Imekuwa kasumba kwa wapinzani kung'ang'ania kugombea nafasi ya urais wakati wa uchaguzi mkuu.Nadiriki kusema ni kung'ang'ania kwa sababu ya msingi kabisa.Iweje mtu kama Prof Shayo au Dr.Mvungi,agombee urais hali akijua kabisa hata akigombea ubunge ni bahati sana kuchaguliwa?Kwa siasa za Tanzania naamini wapinzani kwa ujumla wao wanajua kabisa kuking'oa CCM kwenye nafasi ya kushika dola ni kitu kigumu sana au kisichowezekanika kabisa kwa kipindi hiki.Na sababu yake iko wazi kabisa na wenyewe wanaifahamu.Acha Mapungufu ya katiba,Tume huru ya uchaguzi na vyombo vya dola kama polisi kukipendelea CCM kama wanavyodai,lakini sababu muhimu kabisa ni mizizi ya propaganda ya CCM iliyowaingia watanzania hasa wa vijijini na hata kudhani kuwa CCM ndiyo baba yao na mama yao,hivyo wataambatana nacho hata kiama.
Sasa walau watanzania wameanza kuzinduka.Wito wangu kwa wapinzani wote kuachana na ndoto za kuwa Rais kwa kipindi hiki.Badala yake kwenye uchaguzi ujao waweke nguvu nyingi kwenye majimbo ili wawe na wabunge wengi.Wakishakuwa na nguvu bungeni,chachu ya mabadiliko kwa watanzania itazidi kuongezeka na kuimarika,kwani watakuwa na nafasi nzuri zaidi ya hoja zao kusikika,kuondoa 'ndiyo mzee' ya wabunge wa CCM na kukwamisha miswada yote 'famba'.Naamini hata chances za kuibua ufisadi zitaongezeka.
Hapa siachi hata mmoja,ni wote kina Mbowe,Mtikila,Prof.Baregu,Dr.Mvungi,Mrema,Lipumba,Makaidi,Mbatia nk wakagombee ubunge 2010 na siyo Urais.Muache Mizengwe,kufitiniana nyinyi kwa nyinyi na kutumiwa na CCM.Tunataka upinzani wa kweli tanzania.Tunataka clear majority 2010.Mkishakubalika Tanzania nzima ndipo labda 2015,muweke sasa mgombea urais.Tena awe mmoja,siyo utitiri wa wababaishaji.
Nakaribisha pia wakosoaji!