Vyanzo vipya vya mapato vinavyoweza kupunguza mzigo kwa wanyonge

gerit

JF-Expert Member
Jul 16, 2016
307
181
Poleni na MAJUKUMU

Ndugu zangu bajeti ya Leo binafsi nimeona ina dalili njema kwa sehemu hasa ikitekelezwa.

Ingawa bado kama nchi tunakazi kubwa ya kubuni vyanzo vipya vya mapato tena makubwa mfano ni:-

1. Kupunguza gharama za viingilio kuliko majirani katika vivutio vyetu wa watalii. Hili litasababisha tupate watalii wengi na hivyo mapato kuongezeka.

2. Kurasimisha biashara ndogondogo nazo ziingie kuchangia kama walivofanya wakenya hata kama zitachangia kidogo kidogo sabb tupo wengi mwisho yatakuwa mengi.

3. Kubadiri au kuvunja mikataba yote kandamizi na kuingia mikataba mipya yenye tija. Mfano mwekezaji alosema kuna madini ghali namba mbili duniani ila yapo kwenye eneo la gereza, hivyo atatujengea gereza la kisasa sehemu nyingine alafu yeye ataendelea kuchimba hayo madini. Gereza si hilo tunalo kuhamisha gereza? Jambo hilo lina manufaa gani kwetu.

Hii sio sawa na upolaji wa wazi mali ya masikini.

Kama itawezekana ni vema mikataba yote ya non renewable resources mwekezaji apewe 30 % ya thamani hiyo au isizidi 50% na inayobaki iwe mapato ya nchi yetu.

Nchi zilizoendelea kama ni madini wanauza wao sio mtu unamkabidhi shamba lako ulilolima na kupanda mazao ukayatunza hadi yakakomaa alafu ukamwajiri mvunaji (mwekezaji) akavuna gunia 100 , akachukua 99 akakupa wewe1.it's grave sin

Viongoz wetu jua mnadhamana kubwa ya sisi masikini. Kuingia mikataba kandamizi huku ukijua ili upate maslahi binafsi hakika laana hiyo haitakuacha kamwe. Tunaomba wote tuwe wazalendo

Huo ni mtazamo wangu

Na wewe mwenzangu ongezea ili viongozi wetu akiwemo Waziri wa fedha waweze kuyafikiria haya na kuchukua yanayofaa

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom