Ushauri: Vyama vya Upinzani vifutwe, kibaki CCM pekee kama chama dola

Wengi huamini chama tawala ndo dola yenyewe na kwa hili; wote walioko madarakani na wapinzani huona hivyo. Ndo maana unaona kuwa mara nyingi vyama vya upinzani vimekuwa vikijiweka katika nafasi ambapo vinaonesha kuwa dola ni sehemu ya Chama tawala.

Hapo si kweli Mkuu. Kama kuna mtu anayefanya kosa kuchanganya madaraka ya chama na serikali basi n CCM, ambao wanatumia kisingizio kwamba serikali lazima itekeleza sera zao kwa kuwa wao ndio walioko madarakani. Wapinzani wamekuwa wakililalamikia sana hili. Haiwezi kawa wapinzan ndio wanaokosea juu ya hili kwa sababu hawajawahi kuendesha serikali.

Kushindwa kwa upinzani kusimamisha Chama imara chenye mifumo imara ambayo inaheshimika na kuonekana kama mbadala wa CCM ni mojawapo ya sababu kubwa inayowafanya wananchi kuendelea kuiona na kuamini kuwa serikali ndo CCM na CCM ndo serikali.

Wapinzani watawezaje kusimamisha chama chenye nguvu wakati kila siku wako kwenye mpambano dhidi ya kila aina ya mbinu inayofanywa na CCM kuwadhoofisha kwa kutumia vyombo vya dola? Ni kama CCM ina sera rasmi ya kudhoofisha upinzani, kutowapa nafasi hata ya kupumua ili wapoteze muda mwingi kushughulika na mambo mengine badala ya kuimarisha vyama vyao. Kipofu yeyote anaweza kuuona huu mkakati wa CCM, ndani na nje ya Bunge.
 
Tatizo vyama vingine vilikuwa vinaendeshwa Kama vyama vya harakati badala ya kuwa vyama vya siasa , hivyo kukosa mvuto kwa wapiga kura wengi!!!

Mkuu, Hebu tupe chama kimoja ambacho hata sasa hivi kinaendeshwa kisiasa kinyume na harakati. Mbona kama tunatumia haya maneno bila mpango??
Kuna vyama vina harakati ya kuwafungua watu macho ili waone wang'amue. Muda wa kulala umekwisha. Kuna vyama vina harakati ya kuwafumba watawaliwa macho wasiuone mwanga wakajijua.
Nasema, kila chama kipo kwenye harakati.
 
Acha ushabiki. Ongea vitu vinavyojenga nchi; Tanzania kwanza. Kwani huko CCM hakuna mambo mliyofanya ambayo yameharibu badala ya kuchochea maendeleo? Vipi sera yenu ya kubinafsisha mashirika ya umma ambayo mliitekeleza kama mmevuta majani ya Njombe? Na mikataba ya ajabu mliyosimamia kwa siri ilikuwa ni watu wa vyama vya upinzani? Sera dhaifu ya elimu? Usimamizi mbovu wa upatikanaji wa nishati ya umeme, umeleta maendeleo ya nchi?

Nani waliowalea na kuwakumbatia mafisadi nchini kwa miaka thelathini iliyopita, vyama vya upinzani? Kwani sasa hivi Raisi Magufuli anasafisha uozo na uchafu nchini ulioletwa na vyama vya upinzani, au CCM wenyewe?

Ni kama Nyerere alivyosema; mnakuwa kama mtoto mchanga anayekunyea halafu analia yeye. Kama Tanzania ya leo haijaendelea kama ilivyostahili, kosa sio la vyama vya upinzani, ni la CCM.

Hivi kitu gani hasa kinachowafanya CCM muamini mmekuwa bora sana kuliletea taifa hili maendeleo kuliko kile watu wa upinzani wangefanya wangekuwa madarakani? Mnajiangalia kwenye kioo na kujisifia uzuri?
UCHAFU AMBAO UPINZANI UNADAI UNAPAMBANA NAO INAONEKANA WAZI KWAMBA WAO WANAO KWA KIASI KIKUBWA.KM SWALA LA UFISADI HATA WANAONA AIBU KULITAJA.NI HERI CCM AMBAYO INAONEKANA WAZI INA JISAFISHA KULIKO MAFISADI WENYE NJAA WANAOTAFUTA NAFASI YA KUPORA MALI ZA WATZ.
 
Hebu taja mafisadi walioko upinzani na walianza lini.
 
UCHAFU AMBAO UPINZANI UNADAI UNAPAMBANA NAO INAONEKANA WAZI KWAMBA WAO WANAO KWA KIASI KIKUBWA.KM SWALA LA UFISADI HATA WANAONA AIBU KULITAJA.NI HERI CCM AMBAYO INAONEKANA WAZI INA JISAFISHA KULIKO MAFISADI WENYE NJAA WANAOTAFUTA NAFASI YA KUPORA MALI ZA WATZ.

