Vyombo vya dola vipo kwa ajili ya nani?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyombo vya dola vipo kwa ajili ya nani??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by msnajo, Jul 18, 2012.

 1. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Wakuu salaam.

  Naomba tujadili kama GT. Tuweke tofauti zetu za kiitikadi pamoja na vyama pembeni.
  Vyombo vya dola hasa mahakama na polisi, wapo kwa ajili au faida ya nani?? Je, ni sisi wananchi au ni wenye uwezo, au watawala? Nimelazimika kuleta huu mjadala kutokana na ukandamizaji na uonevu unaofanywa na vyombo husika kwa wananchi ama waliomaskini au wasiokuwa watawala. Mara nyingi kwa watu wa kawaida (ordinary people) wanapofanya makosa, polisi wanawakamata "fasta" na watuhumiwa nao wanakamatwa "fasta" itakapodhibitika hawana hatia wanaachiwa huru. Mfumo huu umejikita kwa watu wachini! Kwa wakubwa hasa watawala na wenye uwezo wa fedha, polisi wamekuwa wakijishauri kumkamata mtuhumiwa au kuacha kabisa hata kuzungumzia habari zake ili kumlinda. Huyu "Ahmed Msangi", (I dont wish to know him) ametajwa sana kwenye swala la uhalifu wa kumteka na kumjeruhi Dr Uli. Masikitiko yangu, kama ni mtuhumiwa kwa nini polisi wasimhoji walau kuupata ukweli? Huyu Kova, huu mchezo wa kudanganya watanzania, kwa nini asimdanganye mkewe na watoto wake ili kufanikisha mambo fulani kwa faida ya familia yake? Iramba kumetokea fujo na mtu mmoja karipotiwa kufa, kuna watuhumiwa saba kati ya kumi na mbili inasemekana wametoka Dar na wamelipwa ili kuweza kuleta madhara. Cha kushangaza hawajahojiwa pamoja na kwamba kinadharia wanaonekana kuhusika kwa namna moja au nyingine katika fujo zile. Badala yake unapikwa uwongo na kuwahoji watu wa chama fulani ili kuwabambikia kesi! Kwa nafasi yangu kama Mtanzania, haya ndo mambo nina uhakika kwamba yatatowesha amani yetu. Watanzania tumechoka kuonewa na vyombo vya dola, je vinamtumikia nani? Mahakama nazo zinapindisha kesi ili kuwa-favour watu fulani, wanamtumikia nani? Serikali kama chombo kinachotawala watu hakioni umuhimu wowote wa kujali wananchi/watu wake, hata kama wanateseka "no problem" watajua wenyewe!! Wenye uwezo wa kudai haki wanauawa au kujeruhiwa vibaya, wananchi nasi tunatazama. Lakini ni hadi lini? Bob Marley aliwahi kusema "how long shall they kill our prophet while we stand side and look". Tujiulize, serikali na vyombo vyake vya dola vipo kwa ajili ya nani??
  Hebu tupeane hoja.
   
 2. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  chukua hatua mkuu kwa kuanza kuchukua fomu za uongozi ili wakulinde. vyombo vya dola husubiri amri tu ndugu.
   
 3. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Cant be an idea! Thank you
   
 4. m

  mbukoi JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 253
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kaka nimekuwa na mawazo yanayokaribia kuwa sawa na yako kwenye hili na nimeona wazi tunayo fursa ya kuchukua hatua ya maboresho ya muda mrefu kupitia katiba mpya kama hatutatoa maoni juu ya muundo wa dola kwenye hii katiba mpya haya maswali yatabaki bila majibu kwa vizazi vingi vijavyo lakini tukipeleka maoni tunayoona ni sahii kwenye hili jambo tutaikomboa nchi yetu na haya malalamiko hayatosikika tena kila mtu atatendewa haki kwa uongozi wa katiba mpya.
   
 5. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  kwenye mfumo wowote wa utawala jukumu la vyombo vya dola ni kuwalinda watawala kwa gharama yoyote ile.
   
 6. B

  Bob G JF Bronze Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  watanzania tumekuwa kama makondoo 2, hata tungeambiwa tulipie hewa hii ya mungu tungelipa 2 hata kama ni mafukara! tumefanya taasisi zote za umma kuwa mali ya ccm na mafisadi, lakini ujinga una muda unakwisha, tutafukua hadi makaburi kwa wote waliofilisi na kutumia vibaya madaraka yake
   
 7. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  wacha pressure time will tell.
  Remember: YOU CAN FOOL ALL PEOPLE ONE TIME, BUT YOU CAN'T FOOL PEOPLE ALL TIME.

  Also know that THEY WATCHES, BUT WE HAVE TIME by Taliban.
   
Loading...