SoC01 Vyeti vya utafutaji ni kujituma, subira, uaminifu na kutokukata tamaa

Stories of Change - 2021 Competition

Theb

JF-Expert Member
Jan 25, 2019
3,929
7,268
Habari zenu wana JamiiForums?

Natumaini mpo wazima..? Poleni na tozo za miamala.

Leo nawaletea andiko linaloelezea vyeti vya utafutaji kitaani. Yaani huku vyeti unakua navyo katika kichwa chako na tabia zako na kuishi kwako na watu wa jamii inayokuzunguka. Nitaelezea uvumilivu, uaminifu, kujituma, kuishi na watu wajamii ikuzungukayo vizuri na kujiamini na mengineyo:-

1. Uaminifu

Hapa nitaelezea kivipi uaminifu ni mtaji kwa maisha ya mtaani katika kujitafutia riziki..? Moja uaminifu ndiyo nguzo katika utafutaji maana kama ni wateja watakukumbuka na kudumu na wewe katika biashara yako kwa kuwa muaminifu. Mfano. Kama una genge au banda la biashara yoyote mteja anaweza kuomba kukuachia mzigo wake kwa muda kidgo. Akija akakuta mzgo upo kama alivyooacha ashajiwekea uaminifu na atazidi kukutangaza kwa mazuri kwa wengine na kuitangaza biashara yako.

Tahadhari kamwe usitunze mzigo usioujua au usioona kaweka nini ndani au unauhalali gani hayo lazima uyajue maana waweza achwa na madawa ya kulevya

2. Kujiamini

Hii nayo ni nyenzo au cheti kingine cha maisha ya itaftaji kwa mitaa. Unataka kukopa mtaji kwa mtu lazima ujiamini ndipo utaweza kumuelezea mtu wazo lako la biashara na akakuelewa na kukuwezesha. Pia kujiamini katika shughuli ufanyayo, mfano kama ni kubeba gunia lazima uwe na kujiamini kuondoa kuwaogopa watu kuwa watanionaje.

3. Uvumilivu au subira katika utafutaji wako.

Katika kutafuta riziki lazima pia ujijengee uvumilivu na subira maana hautapata unachokitafuta kwa siku moja au mwezi mmoja. Mfano unafanya umachinga huwezi kuwa tajiri kwa siku moja lazima upitie vipindi vya changamoto nyingi ili kukuwezesha kujifunza na kutunza kidgo kidgo katika kukuwezesha kufikia malengo na mipango yako. Usipokuwa na uvumilivu na subira ndipo vijana tunajiunga na makundi mabaya mfano ujambazi, wizi, kujiingiza kwenye madawa ya kulevya (biashara hatarishi na zisizo halali), dhuluma, utapeli na kujiuza miili kwa wanawake.

4. Kauli nzuri au kuishi vizuri na jamii ikuzungukayo hususani wateja wako.

Katika utafutaji wa riziki mtaani kauli nzuri inamatokeo yake mazuri na mabaya itategemea na kauli yako wewe mtafutaji. Mfano ukiwa unawatukana au kuwakejeli watu lazima upate wateja wachache lakini ukiweza kuwadhamini na kuwaheshimu watu kulingana na mapungufu yao, dini zao, makabila yao, utaifa yao, rangi zao na jinsia zao bila kusahau hali zao za kiuchumi hii itakusaidia kuitwa mtu wa watu na itajusaidia kujipatia wateja wengi watakao kuhubiri kwa wengine kwa mazuri.

Tahadhari
Kuishi vizuri na watu sio kufikia hatua ya kumuamini kila mtu na kukopesha tu kiholela hiyo hapana. Unaishi vizuri na watu kwa kuangalia je wao nao wanajali biashara yako..? Mfano baadhi ya watu wakijenga mazoea watataka uwakopeshe usikopeshe huo ni mwanzo wa migogoro na kukimbiwa na wateja na kuifilisi biashara. Sio kila mtu anakopeshwa. Wakukopeshwa inabidi uwe nao karibu kila siku mnaonana na unajua shighuli zao na unauhakika hatashindwa kukulipa.

5. Huduma bora na kuwajali wateja, kuwashauri na kuwaelezea kitu wasichokijua wakikuuliza kuhusiana na biashara yako unayofanya.

Katika kutoa huduma yako lazima ujue kuwajali wateja lazima ujue kuwasikiliza na kuwaelezea panapo stahili maelezo.

6. Umakini kwa kile ufanyacho.

Hapa kwanza lazima uwe na umakini katika mipango, uchunguzi na usimamizi au kuendesha biashara kwa ujumla. Lazima ujue kipi kifanyike kwa wakati gani na uhitaji gani. Mfano, bidhaa ikipungua lazima ujue na kuleta haraka, pia lazima uwe makini katika kutoa huduma maana sio kila mtu ni mwaminifu ukijisahau unaweza kuibiwa na unakua mwanzo wa hasara.

7. Jiwekee malengo kwa kidogo upatacho, yaani anza kutunza kidogo unachokipata ndipo kitakua kikubwa kadiri unavyotunza.

Kadiri unavyofanya biashara yako inakubidi utunze kile kidogo unachopata maana kidgo hicho ndicho kikituzwa kitakuinua kesho katika malengo ya biashara yako. Usiwe na tabia ya kutumia chote unachopata kwenye utafutaji wako.

8. Punguza matumizi yasiyo ya lazima.

Hapa lazima mtafutaji uangalie matumizi yapi ya lazima kwako na yapi sio ya lazima. Yaliyo ya lazima inakubidi uyatatue na yasiyo ya lazima inakubidi uyaache. Mfano, vijana siku hizi wanacheza michezo ya kubahatisha ,(bet) sana tena kwa hicho kidogo wapatacho. Kwa tabia hiyo kupiga hatua ni ngumu. Japo kwa wanaopata kushinda hiyo michezo wanabadilisha maisha yao lakini sio wote wachezao watashinda hivyo tahadhari muhimu

9. Kuzingatia sheria za mahali ulipo.

Katika utafutaji pia lazima tuzingatie sheria mfano kulipa ushuru au kodi inapohitajika sawa sawa na biashara yako. Ukiwa unafuata sheria mamlaka husika hazitakuwa na kusumbuana na wewe.

Hitimisho

Utafutaji unajengwa na mambo niliyotaja hapo juu kitabia uwe na mtaji na pia kwa wasio na mitaji lazima ujue na uzingatie hayo niliyoorodhesha hapo juu. Na zaidi juhudi, kujituma, ubunifu na kujutambua ni mengine pia yanayomwezesha mtafutaki yoyote yule katika utafutaji wake
 
kwa pamoja tusome hili na tupige kura kubwa zaidi tujifunze
 
Back
Top Bottom