Vyama vya upinzani: Unganeni kama mnataka kuing'oa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyama vya upinzani: Unganeni kama mnataka kuing'oa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by m_kishuri, Aug 7, 2010.

 1. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145  Kwa mujibu wa the Wikipedia:
  A political party is a political organization that typically seeks to attain and maintain political power within government, usually by participating in electoral campaigns, educational outreach or protest actions.

  Kama vyama vya kisiasa vya Tanzania vinataka kushinda au kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni, basi inawabidi waungane. La sivyo uwezekano wa kuing'oa CCM madarakani ni mdogo. Mifano ipo mingi sana katika bara la Afrika na kwingineko, ambako vyama vikongwe vimeweza kuangushwa tu baada ya upinzani kuungana.

  Wondwosen Teshome (2009) anaandika,
  "So far in Africa, opposition parties are rarely successful in
  ousting the incumbents in elections largely due to their
  fragmentation and their failure to form opposition coalitions."

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  CHADEMA & CUF........That will never happen in our planet TANZANIA!
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kwa vyama kama tlp, udp, upnp kusimaisha mrais si uzandiki? Bado cuf na chadema inaweza kuwezekana
   
 4. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ubinafsi umetawala kwenye vyama vya upinzani, tusitegemee kuona muungano wowote
  kutoka kwao kwa miaka hii ya karibuni. Labda kwa kizazi kijacho.
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Aug 7, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  viungane kwa kutumia sheria ipi, mimi nafikiri ungesema vishirikiane, kuunganisha vyama haiwezekani hapa TZ, haiwezekani hasilani.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ooohh, inaonekana hujui kwamba siasa = ulaji + ubinafsi, kama kungekuwa na nia ya dhati ya kulitumikia taifa kusingekuwa na kuzibiana, na hata vyama vya siasa visingekuwa na sababu ya kuwepo. CCM na watoto wake, wote wasingakuwepo.
   
 7. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa misingi hiyo wataendelea kuwa vyama vya upinzani daima bila kuleta mafanyikio yoyote kwa wananchi.
   
 8. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hii ni hasara kwa walala hoi endapo kila the so called (WANASIASA) wanafikia matumbo yao tu. :hungry:
   
 9. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana ccm nao kwa unafiki,

  Umetoa ushauri na kisha unatoa hitimisho

  Peleka unafiki wako huko Lumumba.... mafisadi bana hamjambo
   
 10. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama vile wewe unavyotumikia matumbo yako hapa kwenye forum kwa kutetea ufisadi wa chama cha mafisadi ccm
   
 11. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Kuna vyama vimeundwa kwa njaa za watu binafsi na sio kuikomboa nchi.
   
 12. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndio maana muungano wa vyama hautakaa uwepo. Maana kuna vingine ni vya matumbo (tlp na wenzake) wakati vingine ni kazi ya kukomboa wananchi - chadema na cuf
   
 13. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 3,999
  Trophy Points: 280
  never say never inawezekana mkuu
   
 14. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Editha Majura

  WAZIRI Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba, ameshauri vyama vya siasa nchini viungane ili viwe na nguvu itakayoleta ushindani wa kisiasa wa kutosha kufikia wananchi wa kada zote. Warioba aliyazungumza hayo jana wakati akizungumzia uchaguzi uliomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita nchini.

  Alisema uamuzi wa kuwa na mfumo wa vyama vingi haukulenga kuweka utitiri wa vyama bali vyama zaidi ya kimoja vyenye uwezo wa kuwafikia wananchi wengi zaidi.

  "Viongozi wa vyama vya siasa waangalie uwezekano wa kuungana bila kujali ni chama tawala au pinzani cha msingi ni kupitia sera zao na kujadili namna wanavyoweza kuungana na kujenga vyama vichache lakini vyenye nguvu kisiasa na uwezo wa kuwafikia wananchi wengi," Warioba alieleza.

  Hata hivyo, alisema hatua iliyofikiwa na vyama vya upinzani ya kupata viti vya ubunge kwenye majimbo mengi zaidi kwenye mikoa tofauti, ni ishara kwamba taifa linaelekea kwenye siasa ya kidemokrasia kwa sababu vitajiongezea uwezo kisiasa na kiuchumi.

  "CCM ilijengwa katika misingi ya jamii kuanzia nyumba kumi kumi ,hilo limeanza kutekelezwa na vyama vya upinzani ambavyo mwaka huu vimepata wabunge mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Kagera, Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Iringa, Mbeya.., inamaanisha vitajiongezea uwezo wa kifedha hali itakayoongeza ushindani wa kidemokrasia," alisema.

  Madai kwamba wazee CCM walimtelekeza mgombea wao wa urais, Jakaya Kikwete, wakati wa kampeni Warioba aliyaelezea kuwa ni ya kisiasa kwa sababu wasingeweza kuongozana naye kila mahala bali walitekeleza majukumu yao kwa namna na nyakati sitahili huku vijana wakienda sambamba na mgombea huyo. Aliwaasa wanaopata uongozi kutambua kuwa ni dhamana ambayo kila mwenye sifa anastahili.

