Vyama vya upinzani vilivyoshiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani wadai haukua huru na haki

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Pamoja na uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Dimani kisiwani Zanzibar kufanyika katika hali ya utulivu na amani , vyama vya upinzani vinavyoshiriki uchaguzi huo vimepinga uchaguzi huo kwa madai hauko huru na haki na una ukiukwaji wa sheria na katiba.

Hali hiyo inatokana na madai ya baadhi wagombea ya vyama hivyo ikiwemo chama kikuu cha upinzani cha CUF ambavyo kwa nyakati tafauti wakiongea na ITV wamedai kutoridhiswa na utaratibu wa uchaguzi huo. Na wapinzani wamekuwa wakinyanyaswa kwa makusudi kwa madai ya kupiga baadhi ya wapiga kura.

Hata hivyo ITV imeshudia katika baadhi ya vituo wananchi wakijitokeza na kutumia haki yao ya kupiga kura bila ya hofu au uonevu ambapo jeshi la polisi likiwa limeweka ulinzi mkali kuhakikisha hakuna vurugu au fujo hali ambayo pia imeshudiwa na mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Ayoub Mohamed Mahmud akiwa na kamati nzima ya ulinzi na usalama na mgombea wa CCM Juma Ali Juma akipiga kura yake Fuoni.

Chanzo: ITV
 
Wala simadai bali ni ukweli ambao hata chembe ya uongo hauna, na pia tunafanya kosa kubwa kuuita UCAHGUZI!!! Haukuwa uchaguzi bali UCHAFUZI wa MARUDIO.

Umeona wapi mwenye haki ya kupiga kura anakataliwa na badala yake anapewa aside na haki ya kupiga kura hawa ni wanausalama wametolewa makambini kwao kumpigia mgombea wa ubunge wa CCM Dimani Zanzibar.
FB_IMG_1485144735699.jpg

Huu no ushahidi mwengine ambao unathibitisha kauli ya wapinzani!! Umeona wapi watu zaidi ya 6000 wapige kura halafu hata moja isiharibike!!?? Wakati mwengine M/Mungu akitaka kukuaibisha basi japo kidogo unaenda mchomo katika uongo wako.
FB_IMG_1485144801415.jpg

Na hii ni kauli nyengine yenye kutoa ushahidi kauli ya wapinzani


Kwa ushahidi wote huu bado unayaita madai upinzani!!!!???? TAFAKARI NA TUMIA AKILI yako kutambua iliyo kweli.
 
Back
Top Bottom