Vyeti vya Kuzaliwa kabla ya Ndoa: Rais Magufuli ALIFUTA agizo la Waziri Mwakyembe

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
ca641427b062619ef8be03a0a2bef46b.jpg


Rais Magufuli leo amelifuta agizo la Waziri Harrison Mwakyembe linalotoa sharti la kuwa na cheti cha kuzaliwa kwa wote watakaofunga ndoa kuanzia Mei 1, 2017.

Swali:
Je, Waziri Mwakyembe hakuwa amewasiliana na bosi wake kabla ya kufikia uamuzi ule?

Mawazo yangu:
Nahisi Waziri Mwakyembe alilengeshwa na ''mfumo" katika hili na akaingia "chaka" na sasa imeshapatikana sababu nzuri kabisa ya kumtumbua ili mteule mpya wa Magufuli, Prof. Kabudi kuendesha Wizara hiyo.

Note: Kumkata kichwa kobe yataka timing

 
Rais wa JMT mh JPM amekatisha agizo lililotolewa jana na waziri wa sheria Harrison Mwakyembe la kuoa/kuolewa mpaka uwe na cheti cha kuzaliwa


  • "tatizo la kupata cheti cha kuzaliwa ni gumu kila mtu anajua tukifanya hivyo tutawakosesha fursa watanzania ya kuoa au kuolewa" JPM

ukitenga watu tunatengua yangu macho
 
Wakuu habari imedondoka.. Leo mpya Mh. Rais amefuta agizo la ndoa bila vyeti
e89036eb31a0a6def65afe3ea8b84763.jpg

Naona Mh. Mwakyembe ameahindwa kujua issue ya vyeti kwa sasa ni tatizo. Asante Rais wangu mpenzi nazidi kukuombea.*****
Hivi waziri kutoa tamko na Mh. Rais kulifuta inaashiria nini au mawaziri hawana washauri? Nisaidieni jamani
 
serikali ya mkurupuko hii,hapo kuna tatizo kubwa sana kwenye uongozi.........
huyu mwakiYembe ndio kila uchao anatishia kuifuta TLS ......
kuna viongozi nimekuwa nao kwa ukaribu kwenye kazi za serikali NI WASANII na wapiga dili tu hawana uzalendo na mabingwa wa kujipendekeza ,wafitini mmoja wao ni huyu wwa sheria na katiba.
serikali inaongozwa kwa sheria sio matamko na kutafuta umaarufu
N.B naomba vyeti vya Daudi Bashite viwekwe mezani
 
Back
Top Bottom