Vyama vya upinzani, tumieni fursa hii kudai tume huru ya uchaguzi maana ndio penalt yenu ya mwisho kwa awamu hii

na wewe

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
231
397
Za muda huu wadau.
Niende kwenye mada moja Kwa moja.

Kwa mda mrefu sasa vyama vya upinzani vimetupa sintofahamu ya Kwa nini awamu hii pamoja na kuonekana kuonewa sana ila haijawekeza nguvu kubwa kudai tume huru ya uchanguzi hali wafuasi na wanachana wao mtaani wamejitahidi kusisitiza na kushinikiza hasa kupitia mitandao ya kijamii.

Ni kweli yawezekana mazingira yalikuwa sio rafiki sana kwa kufanya hivyo.ingawa Mtoto Wa CHACHA WANGWE amejitahidi Kwa sehemu yake na ilionekana ameshinda lakini Kwa sababu ya mazingira ya baadhi ya udahifu wa vifungu vya kuteuwa wasimamizi Wa uchanguzi mwisho ilipelekea kushidwa tena

Lakini pamoja na mazingira kuwa sio rafiki Kwa wapinzani kudai haki zao Kwa uhuru, lakini pale inapotekea nafasi ya penalt kama hii inayoendelea sasa,ni vizuri kuitumia vizuri na yamkini inaweza leta goli linaloitwa "goli LA mkono Wa mungu" Kwa sababu naamini hakuna kukata tamaa.

Kwa sehemu Yangu Mimi niwapongeze kwa vyama vingi vile ambavyo ndio tano bora ya wapinzani kuwa na msimamo mmoja Wa kujitoa ingawa Nina wasiwasi Wa C.U.F anaweza kuwa spy au chambo ili mumsogeze karibu kudini.
Kwa umoja Huu na taharuki iliyopo mda huu, mnaweza tumia udhoefu wenu mlionao kushinikiza mabadiliko hata kama ni machache ambayo yataleta tija kwenye tume ya uchaguzi.

Najua mda sio mrefu jukwaa cha kampeni litakuwa wazi lakini kumbuka litakuwa wazi Kwa wiki moja tu hivyo sio rahisi kueleweka sana majukwaani.lakini mkitumia umoja huu uliopo sasa ambayo kama hamtachoka ndani ya mwaka mmoja uliobaki naamini mnaweza sababisha jambo zuri kutokea katika kuelekea uchaguzi mkuu..maana sasa mmepata sababu ya kusimamia Kwa hoja na ushaidi

Asante
 
Back
Top Bottom