Vyeti vyangu vina majina mawili, NIDA ina majina matatu

uzewela

Senior Member
Jul 29, 2020
119
255
Habari za mida hii wakubwa, naamini kupitia jukwaa hili tunaweza kumsaidia jamaa yangu.inshu iko hivi, alijiunga ajiral portal jina la kati ni la kwenye kitambulisho cha nida ila jina la kati kwenye vyeti ni tofauti na la kwenye nida. Ameitwa kwenye interview ya TPA jumamosi ya wiki hii, afanyeje ili kupata suruhu ya kudumu kwenye ajira nyingine zitakazotangazwa.

Shukran
 
Kwanza: Aambatanishe copy of Certified Deed Poll katika Ajira Portal.

Pili: Kila anavyokwenda interview awe anakwenda na Orijino Deed Poll.
Asante sana chief.hii deed poll anaipata mahakamani au kwa mwanasheria?
 
Halafu mtoa hoja ilikuaje hii hali ikajitokeza?,ni wakati sasa kwa serikali kuwa serious na vitambulisho otherwise DNA ya taifa itapotea, ni LAZIMA tuanze kutoa birth certificates kwa watoto na kinachoandikwa pale kisifutwe kirahisi ili kuzuia matatizo kama haya
 
Nashukuru kwa maoni yenu wadau,tayri ameshalipia ameambiwq asubiri mpaka siku 7 za kazi.
 
Kama anatumia majina mawili mfano, ASHA JUMA (vyeti vyote) na NIDA inasoma ASHA JUMA RWEYEMAMU hii haina hata haja ya viapo vya sijui wizara ya ardhi.
Mfano kwenye nida iwe inasoma ASHA JUMA RWEYEMAMU lakini kwenyevyetivya chuo inasoma ASHA SAID RWEYEMAMU.inshu ndio ilikuwa hapo
 
Back
Top Bottom