Mkuu, mie naona wewe ni kati ya wale mashabiki wa CCM ambao mpo CCM lakini hamjui kwa nini mpo CCM, na bado mpo tayari kufanya lolote kwa ajili ya CCM lakini sio Tanzania, na as long as mnakula na kulala CCM oyee upinzani zii! Kuna wengine tunaenda mbali zaidi ya hapo ndio maana tunataka CCM na upinzani wote wawe na misuli. Hata hivyo ninakuelewa, asante kwa kuchangia thread.
 
Kuna Msemo wa 'Toa boriti kwenye jicho lako kabla ya kuzungumzia kibanzi kilicho kwenye jicho la mwenzio'

Uko sahihi katika hilo.

Yaelekea wote wanaboriti machoni mwao. Sasa basi, ilikufanikisha zoezi la kutoana maboriti

hayo inabidi mwenye boriti kubwa kwenye jicho ndo aanze kutolewa (kwa muktadha huu:boriti la mwenye mamlaka...).
 
Hewaaaa! Ndio maana nikasema, tufike mahali tuache kudanganyana au kuwadanganya hao tuliotaka kuwafurahisha. Tuwe wazi tu na kuwaambia bwana hili suala la vyama vingi vya siasa hapa kwetu haliwezekani. Tuunganishe vyama vyote, kuunda serikali ya ushirikisho wa vyama vyote na kujipanga upya. Tunaona wazi mfumo wa vyama vingi unahatarisha amani na umoja wetu na bado tunajfanya kuukubali, kwa kumfurahisha nani? Tuukemee mfumo wa vyama vingi kama tunavyoukemea udini, kwa kuwa unahatarisha amani na umoja wetu kama Watanzania.
Sasa tukirudi kwenye chama kimoja huoni kwamba tutakosa misaada ambalo ndiyo lengo letu kuukubali mfumo wa vyama vingi?
 
Nahisi sisi wenyewe bado hatujui kuitumia Demokrasia.Hili linatokana na elimu duni.Michakato yote ya chaguzi zetu ina uongo mwingi.Ujanja ujanja wetu unatugharimu sana.
 
Mkuu, Hebu tupe chama kimoja ambacho hata sasa hivi kinaendeshwa kisiasa kinyume na harakati. Mbona kama tunatumia haya maneno bila mpango??
Kuna vyama vina harakati ya kuwafungua watu macho ili waone wang'amue. Muda wa kulala umekwisha. Kuna vyama vina harakati ya kuwafumba watawaliwa macho wasiuone mwanga wakajijua.
Nasema, kila chama kipo kwenye harakati.
Chama cha kisiasa kina fanya shughuli zake kwa kufuata taratibu na kanuni, Chama cha kiharakati
Kina Tumia njia za kusababisha civil dis obedience , mfano kutoka Bungeni badala ya kutumia kanuni ku challenge maamuZi ya spika au naibu wa spika
 
Uko vizur kwenye Uzi wako!Afrika ni nchi chache sana zilizo na utayar na vyama vingi,vyombo vya usalama ni adui mkubwa wa vyama vya siasa.Kwa Tanzania nionavyo tunaelekea kubaya,chuki zinazid kuongezeka kati ya mtu na mtu,kati ya jamii na jamii.Ni bora kama watawala hawataki vyama vingi vifutwe kabisa.Haiwezekani Mkuu wa nchi aviite vyama vya upinzan ni maadui.
 
Chama cha kisiasa kina fanya shughuli zake kwa kufuata taratibu na kanuni, Chama cha kiharakati
Kina Tumia njia za kusababisha civil dis obedience , mfano kutoka Bungeni badala ya kutumia kanuni ku challenge maamuZi ya spika au naibu wa spika

Mkuu nisamehe tu. Hayo ni kwenye jamii inayoelewa vitu wanavyo fanya. Kwe hilo bunge letu, sidhani ka hayo yapo. Kila kitu kwao ni double standards. Kumbuka mh. mmoja wa chama tawala, alipokuwa anachangia hoja. Unakumbuka tusi alilotoa mdomoni; "Fwaki yuu." alitamka kwa kinywa, na mic ikiwa on, huku amesimama. Mambo si yaliendelea kama kawa. Mh mwingine lakini this tyme kutoka upinzani. Akainua mkono na kuwapungia wenzake wa upande wa tawala. Kumbe wao wanachunguza hata vidole vilivyokaa. Tiyari wakaona kidole kimekaa vibaya. Ikawa tusi kuubwa. Yu know what; Kasimamishwa mikutano kibao. Kwa nini double standards?? Umwambie nani wakati wakiomba Taarifa hawapewi nafasi?? Angalia uyasemayo. Nchi hii imekuwa ni nchi ya "Ma double standards tuu". Hata wewe umesimamia kwenye double standard katika hili. Huyaoni yanayotendwa na chama chako???
 
hata wewe unawajua tatizo letu watz mtu akiwa ccm ni fisadi akienda upinzani msafi athari za fisadi ziko pale pale haijalishi yuko chama gani

Ni hivi hebu taja fisadi aliyeko cdm ili nikusaidie kwenye hilo ili usiendelee kupotosha ama kumezeshwa maneno.
 
Mkuu nisamehe tu. Hayo ni kwenye jamii inayoelewa vitu wanavyo fanya. Kwe hilo bunge letu, sidhani ka hayo yapo. Kila kitu kwao ni double standards. Kumbuka mh. mmoja wa chama tawala, alipokuwa anachangia hoja. Unakumbuka tusi alilotoa mdomoni; "Fwaki yuu." alitamka kwa kinywa, na mic ikiwa on, huku amesimama. Mambo si yaliendelea kama kawa. Mh mwingine lakini this tyme kutoka upinzani. Akainua mkono na kuwapungia wenzake wa upande wa tawala. Kumbe wao wanachunguza hata vidole vilivyokaa. Tiyari wakaona kidole kimekaa vibaya. Ikawa tusi kuubwa. Yu know what; Kasimamishwa mikutano kibao. Kwa nini double standards?? Umwambie nani wakati wakiomba Taarifa hawapewi nafasi?? Angalia uyasemayo. Nchi hii imekuwa ni nchi ya "Ma double standards tuu". Hata wewe umesimamia kwenye double standard katika hili. Huyaoni yanayotendwa na chama chako???
First of all sina card ya Chama cho chote , kwa hiyo siwezi kutetea iwe ccm au cuf au cdm .
Kuhusu hizo tuhuma za matusi ya ccm au mbunge wa ccm bahati mbaya siku sikia Maana bunge live hakuna , sasa yakiandikwa inawezekana ya kawa yame chujwa.
Tukirudi kwenye mada ni kwamba ni nacho kiona Bungeni Ukikosea unatakiwa kufuta usemi sasa wakati mwingine mbunge hu goma
Kufuta usemi au maneno ya sio faa , ukikata na Mtu aki lalamika ndipo adhabu hutolewa.
Na sehemu nyingine ambayo nitatofautiana iwe na ccm, cuf au cdm ni hizi machaga ki za graduates wa ccm/cdm/cuf ni ujinga , kwani kwa hali ya bongo Leo unaweza kuwa cdm, kesho Kutwa ccm , pili utawala unaweza kuwa wa ccm Kama ilivyo sasa , sasa Hiyo degree yangu Nilio itanabaisha na siasa za Chama fulani nita itumiaje. Unaposoma jukumu lako ni kutimikia system iliyopo.
 
Hapo si kweli Mkuu. Kama kuna mtu anayefanya kosa kuchanganya madaraka ya chama na serikali basi n CCM, ambao wanatumia kisingizio kwamba serikali lazima itekeleza sera zao kwa kuwa wao ndio walioko madarakani. Wapinzani wamekuwa wakililalamikia sana hili. Haiwezi kawa wapinzan ndio wanaokosea juu ya hili kwa sababu hawajawahi kuendesha serikali.

Wapinzani watawezaje kusimamisha chama chenye nguvu wakati kila siku wako kwenye mpambano dhidi ya kila aina ya mbinu inayofanywa na CCM kuwadhoofisha kwa kutumia vyombo vya dola? Ni kama CCM ina sera rasmi ya kudhoofisha upinzani, kutowapa nafasi hata ya kupumua ili wapoteze muda mwingi kushughulika na mambo mengine badala ya kuimarisha vyama vyao. Kipofu yeyote anaweza kuuona huu mkakati wa CCM, ndani na nje ya Bunge.

Wapinzani lazima wainuke juu dhidi ya yote hayo! Madhaifu ya ndani ni makubwa kuliko hayo yanayotoka nje. Kama madhaifu yao ya ndani yangekuwa Kidogo, uwezekano wa wapinzani kusimama dhidi ya hila za walioko madarakani ni dhahiri. Na ikiwa wapinzani hawawezi kuzishinda hila za walioko madarakani, ni sawa na kusema hatuko tayari kwa upinzani. They should rise above all that! Kuwashinda wale walioko madarakani, kimsingi ni lazima uwe bora, bora zaidi kuliko wao, na ionekane hivyo!
 
Back
Top Bottom