Vyama vya wafanyakazi plus Wafanyakazi wenyewe ni mtaji kwa CCM

ANAUPIGA MWINGI

JF-Expert Member
Apr 14, 2022
389
753
Katika harakati za Kudai uhuru w Tanganyika, Wafanyakazi wali ply part kubwa sana kwa sababu na wao walikuwa na Movement zao zilizo pelekea kupatikana kwa uhuru.

Sio Tanganyika tu bali nchi nyingi hasa za Africa vyama vya wafanya kazi vili fight sana kwa njia mbali mbali kuhakikisha uhuru u apatikana.

Hata Baada ya Uhuru nchi nyingi za Africa still zina Vyama vya wafanyakazi very strong sana, nchi kama South Africa, Zambia, Malawi, Nigeria Kenya, Sudani na Kwingineko vyama vyao vina power sana.

Kenya wana vyama imara saba ndo maana kila mara huwa wanalianzisha.

Tanzania sasa kuna vyama ambavyo ni matawi ya CCM plus Wafanya kazi waoga kuliko hata panya mbele ya Paka, Vyama vyao ni matawi ya CCM, nazani hata chaguzi zao huwa zinasimamiwa na Serikali kabisa.Wafanyakazi ni full waoga haijawahi tokea.Utazania CCM imewapa limbwata.

Kwa Bahati mbaya vyama ni matawi ya CCM na Wafanya kazi ni waogoa mno.

Hawa wafanya kazi wa Bongo kama wangekuwepo enzi za kutafuta uhuru basi tungekuwa still tunatawaliwa na Wakoloni.

Wafanya kazi wamebakia kuandamania kwenye mitandao ya kijamii kama facebook, whatsapp, inst na humu Jamiiforum.

Serikali si kwamba haina pesa za kuwaongezea Mishahara ila ni kwamba wanajua kuna aina gan ya Vyama plus Wanachama wenyewe, Serikali isha soma Upepo zamani sana.

Ni kuhakikishe hata Mishahara isipo ongezwa kwa miaka 20 ijayo hakuna kitu vyama plus Wanachama wanaweza fanya.

Hizo pesa zinazo pigwa zingetosha kabisa kuongeza lakini unawaongezea vipi mishahara watu ambao hawana cha kufanya, sio hatarai kwa usalama wa nchi?
 
Back
Top Bottom