Vyama vya Wafanyakazi vimeshindwa Kuwatetea Watumishi, Wabunge wasaidieni

kijanamdogo

JF-Expert Member
Feb 25, 2018
231
176
Hakika nimeamini kuwa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania havina msaada kwa Wanachama wao ambao ni Watumishi licha ya kuwachukilia michango yao kila mwezi.

Watumishi wamesimamishiwa upandaji wa Madaraja, waliopandishwa madaraja tangu 2015/2016 hawajarekebishiwa mishahara. Watumishi hawajapandishiwa mishahara tangu 2015 yote hayo vyama vya wafanyakazi vimekaa kimya.

Tunawaomba Wabunge wetu hebu wasemeeni watumishi wa umma.
 
Wabunge wapi hao unaowazungumzia? au hawa wanaoitetea serikali?
Usitegemee chochote kutoka kwa akina Ndungai na kina Tulia, wabunge wa ccm ni sawa wachawi waliomzidi shetani roho mbaya mpaka anawashangaa,
Matumbo kwanza mengine baadae
 
Wabunge wenyewe ndo hao ambao serikali inapotimiza wajibu wake kikatiba wanapagawa na kuruka sarakasi as if hilo jambo ni hisani/huruma ya serikali kufanya. Kama wabunge wanashangilia hivi, ss walala hoi itakuwaje? Usipopiga vigelegele pale serikali inapojenga barabara ni lazima ukutane na “kipigo cha mbwa koko”

Hakuna vyama vya wafanyakazi, ni uchafu tu na kutafuna hela. 15% kutoka 8% bodi ya mikopo wameshindwa kuongea. Nadhani siku serikali ikikataa kulipa mishahara hata kwa miezi 3 mfululizo hapo ndo watajitokeza na kupaza sauti maana akaunti zao zinazotegemea makato kwa wafanyakazi nazo zitakuwa zinasoma 0.

Kidooogo! Labda mh BILAGO (CDM, mb) na mh Zito wanaweza kuongea japo watapingwa na ccm ndani ya bunge. Wabunge wengine wa upinzani mfano Lema na Msigwa labda tuwasubiri wakitweet unabii unaosubiriwa kutimia au nukuu za wanazuoni mbalimbali, lakini suala la kujenga hoja ni sifuri wanachoweza ni ujumbe mfupi mfupi wa majungu tu.
 
Back
Top Bottom