Vyama vya Upinzani vyataka Spika Ndugai ajishushe kufuatia sakata la Bunge na CAG

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Vyama Vya Siasa nchini vimemtaka Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai kujishusha kufuatia sakata baina ya Bunge na CAG kutokana na kusababisha mgongano baina ya Mamlaka na kukwamisha utendaji Kazi.

Mwenyekiti wa UPDP mhe. Fahmi Dovutwa amesema kwa hali ilivyo sasa ya Spika kumtaka CAG kwenda kwa Rais kujieleza ni kuongeza mkanganyiko zaidi unaowaweka wananchi njiapanda juu ya uangalizi wa hesabu za miradi ya maendeleo.

Wakati huo huo vyama hivyo ambavyo ni CHADEMA, CHAUMA, ACT Wazalendo, Democratic Party, CCK na UPDP vimeungana na kufungua kesi katika mahakama ya Afrika Mashariki kupinga matumizi ya Sheria ya vyama Vya Siasa ambayo vimedai kuwa inakandamiza misingi ya demokrasia.

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema katika kesi yao wameomba mahakama ya Afrika Mashariki kutoa zuio la matumizi ya Sheria hiyo mpaka kesi yao ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi na mahakama hiyo.

Chanzo: Muungwana Blog
 
vijana ni bendera tu!! akili za kushikiwa na wazee!! ngoja wazee watimkie kwenye udongo if you are lucky alive, you will see! we hujawahi kuona mzee mkoloni akifa vijana wake wanavyotumbua, kuhonga na kuuza na kugawana mali zake? akili za wazee na vijana ni maji na mafuta!!! vijana hawakuchapwa fimbo na mkoloni kulima barabara Manyoni Singida!!!sikuzui we endelea kupiga kelele sie tunaenda shimoni kupiga mawe Mererani watoto wapige menu!

Shimo gani utaingia huko mererani ww muuza sura?
 
sarakasi zote tunazoshuhudia za ukiukwaji wa katiba, wizi , kuviziana, ubabe , ufisadi kutekana , kuuana, kutukanana, kutesana and the like zitakufa a natural death in 50 years baada ya genge la wahusika wote kufukiwa na udongo, i wish wabongo wangetulia tu na kutafuta mkate wa familia, this is my theory of generation/ population! yaani huwa nacheka sana wabongo wakilalamikia chochote from the state!!! imani yangu hakuna ambacho kelele na mayowe vitabadilisha sababu we deal with the same manifesto , the same heads/brains/minds in power for almost 58 years now, si wanazeeka na kuchoka hamna macho? wengine hata kuongea kwa kitetemeshi!!wengine kutembea kwa shida! wengine wako kwenye coma! wengine spana mkononi kila siku wako India!!! for me kulalamika is just a waste of energy and time!! wenye akili watanielewa!!!
Wewe mkuu huzeeki?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani,kuliko kukaa kimya,ni afadhali hata kulalamika kidogo.Ukikaa kimya sana,kwanza wanaweza hata kuongeza "dozi" ya hayo yanayolalamikiwa wakidhani mnayapenda,kuyaunga mkono au hata kuyafurahia na kutamani waongeze dozi.Kusema usubiri kwa sababu wanazeeka na kuja kutokomea,tatizo ni kuwa,hawazeeki tu wao,bali na walala hoi pia-Tena mbaya zaidi,walala hoi ndio wanazeeka kwa haraka zaidi,kuchakaa na kutokomea kwa spidi na kwa wingi kuliko "hao".
Na,hata wakitokomea,kuna 'chipukizi' wao kibao si ajabu wanaatamiwa,kulelewa,kukomazwa na kufundwa katika kuilinda,kuikuza na kuja kuilea mifumo,hulka na tabia hizi hizi.Tena si ajabu ikaja kuwa kubwa zaidi.Hawapo wenyewe.Kuna chipukizi wao wapo 'njiani' kuja kushikilia na kuendeleza hilo gurudumugumu na wana uwezo mzuri tu wa kujitetea na kutetea wanayoyaamini.Na hili limo kwenye pande zote;waliopo kwenye usukani kwa sasa na ambao ni wapiga debe kisiasa kwa sasa!
 
Kazi ni sawa na pilipili isiyowasha hata ukiiweka machoni.Ye ataendelea kubwabwaja kulinda mshahara,Lkn kila MTU ashajua nani ni mzalendo halisi wa kodi zetu.
 
"sikuzui we endelea kupiga kelele sie tunaenda shimoni kupiga mawe Mererani watoto wapige menu!"

imetulia sana
vijana ni bendera tu!! akili za kushikiwa na wazee!! ngoja wazee watimkie kwenye udongo if you are lucky alive, you will see! we hujawahi kuona mzee mkoloni akifa vijana wake wanavyotumbua, kuhonga na kuuza na kugawana mali zake? akili za wazee na vijana ni maji na mafuta!!! vijana hawakuchapwa fimbo na mkoloni kulima barabara Manyoni Singida!!!sikuzui we endelea kupiga kelele sie tunaenda shimoni kupiga mawe Mererani watoto wapige menu!
 
Kwa kweli hulka za huyu spika za kuchukulia kuwa,ilimradi anasimamia mhimili,basi huo mhimili ni kama Mungu,haukosei na haupaswi kukosolewa ama kutambulishwwa kwa neno fulani ambalo,CAG anaona lafaa.Hii inashangaza sana,kuudhi na kusikitisha sana.

Sioni mantiki ya kuelekeza CAG aende kwa rais,ilhali rais hajamwita na ajua yanayoendelea (naamini kwa namna fulani) na anao uwezo wa kufanya hilo la kumwita kama akitaka.Ni kuumua bifu iwe nzito kwa kulengesha kwa mkuu nadhani baada ya kuona anakosa huo uzito kuharakisha mchakato.Inasikitisha sana,haipendezi na haimpendezi kamwe!

Haya mamlaka,kwa wengine ni shida sana kwa kweli!
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom