Vyama vya Upinzani na Wanaharakati Wote Andaeni Maandamano ya Amani Kudai Katiba


Gosbertgoodluck

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Messages
2,865
Likes
32
Points
0
Gosbertgoodluck

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2008
2,865 32 0
Ndugu zangu wana JF,
Kasi ya kudai katiba mpya naona kama imepoa. Wananchi wengi mitaani wanaongelea habari ya katiba mpya lakini wanakosa uongozi wa kuwakusanya ili kuonyesha hisia zao. Jaji Mkuu Mhe. Augustino Ramadhani na viongozi wengi waandamizi ikiwa ni pamoja na Mhe. Jaji Sinde Warioba wameeleza bayana kuhusu umuhimu wa kuwa na katiba mpya inayokidhi matakwa na matarajio ya watanzania kwa ujumla.

Naomba mnifahamishe wana JF, hivi hakuna uwezekano wa chadema na vyama vingine vya upinzani pamoja wanaharakati nchini kuandaa maandamano makubwa ya amani katika mikoa yote ili kutoa fursa ya wananchi kueleza dukuduku lao na kuishinikiza serikali ianze mara moja mchakato wa kuunda katiba mpya? Mimi nina hakika hilo likifanyika litaitikisa serikali na kuiamsha kutoka kwenye usingizi mzito. Mnasemaje wazee?
 
Mungi

Mungi

JF Gold Member
Joined
Sep 23, 2010
Messages
16,994
Likes
482
Points
180
Mungi

Mungi

JF Gold Member
Joined Sep 23, 2010
16,994 482 180
Vyama vya upinzani Tanzania ni CHADEMA peke yake, mengine ni matawi ya CCM.

Sema CHADEMA na wanaharakati wote waandae maandamano hapo utaeleweka broda!
 

Forum statistics

Threads 1,237,815
Members 475,675
Posts 29,301,990