Vyeti bandia vinaweza kuondoa wafanyakazi wengi Wizara ya Afya!

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,266
2,000
ilo ndo tatizo la kuamini vyeti 100% badala na kuwapima na wenye hvyo vyeti ktk field

izzo,kwenye field ndiyo kwenye uhalisia na uwezo wa mtu kufanya kazi kazi anayoisomea,alama A,B,C,D,...F hizi ni pongezi tu za muda mfupi.
 

Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
6,815
2,000
Huku ni sawa na kuingia porini na kuanza kukimbizana na sungura hadi ukija kumkamata huko hoi, wakati mjanja anaweka mtego wake anendelea na shughuli zake anajua tu wingi wa sungura ataingia mmoja tu mtegoni mida ikifika anaenda kuchukua tenga lake na sungura ndani taratibu.

Matatizo serikarini ni mengi sana na uzembe unachangiwa na sababu nyingi sana sio wenye veti feki tu, wengine wanazo kabisa shahada za ukweli lakini performances zao ni below par vile vile.

Kwanza kama mtu anafanya kazi na cheti na feki ina maana HR department aiko makini kwenye ku-assess skill knowledge and attitude za nafasi zao kwa hivyo hicho kitengo kina stahili adhabu pia kuweka watu feki ndani wakiwa na majukumu ya kupangaa timu za tasks.

Sasa katika zama hizi za kubana matumizi serikari lazima itafute cost effective way za kutatua matatizo kama haya kwa pamoja badala ya kuzungukuka zunguka kwenye taasisi zake na kuanza kuchunguza vyeti nafikiria kuna kupiga simu and the likes kwanza the whole processes is time consuming and expensive. Hila ukiweka malengo ya kazi na task zikajulikana based on code of conduct, professionalism and expectations on quality of services kila kitu rahisi.

Mjomba nchi za wenzetu huyo CQC regulator wa quality za afya akifika kufanya uchaguzi yeye anatembea na karatasi lake tu na kufanya observation za kazi, kuongea na wateja kwenye mawodi, kuangalia mazingira ya sehemu kinachofuata ni ripoti kama feedback kutoka kwa wateja kuhusu maswali ya huduma ni tofauti na malengo wanayotegemea na behaviour za manesi au wafanyakazi tofauti zitawekwa, kama mazingira ni machafu tofauti na government expectations ni tofauti zitawekwa, kama hospitali aina rekodi sahihi za wagonjwa na jinsi inavyowaangalia kama framework itawekwa, kama observation ya wafanyakazi airidhishi itawekwa na yote ambayo government inatarajia. Kopi anakabidhiwa MD, kodi wizarani na kopi inabandikwa wateja na familia zao wajue.

Baada ya hapo kinachofuata ni mapendekezo tu na lazima yaanzie juu kushindwa kutimiza malengo ya serikari hayo ya wafanyakazi ni kama sehemu ndogo sana yaripoti sana sana watasema walikuwa awafanyi abc but then ni jukumu la management na HR kuhakikisha kuna supervision sahihi kufikia malengo ya serikari ie including hiring people with skills matches.

Kwenye mapendekezo kama management ina bahati kutokana na makosa madogo madogo inaweza pewa muda wa kubadirisha mazingira, kama ni makosa yaliyopitiliza management watataa ibadilishwe na kama ni kituo binafsi kinachopokea hela za serikari watasema kifungwe kabisa.

Alikadhalika makosa mengine ya yanayo pelekea loss of life kisa kutofuata procedures au daktari sijui kumfanyia mtu operesheni kwa magonjwa ambayo angeweza pata matibabu mengine sio kwamba yana fines bali unafungwa kabisa manager na mfanyakazi aliyehusika thats what they call accountability sasa kama kuna menejimenti yenye akili timamu sidhani kama kuna mtu anaweza weka mtu asiye na qualification kwa sababu the consequences are real na wenyewe wanafanya appraisals all the time ata kama una cheti uwezi kufanya kazi kwa quality wanazotarajia kibarua kinaweza ota majani but then kufukuza watu ni expensive sasa kwanini uajiri wasio na kiwango in the first place mtu kama huyo kama uwezi kumfukuza kila siku inabidi umpeleke training again it cost money too na ataa ukimfukuza na kuajiri mpya it cost money too kumfundisha taratibu za kazi this is why the HR department is crucial to success of any organization.

Kinachoitajika ni ubunifu sio kukurupuka
 

izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,814
2,000
izzo,kwenye field ndiyo kwenye uhalisia na uwezo wa mtu kufanya kazi kazi anayoisomea,alama A,B,C,D,...F hizi ni pongezi tu za muda mfupi.

mkuu askari bora ni yule anaefanya vizuri na kushinda ktk uwanja wa kivita si yule anaefanya SHOW OFF uwanjani kwa kupasua matofari kwa kichwa 2mekuwa na tatizo la kuwapima wasomi wetu kwa show off za vyeti c ktk field za kazi na utendaji wao na ufahamu wake unalingana na GPA ya cheti?
 

swagazetu

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
4,098
2,000
Hakuna upungufu utakaotokea vyuo viko vingi na wahitimu ni wengi sema labda wazoefu watapungua.

Ktk sekta yenye watu feki waliotumia vyeti feki ni Polisi na Afya.
 

swagazetu

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
4,098
2,000
mkuu askari bora ni yule anaefanya vizuri na kushinda ktk uwanja wa kivita si yule anaefanya SHOW OFF uwanjani kwa kupasua matofari kwa kichwa 2mekuwa na tatizo la kuwapima wasomi wetu kwa show off za vyeti c ktk field za kazi na utendaji wao na ufahamu wake unalingana na GPA ya cheti?

A good tactical personal must be both Knowlegeable and practical.
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
20,851
2,000
Hakuna upungufu utakaotokea vyuo viko vingi na wahitimu ni wengi sema labda wazoefu watapungua.

Ktk sekta yenye watu feki waliotumia vyeti feki ni Polisi na Afya.

Hata wizara nyeti Kama wizara ya ulinzi napo vimejaa tele.
 

BINARY NO

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
2,054
2,000
Mh.....jamani kwan sisi wenye vyeti feki tunawazuia nyie msipate kazi au mishahara?
Kwahiyo Tukitumbuliwa MAJIPU yetu nyie ndo mtaongezewa mishahara?
Sijui nika reseat ila Basic mathematics itanifanya tena.....
 

habari ya hapa

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
12,795
2,000
Hii tabia imezaliwa na kulelewa na chama cha matamko na serikali yake tukufu, mambo ya hovyo yanafanyika utadhani hakuna serikali, hapo hakuna wa kulaumiwa,
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
20,851
2,000
Tanzania kuna wasomi Feki kuliko Nchi zote Duniani ikija top 10 ya Nchi zenye wasomi wasomi magumashi Tanzania itaongoza Kwa miaka yote .
 

habari ya hapa

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
12,795
2,000
Tanzania kuna wasomi Feki kuliko Nchi zote Duniani ikija top 10 ya Nchi zenye wasomi wasomi magumashi Tanzania itaongoza Kwa miaka yote .

Kwani tushai ingia hiyo top ten kwa jambo lolote, labda siku sikia mwenzenu
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
20,851
2,000
Hii tabia imezaliwa na kulelewa na chama cha matamko na serikali yake tukufu, mambo ya hovyo yanafanyika utadhani hakuna serikali, hapo hakuna wa kulaumiwa,

Magufuli anaogopa kutumbua Jipu la vyeti maana anajua itakuwa Aibu kutokana na baadhi ya viongozi wakubwa Serikalini kumiliki vyeti feki huku wengine wakiwa ni Marafiki zake na wapiga kura wake.
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
20,851
2,000
Mkuu pole sana, inauma sana wako watu wamesoma wako mtaani wengine wenye vyeti feki wako makazini.
Je kuna madudu mangapi wanasababisha hao wenye vyeti feki??

10%ufisadi na mbinu zote za wizi zimesababishwa na hao hao wajanja wanaomiliki vyeti feki.
 

izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,814
2,000
A good tactical personal must be both Knowlegeable and practical.

mkuu fanya uchunguzi kama utawakuta ambao wako empty sehemu zote bahati mbaya maskini elimu yetu imekuwa ni watoto wetu wakariri ili kupata vyeti na kuajiliwa tu ndio akili za vjana wetu wasome ili wapate vyeti waajiliwe tu sasa tumejikuta tuna vilaza wengi wanaojiita wasomi mabingwa wa kukariri difinition tu mimi nawaita ni wamiliki wa vyeti halali lakini wenyewe ni fake
 

Chosen generation

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
4,380
2,000
hiyo ni kweli, mimi mwenyewe nilishangaa kumuona mtu kakomea form tu ameanza kusomea uuguzi nilipouliza nikaambiwa amegushi vyeti. Na hivi karibuni atamalizia masomo yake akaajiliwe.

kuna watu mtaani wanasugua benchi na walipata elimu na matokeo ya halali afu ajira zimekaliwa na wahuni tu.

wakwanguliwe tu.

maana imefika kipindi watu wanaona kusoma ni kupoteza muda na mali kwa kuwa ajira ni tatizo kumbe kuna watu wanakaa tu stationary na kutengeneza vyeti na kesho wanakuwa wafanyakazi.

wawafagie wote.

hakuna cha kujutia kwa kuwa hata wao wanajua hawastahili kuwepo hapo ila ni ujanja ujanja tu.

Wewe umesomea kozi mojawapo ya afya katika chuo kinachoeleweka? Na umekosa ajira? Nikukumbushe tu, vijana wengi walikimbia masomo ya sayansi na wengi walikuwa wanafeli, sasa ulitegemea serikali ingepata wapi hao wauguzi, ambao ni wengi kuliko kada zingine za afya? Kuwafukuza kazi siyo suluhisho, hao wengi walioko mtaani wako wapi?
 

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,266
2,000
Kutambua vyeti feki inabidi ushirikishe watoaji wa hicho cheti kama kipo kwenye kumbukumbu zao,na kumtambua mmiliki halali ongeza na cheti cha msingi.
 

Mshinga

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,536
2,000
Wewe umesomea kozi mojawapo ya afya katika chuo kinachoeleweka? Na umekosa ajira? Nikukumbushe tu, vijana wengi walikimbia masomo ya sayansi na wengi walikuwa wanafeli, sasa ulitegemea serikali ingepata wapi hao wauguzi, ambao ni wengi kuliko kada zingine za afya? Kuwafukuza kazi siyo suluhisho, hao wengi walioko mtaani wako wapi?

kwa hiyo unataka kumaanisha kuwa serikali iliruhusu watu kugushi vyeti wakasome mambo ya afya kisa wengi wamekimbia sayansi?
 

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,266
2,000
izzo mtazamo wako kuhusu vyeti na namna mtu anavyoitumia elimu aliyoipata ni mzuri sana,lakini tumezoea kuamini vyeti,kazi kwanza cheti baadaye.
 

LOOOK

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,390
2,000
Nyie wenye vyeti halali mmelifanyia nini taifa?

Walicho lifanyia taifa ni kuonesha uaminifu kwa kumiliki vyeti halali kutoka serikalini na ndio wanahitaji fursa zaidi ili waweze kulifanyia mema mengi zaid taifa lao.
 

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,266
2,000
Nikiwa nimehitimu kozi fulani bila kupata cheti,palikuwa na shida ya mtaalamu wa kutatua tatizo lililokuwa linaikabili jamii hiyo.Kutokana mazingira magumu wenye vyeti hawaendi huko. Nikajitokeza kutatua tatizo bila kuwa na cheti hata cha kufoji.Je utaniweka fungu gani?,maana ujuzi ninao na kazi naimudu vizuri mpaka kuwa mfanyakazi bora!.
 

Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
8,440
2,000
Asilimia kubwa ya wafanyakazi Tanzania wana vyeti Feki ndio maana maamuzi mengi yanafanyika ya ajabu ajabu na utashangaa bodi nzima iliyoteuliwa hata na Raisi maamuzi yao ni ya kushangaza sana..ni watanzania wachache sana ambao jina la cheti la shule ya msingi ulikute ndio ilo ilo katika cheti cha chuo..au form four..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom