Vyeo vya "Mkuu wa Nchi" na "Mkuu wa Serikali" vigawanywe kati ya Rais na Waziri Mkuu?

Mimi nadhani mfumo wote uliopo sasa hivi ni mbovu sana.Ingekuwa vizuri kama tungekuwa na "ceremonial president"Huyu asiwe na madaraka yeyote katika serikali.Bali tuwe na waziri mkuu atakaechaguliwa kwa kura za watanzania ambae atawajibika moja kwa moja bungeni na kwa wananchi. Hii itatusaidia kuondoa msururu wa viongozi wasiokuwa na tija kiuchumi katika taifa letu.
 
Naunga mkono hoja ili kupunguza madaraka makubwa ya rais hili ni jawabu mojawapo kutenganisha mkuu wa nchi na mkuu wa serikali kama Germany. Au kama hili wazo ni ngumu kutekeleza basi tusiwe na waziri mkuu hana kazi zaidi ya kushauri tu, tuwe na rais na makam watendaji kama US kuliko sasa ambapo waziri mkuu anapewa marupurupu kibao bila kufanya kitu chochote tangible kwa nchi.
 
Sasa hivi vyeo hivi vimewekwa kwa Rais. Yeye ndiye "Mkuu wa nchi" yaani "Head of State" na vile vile yeye ndiye "Mkuu wa Serikali" yaani "Head of Government". Kama mkuu wa nchi ndiye amiri jeshi jeshi mkuu, na ndiyo alama ya umoja wa serikali na alama ya nchi. Lakini kama Mkuu wa Serikali yeye ndiye anayeunda baraza la mawaziri na kuliwajibisha na vile vile ndiye mkuu wa serikali hiyo.

Waziri Mkuu wa Tanzania siyo Mkuu wa Nchi wala siyo Mkuu wa Serikali. Anashiriki kwenye kuunda baraza la mawaziri kwa kushauriana na RAis tu lakini rais ndiye mwenye uamuzi wa mwisho wa kuundwa kwa baraza hiilo na baraza hilo haliwajibiki kwa Waziri Mkuu bali kwa rais. Waziri Mkuu ni kiongozi tu wa "shughuli za serikali" tena ni kiongozi wa shughuli hizo "Bungeni"! Nje ya bunge ni Rais ndiye mkuu wa shughuli hizo na anasaidiwa na rais na waziri mkuu.

Sasa tufanye vipi:

Rais abakie kuwa Mkuu wa Nchi na Amiri jeshi mkuu -na apatikane katika uchaguzi wa kawaida. Atakuwa na madaraka mengine mengi tu yakigawanywa kati yake na Waziri Mkuu. kwa mfano, Rais anateua wale wenye kushika nafasi za kitaifa tu katika Mahakama, Majeshi, na Taasisi nyeti wakati Waziri Mkuu anateua watendaji wa civil service nyingine n.k

Waziri Mkuu awe Mkuu wa Serikali - achaguliwe na wabunge baada ya kupendekezwa na chama chake kilichoshinda uchaguzi wa rais). Akishaguliwa ndiye anaunda baraza la mawaziri na anapeleka majina yake kwa rais kwa kukubaliwa "approval" na rais apewe muda fulani - not more than 7 days - kukubali baraza hilo. Akilikataa mbunge mwingine anapewa nafasi ya ukwa waziri mkuu na kuunda baraza jingine. Akikubaliwa basi Baraza linatangazwa chini ya Waziri Mkuu na baraza hilo litakuwa likisimamiwa na kuongozwa na Waziri Mkuu huku WM akiwa na uamuzi wote juu ya baraza hilo ikiwemo kumfukuza Waziri au kumbadilisha Waziri. Waziri Mkuu akijuzulu, baraza linajiuzulu lakini rais anabakia kwa muda wote wa kipindi chake; rais akiondolewa au akiondoka kwa sababu yoyote Waziri Mkuu anabakia wakati makamu wa Rais anakuwa rais na chama chake kupendekeza jina la Makamu - kama ilivyo sasa.

Kwa kufanya hivyo - Waziri Mkuu atajiwabika kwa baraza aliloliunda yeye na Rais atawajibishwa kwa nafasi yake. Waziri Mkuu ataweza kuulizwa maswali kuhusu mawaziri akiwa na madaraka ya kuwawajibisha mawaziri wake au yeye mwenyewe kuondolewa.

Ulichopendekeza its real should be granted,kumlimbikizia mtu mmoja madaraka kama nchi haina wasomi na wataalamu ni ukiritimba wa madaraka.Ndo maana utaona katiba yetu kuanzia mwanzo inataja rais atafanya hiki ,atafanya kile.Hata hii jeuri inayofanywa na mawaziri kwa Waziri mkuu ni kejeli kwa nafasi yake kwa kuwa tu wanajua hana nguvu kisheria kuwawajibisha zaidi ya kumshauri rais.Na kama wanatekeleza maagizo yenye maslahi na rais ndo hayo yanajiri kuwa hili ni suala la upepo tu.
 
i think jina waziri mkuu libadilishwe maana tumeshashuhudia recently kua PM hana madaraka sana na sio really mkuu wa mawaziri wote yaani boss wao maana nilikua nafikiria kua waziri mkuu ndio boss wao anaweza kuwakemea kumbe hamna kitu i think hili neno waziri mkuu libadilishwe mtu kama huyo awe tu anaitwa kiongozi wa shughuli za serikali bungeni or somethin like that,....i think waziri mkuu is too strong a word..
 
Ni kama system inayofanya kazi Ujerumani, Japan na nchi nyingine, hii inamaanisha kubadilisha kabisa majukumu, mfumo na katiba, lakini pia ni mfumo mzuri kwa sababu utaunda taasisi mbili (ya rais kwa mambo ya nchi au kitaifa kama utapenda na ya uendeshaji wa serikali)

Unapotokea uozo kama ulioripotiwa na CAG hakuna haja ya mtu kutoka brazil hadi dodoma kusema kugundua kuwa ni upepo tu wa kisiasa hapana, waziri mkuu anakua na mamlaka ya kufanya mabadiliko na kuchukua hatua.

mfumo tulionao sisi, rais ni almost dikteta, ungekua mfumo mzuri kama tungekua na kiongozi wa style ya kagame, lakini ni mfumo wa hovyo sana kama tuna rais kama hawa tunaopewa na CCM
 
Back
Top Bottom