Vyama vya ushirika vinawatia umaskini wakulima, havitakiwi dunia ya leo. Mkulima amka!

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,315
15,062
Wakuu,

Mkulima wa Tanzania anateswa naamini kuliko yeyote duniani.

Unalima kwa gharama zako, unapalia na kuweka mbolea hadi hapo huoni mtu wala serikali kuja.

Mazao yakiiva unapangiwa sehemu ya kuuza tena na bei wapange wao sijui wanawaza nini?

Ifike hatua huu udalali wa stakabadhi ghalani uishe maana umekaa kiujanjaujanja na haumfai mkulima kwa lolote.
 
Kweli mkuu nauchukia ushiriaka umeua soko la kahawa huku mbinga ruvuma wanakijiji wakulima ni masikini sana aiseee ...bora soko huria

Ushirika haufai kabisa kwenye biashara hiyo modal ya ushirika inafaa kwenye uchumi wa kijamaa na sio dunia ya ushindani
 
Ushirika ni kitanzi kwa wakulima maana nao husimama kama madalali tu hakuna lolote
 
Mimi mpaka leo huwa nasikia tu vyama vya ushirika , sijawahi kabisa kukaa na kujua kazi yake nini hasa.
 
We si mkulima wa mazao makubwa ya biashara mfano
Kahawa,ufuta,korosho,pamba nk siku ukijihusisha na shughuli hizo ndo utajua kaz ya vyama vya ushirika
 
Wakuu,

Mkulima wa Tanzania anateswa naamini kuliko yeyote duniani.

Unalima kwa gharama zako, unapalia na kuweka mbolea hadi hapo huoni mtu wala serikali kuja.

Mazao yakiiva unapangiwa sehemu ya kuuza tena na bei wapange wao sijui wanawaza nini?

Ifike hatua huu udalali wa stakabadhi ghalani uishe maana umekaa kiujanjaujanja na haumfai mkulima kwa lolote.
Kwa mfano kwetu Kyela ndio majanga makubwa , tuliuza cocoa kwenye makampuni muda wowote tuliotaka na tulilipwa papo kwa papo , lakini sasa tunaambiwa tuuze Kyecu na malipo ni mpaka mwisho wa mwezi .

Wazee wamekasirika sana , wazee sasa hivi hata tule tupombe twao twa jioni pale Ikato lya Nyerere haiwezekani tena .
 
Hivo vyama vya ushirika ni madalali wa hovyo maana wao hawana hela hadi nao wapeleke kuuza huko ndio mlipwe wala mfumo wa ushirika hauna tija kwa dunia ya leo huo ulifaa kwenye ujamaa na sio leo watu wanapokimbizana na pesa ili kuendelea
 
We si mkulima wa mazao makubwa ya biashara mfano
Kahawa,ufuta,korosho,pamba nk siku ukijihusisha na shughuli hizo ndo utajua kaz ya vyama vya ushirika

Huyo sio mkulima usisumbuke sana kujieleza
 
Hili zoezi kama ni wa kweli kabisa bila unafiki wowote walitazame vizuri. Haupo Ushirika wa kulazimishana na Kuweka mazingira magumu kwa yule asiye tayari.

Ushirika kama ilivyo jina lake huwa ni kujiunga wakulima sio kuunganishwa hata ndoa hawalazimishwa kuaona
 
Wana tuumiza wakulima wana tukata pesa nyingi mara mifuko usafiri sijui utunzaji yaani ni upumbavu mtupu pesa zenyewe zina cheleweshwaaa ,nikiuza mwenyewe sina cha mifuko wala usafiri mnunuzi ana nifuata magetoni tuna malizana maisha yana songa wakulima tunataka pesa kabla jasho letu halija kaukaaa!!!!!
 
Nina Soya zinazofikia Tani 30 ,eti wanadai lazima niziuze kwenye stakabadhi ghalani kwa sababu bei hazinilipi wanataka Kilo 650 ,nimeziweka mpaka nitakapopata mtu binafsi niziuze.
 
Hiyo ni mizimu ya ujamaa ambayo lazima ife ili tuweze kusonga.

Japo vyama hivi vilikua bora sana kabla ya uhuru, thanks to Nyerere alieamua kuviua kwa kuviweka chini ya TANU.
 
Vyema vya ushirika ni madili kama madili mengine haramu yaliyohalalishwa.
Walio na maisha mazuri ni viongo-ziii
 
Wakuu,

Mkulima wa Tanzania anateswa naamini kuliko yeyote duniani.

Unalima kwa gharama zako, unapalia na kuweka mbolea hadi hapo huoni mtu wala serikali kuja.

Mazao yakiiva unapangiwa sehemu ya kuuza tena na bei wapange wao sijui wanawaza nini?

Ifike hatua huu udalali wa stakabadhi ghalani uishe maana umekaa kiujanjaujanja na haumfai mkulima kwa lolote.
Wapuuzi na wajinga kutokea katika ulimwengu baada ya adamu Ni vyama vya ushirika ujinga
 
Back
Top Bottom