Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Sasa hivi vyeo hivi vimewekwa kwa Rais. Yeye ndiye "Mkuu wa nchi" yaani "Head of State" na vile vile yeye ndiye "Mkuu wa Serikali" yaani "Head of Government". Kama mkuu wa nchi ndiye amiri jeshi jeshi mkuu, na ndiyo alama ya umoja wa serikali na alama ya nchi. Lakini kama Mkuu wa Serikali yeye ndiye anayeunda baraza la mawaziri na kuliwajibisha na vile vile ndiye mkuu wa serikali hiyo.
Waziri Mkuu wa Tanzania siyo Mkuu wa Nchi wala siyo Mkuu wa Serikali. Anashiriki kwenye kuunda baraza la mawaziri kwa kushauriana na RAis tu lakini rais ndiye mwenye uamuzi wa mwisho wa kuundwa kwa baraza hiilo na baraza hilo haliwajibiki kwa Waziri Mkuu bali kwa rais. Waziri Mkuu ni kiongozi tu wa "shughuli za serikali" tena ni kiongozi wa shughuli hizo "Bungeni"! Nje ya bunge ni Rais ndiye mkuu wa shughuli hizo na anasaidiwa na rais na waziri mkuu.
Sasa tufanye vipi:
Rais abakie kuwa Mkuu wa Nchi na Amiri jeshi mkuu -na apatikane katika uchaguzi wa kawaida. Atakuwa na madaraka mengine mengi tu yakigawanywa kati yake na Waziri Mkuu. kwa mfano, Rais anateua wale wenye kushika nafasi za kitaifa tu katika Mahakama, Majeshi, na Taasisi nyeti wakati Waziri Mkuu anateua watendaji wa civil service nyingine n.k
Waziri Mkuu awe Mkuu wa Serikali - achaguliwe na wabunge baada ya kupendekezwa na chama chake kilichoshinda uchaguzi wa rais). Akishaguliwa ndiye anaunda baraza la mawaziri na anapeleka majina yake kwa rais kwa kukubaliwa "approval" na rais apewe muda fulani - not more than 7 days - kukubali baraza hilo. Akilikataa mbunge mwingine anapewa nafasi ya ukwa waziri mkuu na kuunda baraza jingine. Akikubaliwa basi Baraza linatangazwa chini ya Waziri Mkuu na baraza hilo litakuwa likisimamiwa na kuongozwa na Waziri Mkuu huku WM akiwa na uamuzi wote juu ya baraza hilo ikiwemo kumfukuza Waziri au kumbadilisha Waziri. Waziri Mkuu akijuzulu, baraza linajiuzulu lakini rais anabakia kwa muda wote wa kipindi chake; rais akiondolewa au akiondoka kwa sababu yoyote Waziri Mkuu anabakia wakati makamu wa Rais anakuwa rais na chama chake kupendekeza jina la Makamu - kama ilivyo sasa.
Kwa kufanya hivyo - Waziri Mkuu atajiwabika kwa baraza aliloliunda yeye na Rais atawajibishwa kwa nafasi yake. Waziri Mkuu ataweza kuulizwa maswali kuhusu mawaziri akiwa na madaraka ya kuwawajibisha mawaziri wake au yeye mwenyewe kuondolewa.