ya Udaku na VibuyuWazi wachache wasiojua chochote kuhusu society hiyo ndipo wanapotafutia ujiko na ulaji. Wenyewe walikuwa wanajiunga kwa siri sasa kila mhuni anayetaka kujiongezea maujiko feki anatangaza kwenye magazeti ya udaku kuwa na yeye ni Freemason! Ukimuuliza swali rahisi tu la nini society hiyo inachosimamia , anang'aa macho, hana moja! halafu Vyombo vyetu vya habari navyo vimeingia mkumbo huo kwa vinawaita studio watu kama hawa kuelezea kuhusu Freemasons, kama yule jamaa pale Posta mpya anayeuza DVD zisemekanazo kuwa na mambo yanayofanywa na Freemasons wakati picha nyingi amezinyonya kwenye website mbali mbali mtandaoni. Usanii kila mahali.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom