Vyeti Vya Ndoa Vichanwe?

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,720
Wana JF,

Kuna hii kitu nataka kushea na nyie.

Watu wote waliooa, waumini wa dini zote wanakutana na rabsha na matatizo mbalimbali katika maisha yao ya ndoa, na matatizo mengine hufikia hatua mbaya(irreparable) na kusababisha kuachana kwa wanandoa(Mungu pishia mbali).

Na ikumbukwe kwamba couples zote zinapofunga ndoa zinapata cheti cha aina moja cha kiserikali (kwa Tanzania).

Swali langu linakuja hivi, je ndoa inaposhindikana, na wanandoa wakaamua kuachana pasipo uwezekano wa kurudiana, kwanini kile cheti cha ndoa hakichanwi ili kuthibitisha kutengua ndoa husika?

Je haihofiwi kwamba kinaweza kutumika kinyume na ndoa iliyovunjika?...
 
MKUU, mi sioni wapi ulipo wasiwasi wako.

kimsingi ile hati rasmi ya talaka itolewayo na mahakam, "hukichana" kile cheti cha ndoa na kukifanya kutokuwa na nguvu kisheria. hivyo kama mtu atakitumia baada ya talaka si vibaya kama malengo ni mazuri, mfano mtu anataka kufamya kumbukizi ya maisha ya ndoa ama kutoa usia, ama kuthibitisha ndoa ile japo ilishavunjika kwa minajili anuai ya kisheria.

k\wa kifupi kukichana kwa mikono kitu ambacho tayari kimechanwa kisheria ni hasira za kijinga!
 
Wana JF,

Kuna hii kitu nataka kushea na nyie.

Watu wote waliooa, waumini wa dini zote wanakutana na rabsha na matatizo mbalimbali katika maisha yao ya ndoa, na matatizo mengine hufikia hatua mbaya(irreparable) na kusababisha kuachana kwa wanandoa(Mungu pishia mbali).

Na ikumbukwe kwamba couples zote zinapofunga ndoa zinapata cheti cha aina moja cha kiserikali (kwa Tanzania).

Swali langu linakuja hivi, je ndoa inaposhindikana, na wanandoa wakaamua kuachana pasipo uwezekano wa kurudiana, kwanini kile cheti cha ndoa hakichanwi ili kuthibitisha kutengua ndoa husika?

Je haihofiwi kwamba kinaweza kutumika kinyume na ndoa iliyovunjika?...
hahaha!
swali zuri sana
majibu ni mengi pia
hatuchani vyeti:
-for our records
-hata tusipo chana bado ndoa inatambulika imevunjwa-(kuna talaka/devorce)
-kuna baadhi ya madhehebu ndoa huwa HAITENGULIWI-(serikali ililiangalia hilo pia)
-kuchana/kutochana haileti maana WALA HAIPINDISHI UKWELI
 
Geoff
Nimeongelea generally, but broda, kwa aina ya ndoa unayoingia wewe(bolded above), sahau kabisa kuachana broda!

Piga ua, ni lazima mwisho wa siku mpatane na kushea kitanda...lol!
 
Mi hufikiria sana juu ya swala hili alafu mtu amekula kiapo aidha kanisani au msikitini lakini baada ya muda flani anakiuka kile kiapo naona ni bora cheti kichanwe kama zinavyo chanwa leseni barabarani pindi unapo kwenda kinyume na sheria.
Ndoa za uzeeni ni ndoa bora na imara na zinadumu maana baba na mama wanakuwa wamepita katika misuko suko mingi na sasa wana amua kutulia na kuishi pamoja kama mke mmoja na mme mmoja.
 
jamani kikishachanwa mahakamani inatosha jamani mahakamani mnapewa talaka kuonyesha akuna ndoa tena mm naona inatosha na tangu siku mliposhindwana wawili tayari mlishachana vyeti wenyewe kwani mmesaliti viapo mlivyoapa
 
Swali langu linakuja hivi, je ndoa inaposhindikana, na wanandoa wakaamua kuachana pasipo uwezekano wa kurudiana, kwanini kile cheti cha ndoa hakichanwi ili kuthibitisha kutengua ndoa husika?
Mkuu unafikiria mbali sana wewe
Au hata kukichoma moto au kukitia maji kikalowana

Ila swali la msingi je ndoa ni cheti cha ndoa au ni nini? Jibu tafadhali
 
Mkuu unafikiria mbali sana wewe
Au hata kukichoma moto au kukitia maji kikalowana

Ila swali la msingi je ndoa ni cheti cha ndoa au ni nini? Jibu tafadhali

cheti ndio kinawaaapa vicha ma wife, hata hivyo kukichana ni kazi bure, kwani talaka ilishamaliza kazi!!!!!!!!!!!!!! yoooooooooooooooooooote!!
 
Mkuu unafikiria mbali sana wewe
Au hata kukichoma moto au kukitia maji kikalowana

Ila swali la msingi je ndoa ni cheti cha ndoa au ni nini? Jibu tafadhali
Ndo si cheti cha ndoa, bali cheti cha ndoa ni SEAL ya ndoa!

Yaani mtaongea kila lugha ya kupendana wee, lakini mwisho wa siku lazima kuwe na something tangible(machoni pa wanadamu) kwaajili ya kuhitimisha maridhiano ya ndoa, nacho ni cheti!

Kama kwa mioyo watu watakuwa wameachana na kuapa kutorudiana, kunakuwa na ugumu gani kuchana vyeti?

Mi nishaona watu walioshindana kabisa wakigawana vile vyeti vya ndoa, (maana hutolewa viwili!), nikajiuliza badala ya kuvi'dump wanahakikisha wamevipack vizuri kwenye mabegi?

There is something behind these vyetis!
 
Yaani mtaongea kila lugha ya kupendana wee, lakini mwisho wa siku lazima kuwe na something tangible(machoni pa wanadamu) kwaajili ya kuhitimisha maridhiano ya ndoa, nacho ni cheti!
kwa mfano kama sitaki je na mwenzangu hataki je? kuna ulazima?
 
kwa mfano kama sitaki je na mwenzangu hataki je? kuna ulazima?

Kama hamtaki vyeti mtamshawishi nani kwamba mnaishi katika ndoa?

Na itafungishwa na nani?..Kasisi gani wa hivyo?
Wazazi gani?...Nchi gani..Sheria gani?

Na shida ni kwamba ILI IWE NDOA ni lazima iwekwe hadharani machoni pa wengi, au hata wachache, lakini cheti ni kipengele kimojawapo!

Hakuna njia ambapo unaweza ukatangaza boldly kwa watu kwamba unaishi kwenye ndoa wakati huna cheti!...hakuna!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom