Vyeti bandia vinaweza kuondoa wafanyakazi wengi Wizara ya Afya!

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,266
2,000
tatizo lipo pale walipogushi vyeti pamoja na kudanganya mamlaka za uajiri kwa kutumia vyeti bandia.

tunataka kuwapeleka mtaani na ujuzi wao wa kugushi.

naona hawakukaguliwa. saizi inabidi wakaguliwe sasa.

Mlitakiwa mkague kwanza cheti kabla hajaanza kozi mjiridhishe.
 

Mshinga

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,536
2,000
kama wakati tunapata uhuru mwaka 61 nchi inamaengineer 3 leo wapo zaid ya maelf lakini hakuna k2 majengo yanaanguka madaraja yanavunjika rami ikinyesha manyunyu tu inabomoka ckia mkuu tuna watu wanaohold vyeti tu c wasomi leo orgnal aiwezi kukaa na fake hata kdg utajua 2 je mtu mmefanya kazi nae miaka 10 yeye anachet fake ww una orgnal lakn umeshindwa kumtambua tena inawezekana kazi zngne yeye ndo anakuelekeza sasa hapo orgnal ni nani wewe au yeye?

kwanza ujue kuwa hizo kazi nyingi mbovu zinasababishwa na hao waliofoji vyeti. MAKANJANJA.

usitake kuwaaminisha watu kuwa wenye vyeti halali ndio wanasababisha kujengwa kwa miundombinu mibovu na majengo mabovu afu wenye vyeti kwa kufoji ndio wanajenga vitu vizuri. Huu ni upuuzi wa hoja.

Kingine unapaswa kujua kuwa kuna makosa ya kitaalamu yanaweza kufanywa na wataalamu yakasababisha ubovu wa miundombinu. Lakini kwa mtaalamu inatokea mara chache ika kwa wasio wataalam ni kawaida kusababisha majanga.

inaelekea hujui taratibu za kazi na ajira.
Kama una cheti feki ni kwamba haustahili kuwepo pale pale. Unaweza kuajiliwa kwa kazi ya kufagia ikulu lakini sharti uwe na elimu halali ya form four. pamoja na kwamba hata asiyeenda shule anaweza kufagia ukigundulika ujue hutakiwi kufanya kazi hiyo.
 

tres bien

JF-Expert Member
Jan 27, 2015
559
500
Wauguzi wanaongoza kwahili wakifuatiwa na kada nyingine za afya . MD feki wengi husingizia wamesoma IMTU. Zoezi la uhakiki kwa watumishi wote linahitajika kwa haraka.
 

izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,814
2,000
yaani upite form four kihalali,form six mpaka chuo afu uwe hujui kuandika barua ya kawaida kuomba kazi? huyo ndio wale wa vyeti feki.

labda kuandika barua kama professional hapo sawa.

mfano huwezi kulazimisha kila aliyesoma Physics,Chemistry na Biology aandike barua nzuri sawa na aliyesoma masomo ya arts.

vyeti feki havitakiwi.

uzoefu kwani si unapatikana kazini. Hao wenye vyeti feki walizaliwa na uzoefu kiasi kwamba wenye vyeti original hawawezi kuwa na uzoefu ama kupata uzoefu.

nashangaa watu kutetea ujinga huu.

Wakague idara zote.

mkuu ucjitoe ufahamu kwan kama unaishi tanzania c jambo la ajabu kusikia m2 kasoma miaka 7 mpaka form one hajuhi kusoma wala kuandika na amefaulu tena shule ya serikali? leo kuna mwanafunz tena wengi tu mpaka anamaliza form four mtiani wa mwisho ajuh ajibu nini mpaka wanachora ronaldo au anaandika mistari ya bongo flava? huyu wa mpaka form one hajui kusoma wala kuandika darasa la 4 kaptaje na huyu wa form 4 je form 2 kaptaje??
 

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,266
2,000
tatizo lipo pale walipogushi vyeti pamoja na kudanganya mamlaka za uajiri kwa kutumia vyeti bandia.

tunataka kuwapeleka mtaani na ujuzi wao wa kugushi.

naona hawakukaguliwa. saizi inabidi wakaguliwe sasa.

