Vyama vya upinzani vifutwe, kibaki CCM pekee kama chama dola

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Messages
4,973
Points
2,000

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2012
4,973 2,000
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu siasa za Tanzania tangu miaka ya tisini. Baada ya uchaguzi wa mwaka huu,nimeamua kukubali kuwa CCM hakitakaa kiondoke madarakani kwa njia yoyote ile unayoijua wewe duniani kwa sasa, hata kama itafanya vibaya namna gani!

Mipango yote,mikakati yote ya kukiondoa chama hiki haiwezi kufanikiwa kwa kuwa ukweli unaonekana dhahiri kuwa kimewekeza sana katika kuhakikisha kinakuwa salama baada ya uchaguzi hata kama ni kwa gharama ya maisha ya watu wake.

Mikakati wanayoifanya CCM ni pamoja na kuhakikisha wanatumia inteligensia ya taifa,kuhakikisha kuwa hakuna chama kinachoweza kukua na kuwa tishio kwa ccm halafu kikabaki salama. Kwa watu wengine tulijua mapema jinsi cdm ilivyouwawa hata kabla ya kuingia katika uchaguzi huu. Naweza kusema hivi chadema ilivyo ni kwa sababu ya ubishi na uhodari wa Mbowe. Naamini wasingefika hata hapo walipo bila uthabiti wa viongozi wa juu akiwemo pia dr Slaa.

Kwa hali ilivyo, ninajaribu kuviona vyama vya upinzani kama vile vinatumika kuweka uhalali wa kuendelea kutawala kwa ccm mbele ya jamii ya kimataifa. Baadhi ya vyama vinavyoonekana kuanza kuwa tishio hukabiliana na misuko suko mikubwa na hata kwa baadhi ya wanachama wake kupoteza maisha kwa vile tu wao ni wapinzani. Sasa nadhani umefika wakati ili kuepusha watu wasio na hatia kuumia kwa vile tu ni wapinzani,vyama hivi vifutwe na kibaki chama kimoja kama zamani. Hakuna sababu ya ccm kutumia nguvu kubwa na rasilimali za taifa kwa kuandaa uchaguzi ambao wao wanajua wanataka kushinda kwa namna yoyote ile.

Nawaomba watanzania waniunge mkono katika hili, wale wabunge waliochaguliwa kupitia upinzani, mniunge mkono kwani mnaweza kugombea tena kupitia CCM pia. Sioni tumaini tena katika mfumo huu wa vyama vingi. Ni bora kuwe na mfumo wa mgombea binafsi au hata CCM wachaguane wenyewe kama wanavyopenda ili mradi watu wasiumie kwa sababu ya uadui wa kisiasa.
 

PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Messages
4,874
Points
2,000

PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2013
4,874 2,000
Kaka msingi wa CCM ulisimikwa na mfumo wa katiba iliyopo. ni ngumu sana kuitoa CCM madarakani kwa mfumo wa katiba iliyopo. Ndiyo maana mfumo wa rasimu ya pili ya Warioba ulikuwa ni hatari sana kwa CCM kuendelea kubaki madarakani, ndiyo maana waliikataa.

Mimi nakuunga mkono kabisa, haina maana vyama vya upinzani kupoteza rasilimali zao wakati Rais ameshawekwa kabla hata ya uchaguzi.
 

Radhia Sweety

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2011
Messages
4,440
Points
1,500

Radhia Sweety

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2011
4,440 1,500
Kaka msingi wa CCM ulisimikwa na mfumo wa katiba iliyopo. ni ngumu sana kuitoa CCM madarakani kwa mfumo wa katiba iliyopo. Ndiyo maana mfumo wa rasimu ya pili ya Warioba ulikuwa ni hatari sana kwa CCM kuendelea kubaki madarakani, ndiyo maana waliikataa.

Mimi nakuunga mkono kabisa, haina maana vyama vya upinzani kupoteza rasilimali zao wakati Rais ameshawekwa kabla hata ya uchaguzi.
Katiba inahusiana nini na watu kujitokeza kwa wingi kuipigia kura CCM katika jimbo la Namtumbo kwa mfano?
 

sawabho

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Messages
5,290
Points
2,000

sawabho

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2011
5,290 2,000
Uloi nga mâché68;14475138 said:
Vyama vya upinzani vinajiandalia vyenyewe mazingira ya kushindwa kwa kukosa mikakati thabiti ya ushindi na usaliti wao! Mfumo ungekuwa mbaya wasingeshinda majimbo mengi ya UBUNGE na UDIWANI!
Wanaosaliti huwa wanapata support kutoka sehemu fulani.
 

RockSpider

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2014
Messages
6,869
Points
1,500

RockSpider

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2014
6,869 1,500
Binafsi nilishangaa sana kwanini UKAWA walikubali kuingia kwenye uchaguzi kwa katiba hii ya CCM .... Hakuna maana ya kupiga kura kama vyombo vya dolla viko upande wa CCM ...
 

james chapacha

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
941
Points
195

james chapacha

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
941 195
Nyie kateni tamaa lkn mimi siwezi kurudi Misri nitapambana mpaka nifike nchi ya ahadi,siwezi kuwaacha wanangu jangwani ki-raisi namna hii. Na hata nisipofika sina shaka nitakapoishia hapatakuwa mbali na nchi ya ahadi, jambo ambalo litawafanya wasitembee mwendo mrefu. Mungu nisaidie
 

Forum statistics

Threads 1,392,344
Members 528,599
Posts 34,105,857
Top