Vyama vya upinzani Tanzania vinaongozwa na madikteta

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,205
12,702
Hawa watu ukiwaangalia bila bias utaona ni madikteta wakubwa sana. Cha kushangaza wafuasi wao hawaoni hilo kuwa ni tatizo.

Moja ya sifa kuu ya udikteta ni kung'ang'ania madaraka. Cheki wanavyofanya.

1. Mrema ni mwenyekiti wa TLP toka 1999-leo. Miaka 23

2. Zitto amakuwa kiongozi wa ACT toka 2015. Miaka 7. Ukomo wake haujulikani.

3. Mbowe kawa mwenyekiti wa CHADEMA toka 2004. Miaka 18.

4. Mbatia huko NCCR hana chini ya 10yrs.

5.Lipumba. mwenyekiti wa CUF toka 1995 hadi leo. Miaka 27!!! Acha ile likizo yake.

Inaonekana CCM kina demokrasia sana. Wamekuwa wakibadili kiongozi wao kidemokrasia sana.

Ni wakati vyama hivi vikaweka ukomo wa kuwa mwenyekiti, vinginevyo vitakuwa mazalia ya madikteta.
 
Mzee wa ubwabwa umemsahau naye amekaa na hana mawazo ya kuachia ngazi.
 
Back
Top Bottom