Haya ni maajabu kwenye elimu yetu!
 

izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,814
2,000
cteteh vyeti fake ila kama msako unafanyika ufanyike 2 ila nazungumzia hari halisi ya tanzania ilivyo 70% ya watanzania waliopo makazn ni kama fake 2 ila wapo wenye vyeti halali lakini ni fake mkuu Mshinga tanzania tuna tatizo kubwa kuna watu wana vyeti orgnl lakini wao wenyewe ni fake mpaka unaweza kujiuliza hiyo PHD, shahada au dploma kaipataje?? na kuna watu wana vyeti fake lakini wenyewe ni orgnl tena unakuwa huna wasiwasi kabsa na elimu yake nilishawah kufanya kaz kwa mzungu mmoja aliwah kuniambia tatizo watanzania mna trust sana watu wenye vyeti vzr lakn kwenye field m2 unakuta hawez kabsa kazi unakuta m2 ni bingwa wa masoko acordng to vyeti vyake lakini kutwa utamkuta kwa boss wake na kuhuliza maswali au kuomba ushauri je unajiuliza cc tumekuamini na kukupa ofc na tunakupa mshahara lakini kutwa 2nakufanyia kazi yako kwa nn uje uhulize au uombe ushauri wakt ww ni bingwa tena msomi kwa nn ucjiamini kwa maamuz juu ya fani uliyosomea
 
Last edited by a moderator:

Ntaluke.N.

JF-Expert Member
Jun 21, 2015
1,341
1,500
Lakini me bado siamini kama kuna watu huwa wanafoji vyeti tena vya elimu ndogo kama form 4,nilitegemea walau watu wafoji vyeti vya degree au masters!sasa form 4 ni kwamba mtu alikua kilaza namna gan akashndwa kupata hata div 4 ya pts 28 mpaka akahangaike na kufoji cheti?

Wewe inawezekana una vyeti vya kugushi.
 

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,266
2,000
cteteh vyeti fake ila kama msako unafanyika ufanyike 2 ila nazungumzia hari halisi ya tanzania ilivyo 70% ya watanzania waliopo makazn ni kama fake 2 ila wapo wenye vyeti halali lakini ni fake mkuu Mshinga

Mkitaka viaja zaidi linganisheni na vya msingi.
 
Last edited by a moderator:

Mshinga

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,536
2,000
mkuu ucjitoe ufahamu kwan kama unaishi tanzania c jambo la ajabu kusikia m2 kasoma miaka 7 mpaka form one hajuhi kusoma wala kuandika na amefaulu tena shule ya serikali? leo kuna mwanafunz tena wengi tu mpaka anamaliza form four mtiani wa mwisho ajuh ajibu nini mpaka wanachora ronaldo au anaandika mistari ya bongo flava? huyu wa mpaka form one hajui kusoma wala kuandika darasa la 4 kaptaje na huyu wa form 4 je form 2 kaptaje??
ina maana hujui maana ya kugushi ?

hawa wote wapo katika kundi la kugushi vyeti.

kufanyiwa mtihani na kufaulu ni sehemu ya kugushi

nao wakibainika waondolewe tu.

ukibainika hujui kusoma wala kuandika ila umepita unafutwa shule.

na mara nyingi hawa huishia kupata 0 form four na wengine huishia form one ama two.

lakini hawa ni wachache na pengine hawapo kazini.

hawa waliogushi ili kutafutia kazi wanajua kabisa kusomz na kuandika.

ukitafuta asilimia ya walio sekondari hawajui kusoma na kuandika haifiki hata 0.05 ya wanafunzi wote.

ila ukitafuta wanaofeli mtihani form four ni balaa. Mfano 2012 ilikuwa zaidi ya 90 watu wamekula division zero. hawa ndio wanafoji na kuajiliwa kazini.

wakaguliwe tu
 

msem

JF-Expert Member
Nov 7, 2015
1,811
2,000
Idara ya afya inaweza kuongoza nchi nzima kwa wafanyakazi wenye vyeti vya kukugushi! Kuna mtu moja nilimsikia akilalamika kua kuna Muuguzi mmoja pale Muhimbili ana degree ya nursing lakini amereseat mtihani wa form four mwaka huu! Jiulize chuo kikuu aliendaje mpaka akamaliza.

Sio tu kwamba inasikitisha bali inatisha,hata kama kuna mpango wa kufunika kombe mwanaharamu apite kwenye tatizo hili la kugushi vyeti lakini kwenye sekta ya afya ni muhimu sana serikali wakalichukua kwa uzito jambo hili kwa kuwa afya ndiyo utajiri nambari one na hakuna mbadala wa afya.Wapo wanaogushi kwa mtindo wa kubadili matokeo na wapo wanaogushi kwa kutumia vyeti vya watu wengine,na huu ndio mwanzo wa kupasuliwa kichwa badala ya kupasuliwa mguu.
 