  Alikemea tabia ya baadhi ya viongozi ambao wakipata madarakani wanadhani hakuna anayestahili zaidi yao na ikitokea mwingine kugombea wadhifa huo wanamuona kuwa amewaingilia. Waziri huyo mstaafu alipongeza hatua ya utulivu na amani iliyozingatiwa visiwani Zanzibar kipindi chote cha uchaguzi kwamba ni tukio la kihistoria kwa visiwa hivyo kuwa na uchaguzi wa aina hiyo huku matokeo yakitangazwa mbele ya vyama vyote vya kisiasa na kufuatiwa na hotuba zenye kuashiria umoja wa kitaifa.

  Ingawa uongozi wa umoja wa kitaifa visiwani humo unatarajiwa kukabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ya tofauti za sera za vyama husika na matatizo ya muungano, Warioba alisema kwa mshikamano uliyoonekana wakati wa uchaguzi ni dhahiri kwamba changamoto hizo zitadhibitiwa.

  "Tofauti ya sera za vyama hivyo, siyo kubwa sana naamini zitawekwa sawa. Matatizo ya muungano awali yalikuwa kati ya Bara na Visiwani lakini baadaye yakachukua sura ya kisiasa na kuwa ya CCM na CUF jambo ambalo baada ya vyama hivyo kuonyesha mshikamano, matatizo hayo yatakwisha kwa sababu kiini cha muungano ni kikubwa kuliko cha matatizo hayo," alisema Warioba.  SOURCE: Warioba ashauri vyama vya upinzani viungane
   
 15. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Wananchi wengi wanapenda mageuzi¬Ö!!, wananchi wengi wameshachoka¬Ö!! Kinachozuia Mageuzi ni mbinu chache tu.

  Baadhi ya mbinu zinazotumiwa sasa tumezisikia:-

  • Kununua shahada (lakini hili kama kuna fomu za kujaza kama umepoteza shahada) basi mtu anaweza kuuza shahada yake na bado siku ya siku akapiga kura, kwa kusema kwamba shahada yangu imepotea.
  • Mbinu nyingine ni propaganda ambazo wamebatiza kila Chama kuanzia Dini, fujo mpaka Ukabila. Utaona dawa ya hii propaganda ni kwamba wapinzani wote wakiungana hii itakuwa diluted. Na wakiungana na kusimama kama Chama kimoja kwenye Uchaguzi 2015, CCM watakuwa hawana pa kukimbilia na propaganda za sasa hazitafanya kazi.
  Kila Chama kina vichwa na wanamageuzi wa kutosha ifike wakati wote waone kwamba kutengana na kuendelea kugawana kura na kupata ruzuku za hapa na pale haitoshi, inabidi kuweka nchi mbele na kuiangusha CCM na kutaifisha mali zetu, (viwanja vya mipira majengo n.k., na kufuta makada wao wanaofuja pesa zetu ambao ni wakuu wa wilaya n.k.); Just imagine wote wasimamishe mgombe Urais mmoja na wengine kina Lipumba Mtikila et al wote wakasimama kwa kugombea Ubunge...

  Kama bado wapinzani watataka kutengana basi watatengana baadae baada ya kumuondoa CCM yaani uchaguzi wa 2025 (baada ya kufanya shughuli pevu ya miaka 10)
   
 16. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,081
  Likes Received: 6,544
  Trophy Points: 280
  hakuna hata haja ya kuungana, chadema inakubalika, wengine ni wanafiki wakubwa watatutia aibu tu huko mbele.
   
 17. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #17
  Oct 5, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vyama vya upinzani vikitaka kuungana viungane lakini chama makini kama CDM wasishiriki kwani karibu vyama vyote vya upinzani ni wanafiki. Hawapo kwa maslahi ya nchi na kuna mifano mingi. CUF tayari wana ndoa na CCM ni sehemu ya serikali Z'bar; sijui kama inawezekana mwanamke mmoja kufunga ndoa na waume wawili. Vyama cha NCCR na vingine vyenye wabunge wana kambi yao ndogo ya upinzani na walikataa kuunga mkono CDM bungeni hata kwa masuala ya msingi yenye maslahi kwa wananchi kama vile kufuta 'sitting allowance'. Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, CCM imekuwa na vyama pandikizi na pia kutumia mamluki ndani ya vyama pinzani vyenye nguvu. Vyama vya upinzani vinaweza vikaungana vyote kwa nia nzuri tu, lakini ikitokea KWA MFANO uchaguzi mkuu wa 2015 vikaamua kususia uchaguzi mpaka katiba mpya ipatikane, CCM inaweza ikatumia mbinu kikasajiliwa chama kipya kwa haraka haraka ali mradi kikubali kuingia kwenye uchaguzi. Uchaguzi unaweza kufanyika kwa sababu masharti ya kufanyika uchaguzi katika mfumo wa vyama vingi yamekidhi haja. Hii iliwahi kutokea Zanzibar ambapo chama cha PPT cha Dr. Che-Mponda kilianzishwa na kusajiliwa kwa muda mfupi, CUF kilipotishia kususia uchaguzi kutokana na rafu za CCM. Chama hicho kwa sasa kipo kwenye usingizi wa milele kwa sababu malengo ya kusajiliwa kwake yalitimia. CDM ni chama makini wanayafahamu hayo, janja nyani kula mahindi bichi.
   
 18. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Mkuu mbona uchaguzi wa 2000 iliwezekana?
   
Loading...