Vyeo vya wabunge /viongozi wa wapinzani bungeni geresha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyeo vya wabunge /viongozi wa wapinzani bungeni geresha?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jombi Jombii, Jun 5, 2011.

 1. J

  Jombi Jombii Senior Member

  #1
  Jun 5, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 186
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana jamii forum Salaam!!!!!!!!!

  Naomba kupata ufafanuzi kuhusu hadhi na kinga ya wabunge wa vyama vya upinzani vs wale wa CCM.Wabunge wa CCM wanapofanya makosa dhahiri wanaachwa au kubembelezwa lakini wale wa upinzani wanadhalilishwa kupita kiasi.Nitatoa mifano miwili kuhalalisha wasiwasi wangu juu ya vitendo hivyo;
  1.Mbunge wa Tarime Bw.Nyangwane amewahi kuwatukana wananchi waliokuwa wanamuhoji jimboni mwake hadharani.
  2.Mbunge wa Busega Dr. Titus Kamani anadaiwa kupanga njama za kumuua Mbunge wa zamani wa jimbo hilo Dr.Chegeni lakini polisi wamesema wamepeleka barua kwa spika wapatiwe kibali cha kumuhoji badala ya kumkata mara moja kama wahalifu wengine.

  Kwa upande wa wapinzani mambo ni tofauti kuanzia kwa Mtatiro wa CUF wakati wakienda kwa Kombani,Juzi tena Mbunge wao wa viti maalum kule Tabora kawekwa lupango bila idhini ya spika.Upande wa chadema wao naona ni kama wanahesabika ni magaidi ndani ya nchi yao kwani Serikali inashindana nayo kila kitu.

  Bila kuweka ushabiki wa kisiasa mustakabali wa nchi hii kwa mashindano haya na upendeleo wa waziwazi ni hatari kwani chuki na visasi vinajengwa kati ya makundi yanayotakiwa kupeana changamoto na kukabiliana nazo kidemokrasia.:majani7:

  Nawasilisha.
   
 2. Bushloiaz

  Bushloiaz JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Sheria za tanzania kiini macho ndugu,siku zote tunaambiwa no one is above the law but magamba people siku zote wako juu ya sheria
   
 3. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,192
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  hilo si liko wazi, hamna cha kuuliza.
   
Loading...