Mshinga

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,536
2,000
Hivi wanakagua vyeti feki au watu feki?

hakuna watu feki wewe.

kuna vyeti feki.

ufeki wa cheti unatokana na sababu mbalimbali

mtu kuwa na cheti ambacho hakitoki NECTA bali ni cha kuunda mtaani.

mtu kuwa na cheti feki kinachotoka NECTA ila kafanya mchakato wa kukipata.Ukifatilia details ikiwa ni pamoja na uhalali wa mtu huyo kupita katika shule husika unakuta sivyo. Hicho feki.

Mtu kuwa na cheti cha marehemu. Ni cheti halali kwa marehemu lakini ni cheti feki kwa aliye hai.

mtu kufanyiwa mtihani na kufaulu ama kuiba mtihani nacho ni cheti feki kwa kuwa si stahili yake. Japo huyu kumbaini ni ngumu kama alifanikisha dili.

kwa vyovyote vile ukaguzi wa vyeti ndio sehemu ya kwwnza na pointi ya kuanzia. Mengine yanaibuka baadae.
 

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,266
2,000
Kama ni hivyo waanze upya usaili ukieeleza historia ya elimu yako na vyeti vyake,toka ulikotoka mpaka ulipo.Kama kuna udanganyifu wa cheti au mtu utaonekana tu,pia kumbukumbu zipo kwa watoa hivyo vyeti halisi.
 

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,168
2,000
wataisoma namba.

afu wafanyakazi kama hawa ndio wanasababisha wenzao waumie.

hawa hata ukitokea mgomo wa Madaktari na manesi kudai kuboreshwa maslahi huwa hawadhubutu kushiriki mgomo.

wao wanaenda kazini kama kawaida kwa kuwa ajira ikiondoka ndio kwa heri tena
Una akili kweli, ukiona mtumishi yeyote yule anaogopa kudai haki jua ana cheti fake.
 

Mshinga

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,536
2,000
wakiamua kutract vyeti kwa system mbona watadaka wengi wengi.

NECTA wanasystem tayari.

wakiambiwa wote wawasilishe namba ya vyeti vyao na taarifa za vyeti vyao afu NECTA waingize kumarchisha matokeo wapo watakodakwa kibao. Hasa waliotoa vyeti mtaani.

wanaotumia cheti kimoja zaidi ya mtu mmoja nao wataonekana.

hao wa vyeti vya marehemu utaratibu unaweza kuwa yofauti na wale walionunua vyeti.
 

izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,814
2,000
ina maana hujui maana ya kugushi ?

hawa wote wapo katika kundi la kugushi vyeti.

kufanyiwa mtihani na kufaulu ni sehemu ya kugushi

nao wakibainika waondolewe tu.

ukibainika hujui kusoma wala kuandika ila umepita unafutwa shule.

na mara nyingi hawa huishia kupata 0 form four na wengine huishia form one ama two.

lakini hawa ni wachache na pengine hawapo kazini.

hawa waliogushi ili kutafutia kazi wanajua kabisa kusomz na kuandika.

ukitafuta asilimia ya walio sekondari hawajui kusoma na kuandika haifiki hata 0.05 ya wanafunzi wote.

ila ukitafuta wanaofeli mtihani form four ni balaa. Mfano 2012 ilikuwa zaidi ya 90 watu wamekula division zero.

mfano ni mtoto wa mkwere alipata zero form 4 je unajua alipo nw cku akija utamkuja ana degree nani boss sehem tena unaweza kukuta ni selikarini je huyu utamwitaje mm nahamini katika kuwapima watu vichwani c vyeti tu watanzania 2mekuwa wajanja mpaka kwenye elimu mimi naamini ktk ufahamu si ktk makaratasi a.k.a vyeti
 

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,168
2,000
Wanao resit ni wale ambao walisoma zamani kuna walioanzia medical attendant na wengi assistant nersu kipindi cha nyuma ulikuwa hata secondary ulisoma masomo ya arts au biashara walikuwa naenda kozi za medical isipokuwa ofisa muuguzi au MD.lakini sasa ukitaka kujiendeleza lazima u risiti masomo ya sayansi kwanza hata kama umefanyakazi miaka mingi.ila wakifuatilia vyeti vya form four watakamata wengi sana vya taaluma ni ngumu kugushi mbona unakamatwa mara moja ukiwekewa mtego wa procedure ya kufanya utabaki unatoa macho.

Serikali ilitoa maagizo kwa kada zote kwamba yeyote asiyekua na cheti cha sekondari ajiendeleze,tofauti na hapo watatimuliwa maofisini muda ukifika. Sasa utashangaa mtu anaitwa senior officer hata cheti cha sekondari hana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom