Vyombo vya habari acheni unafiki

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,643
33,427
Hakuna coverage ya maana kuhusu tukio la Arusha.Bila mtandao kama JF hakuna chombo cha habari kinachotoa updates live ktk tukio hili zito kabisa na mbaya zaidi baadhi ya magazeti yameipa uzito mdogo na wengine hawajaiandika.
Huu mtindo wa kutoshikamana seriously pale swala zito kama hili linapotokea hatutamaliza tatizo kama hili.
Nashangazwa na jinsi vyombo vya habari vinavyo react taratibu while wao pia ni waadhirika wa huu upuuzi.
Hivi ingekuwa hata Kenya Citizen wangekuwa wanarusha vipindi vya kawaida kama TV zetu sasa hivi?
Tunahujumiana alafu baadae mnataka mshikamano huu ni unafiki.
Angalizo:
Taifa Stars leo mfunge vitambaa vyeusi pia kuwe na dk 3 za ukimya.
 
Bila vyombo vya habari kusimama haya yataendelea maana wao ndio wanaopaswa kutoa habari tena za uchunguzi ili kutupa ukweli.
 
jana ITV walifanya kitendo cha unyama sana kuhusu suala la watanzania kuuwawa. wameripoti kinafiki na kupotosha eti wamejeruhiwa watu saba huku wakifahamu kuwa kuna watu wamekufa. Isitoshe wamemrusha Nape kwa kusema CDM ni wafanya fujo. Ndio maana hawa jamaa na MCT wao wanakatwa vidole kumbe ni wanafiki wakubwa!!!
 
wamiliki wa vyombo vya habari wanalinda maslahi kwa kuichukia CHADEMA. nimeona live wafuasi wa CCM wakichekelea tukio hili...
 
Namimi pia nmeliona hili, nadhani tz bado tuna safar ndefu ya kufika kwenye demokrasia ya kweli kwa kuzingatia zle "democratic principles" ambazo zote tunazionja tu bila kuzila!
 
Mkuu, umesahau kwamba kuna vyombo vya habari na habari za vyombo? Vyombo vya habari ni taasisi huru na hutumikia umma lakini habari za vyombo ni mfumo kandamizi ambapo umma utaona,kusikia au kusoma habari ambazo chombo husika kinazipenda na zina maslahi kwao!
 
Vyombo vya habari nahisi na vyenyewe vinaiogopa ccm, sijui vimesahau kuwa viko huko isipokuwa tbc
Au ni mpaka yawakute waandishi wa habari ndio watangaze
 
Hakuna coverage ya maana kuhusu tukio la Arusha.Bila mtandao kama JF hakuna chombo cha habari kinachotoa updates live ktk tukio hili zito kabisa na mbaya zaidi baadhi ya magazeti yameipa uzito mdogo na wengine hawajaiandika.
Huu mtindo wa kutoshikamana seriously pale swala zito kama hili linapotokea hatutamaliza tatizo kama hili.
Nashangazwa na jinsi vyombo vya habari vinavyo react taratibu while wao pia ni waadhirika wa huu upuuzi.
Hivi ingekuwa hata Kenya Citizen wangekuwa wanarusha vipindi vya kawaida kama TV zetu sasa hivi?
Tunahujumiana alafu baadae mnataka mshikamano huu ni unafiki.
Angalizo:
Taifa Stars leo mfunge vitambaa vyeusi pia kuwe na dk 3 za ukimya.

Vyombo vyenyewe unavielewa lakini Mkuu? Kuna watu mle wanajiita waandishi wa habari kwa sababu tu wanaweza kuminya batani la kupiga picha na kamera. Hapo sasa ni mtu kabangaizabangaiza kapata vihela kanunua kikamera cha elf 50,000 tayari keshakuwa mwandishi wa habari.

Wengine wanajiita waandishi wa habari kwa sababu mjomba alibangaiza vihela akafungua kibiashara cha gazeti. Hakuna waandishi wa habari Tanzania! We umesikia wapi waandishi wanawadai watoa habari hela kuandika habari. Pale Arusha kwenye lile bomu nani angewapa bahasha ya elf 20,000.
 
Vyombo vya habari nahisi na vyenyewe vinaiogopa ccm, sijui vimesahau kuwa viko huko isipokuwa tbc
Au ni mpaka yawakute waandishi wa habari ndio watangaze

tatizo sio kuogopa mtu mkuu, tatizo ni ukilaza tu uliopo kwenye hivyo vyombo mkuu. maneno unayoweza kuyasema kuhusu vilaza waliopo katika jeshi la polisi ndo hayohayo unaweza kuyasema kuhusu waandishi wa habari tanzania. kuna form four felia mule, kuna fom six felia mle, na wachache waliochukua masomo chuo kikuu ambayo hayana soko jingine zaidi ya umbea. hakuna waandishi wa habari tanzania.
 
Mkuu wala usishangae sana, siku ya jana Tv na radio za bongo nyingi zilillipwa pesa ya kutosha na CCM ili kufanya coverage ya propaganda za CCM, na magazeti ya leo pia walishalipwa kufanya hilo.
Ninao ushahidi juu ya malipo hayo ya CCM.
 
Da. Aiseee....aibu! Kule Iraq bomu moja likilipuka na hata mtu mmoja tu akifa vyombo vyote vya habari vya kiamerika vinafanya habari kuu.

Jana Arusha watu watatu wamekufa na rundo wamejeruhiwa. Hii ni international main story na haipo kokote kama habari Kuu?

Aibuuu.......mungu wangu. hii nchi kweli ni nchi ya vilaza.....
 
chombo cha habari hapa TZ kutoa update za tukio wanategemea msemaji wa jeshi la polisi,mana TCRA wanawafinya kinouma,wanatozwa fain kila siku ndo mana wanakuwa waoga
 
Ata Star wamejitahidi sema wenzangu na mie TBC kama kawaida..!!!!

hi TBC cjui inaumuhimu gan kwa waTZ mana chombo cha habari cha wananchi kam kinabakinyuma kutoa habari kama ya arusha kuna walakini,,,,yan Enzi za Tido pale TBC ilikuwa ful update,sas uyu wa sas sijui ananini?
 
Wamiliki wa vyombo vya habari wengi ni makajanja, tabia yao ya kuficha habari kwakisingizio zitachochea uvunjifu wa amani, zinanikela sana, wakati nchi hii ishaoza
 
Hakuna coverage ya maana kuhusu tukio la Arusha.Bila mtandao kama JF hakuna chombo cha habari kinachotoa updates live ktk tukio hili zito kabisa na mbaya zaidi baadhi ya magazeti yameipa uzito mdogo na wengine hawajaiandika.
Huu mtindo wa kutoshikamana seriously pale swala zito kama hili linapotokea hatutamaliza tatizo kama hili.
Nashangazwa na jinsi vyombo vya habari vinavyo react taratibu while wao pia ni waadhirika wa huu upuuzi.
Hivi ingekuwa hata Kenya Citizen wangekuwa wanarusha vipindi vya kawaida kama TV zetu sasa hivi?
Tunahujumiana alafu baadae mnataka mshikamano huu ni unafiki.
Angalizo:
Taifa Stars leo mfunge vitambaa vyeusi pia kuwe na dk 3 za ukimya.

Tv zilizobaki TZ ni star tv,ch.10,itv na eatv zingine MAGUMASHI 2,yan hawaelewek
 
Back
Top Bottom