Vyama vya upinzani vimekufa, vimelala au vinasubiri Uchaguzi Mkuu?

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,934
3,805
Vyama vya upinzani vimekufa au vimelala au vinasubiri uchaguzi mkuu utangazwe? Ndio wazuke na kudai tume huru na Katiba mpya, ile kasi imeenda wapi?

Mwisho wa siku mtaambiwa siku hazitoshi kwani uchaguzi unakaribia.

Tunahitaji muamko sio mgawanyiko katika madai husika ya Tume huru ya uchaguzi na Katiba mpya, kama ni wasubiria ruzuku vunjeni vyama.
 
Katiba mpya na tume huru ni mahitaji ya wananchi sio vyama vya upinzani pekee,kitendo Cha kuona kwamba wapinzani ndo wenye wajibu wa kudai katiba mpya na tume huru ni wazi kwamba Kama taifa tuna safari ndefu Sana ya mageuzi ya akili na fikra.

Ndio maana USSR huwa anasema "shule mlikwenda kusomea ujinga"
 
Yule angeweza kutoa laana na ikashika kweli? Nadhani yeye ndiye alikutana na laana za watanzania na zilifanya kazi inavyopaswa.
Zile dua zilizofanyika tarehe 27/10/2020 ndiyo zilimaliza mchezo, huwezi kutumia mabilioni yote Yale ya kodi za Watanzania kufanya uchaguzi halafu ukaagiza mbwa wako wauchafue Kwa kuiba kura na ubaki salama, haiwezekani kabisa.
 
Back
Top Bottom