Vyama vya upinzani msipoungana na mkawa na UMOJA imara wenye hoja bora CCM itashinda kila uchaguzi

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,318
Vyama vya upinzani visipotafuta mbinu mbadala wa kujenga umoja imara na kuwa na hoja bora na zenye mashiko basi CCM itaendelea kushinda ktk uchaguzi kila uchaguzi mkuu unapofika.

Watanzania wana shida nyingi sana ambazo zinahitaji kutatuliwa ni wakati muafaka wa viongozi wa siasa kuja na mbinu tofauti na zilizo zoeleka na wengi toka siku nyingi.

Watanzania wanahitaji mabadiliko ya kweli kabisa toka kwa viongozi wazalendo wa siasa.

Wapinzani wasipokuwa wamoja kuelekea 2020 basi CCM itawasambaratisha
 
Sasa kama Ben Saanane tu kawatoa jasho ndio watawaweza ukawa, endeleeni na maandalizi ya kuiba kura ndio mnachoweza.
 
kwa sheria za uchaguzi zilizopo saivi na tume ya uchaguzi hii hata wakaungana upinzani wote wa tz, kenya na uganda ccm itashinda milele hata wasiibe kura hata moja watashinda tu

-kwa ufupi mfumo wetu wa vyama vingi ni kiini macho tu, mamlaka yote ya tume ya uchaguzi inatokana na kuteuliwa na mwenyekini wa chama kilichopo madarakani hiki ni kichekesho
-chama kilicho madarakani kinaweza kubadili sheria yeyote kuhusiana na jambo lolote wakati wowote au kutoa tafsiri za sheria zilizopo kama unavyopenda wao

mfumo wa upinzani wa aina yeyote unakuwa na timu mbili au zaidi zinazoshindana na kunakuwa na referee na linesman ambao hawahusiani na upande wowote wa timu hizi ,wala hakuna timu ambayo inapewa mamlaka ya kuchagua referee au linesmen hata kama timu inaumili uwanja basi haiwezi kuchagua referee wa kuendesha mechi.

na ikibidi kama timu inakuja na referee wake basi inajulikana mwanzo kuwa hapo hakuna mechi na mshindi keshajulikana kabla ya pambano kuanza

na katika jambo hili, hapa ndio tunapotilia shaka upinzani kuwa nao pia wamo katika kiini macho cha kuzingua watu,kwa sababu unakubalije kucheza mechi wakati mpinzani wako anakuja na referee wake,haya si mambo ya kitoto?, manake hata mambo ya michezo ya timu za mpira hayakubaliki mambo haya lakini hapa wasomi na wataalamu wa nchi nzima wanaona ni mambo ya kawaida tu,

nchi ikubali kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi chama kilicho madarakani hakiwezi kuwa na mamlaka ya kumiliki tume ya uchaguzi au sheria za uchaguzi na kama kitakuwa mamlaka hayo basi hapo hakuna mfumo wa vyama vingi ni kupotezea watu wakati tu
 
Na kuungana kwenyewe isiwe kipindi cha kukaribia uchaguzi. Waungane mapema na kujipambanua misimamo yao, wawatembelee wananchi, wazoeleke na iwe umoja wa kudumu.
 
kwa sheria za uchaguzi zilizopo saivi na tume ya uchaguzi hii hata wakaungana upinzani wote wa tz, kenya na uganda ccm itashinda milele hata wasiibe kura hata moja watashinda tu

-kwa ufupi mfumo wetu wa vyama vingi ni kiini macho tu, mamlaka yote ya tume ya uchaguzi inatokana na kuteuliwa na mwenyekini wa chama kilichopo madarakani hiki ni kichekesho
-chama kilicho madarakani kinaweza kubadili sheria yeyote kuhusiana na jambo lolote wakati wowote au kutoa tafsiri za sheria zilizopo kama unavyopenda wao

mfumo wa upinzani wa aina yeyote unakuwa na timu mbili au zaidi zinazoshindana na kunakuwa na referee na linesman ambao hawahusiani na upande wowote wa timu hizi ,wala hakuna timu ambayo inapewa mamlaka ya kuchagua referee au linesmen hata kama timu inaumili uwanja basi haiwezi kuchagua referee wa kuendesha mechi.

na ikibidi kama timu inakuja na referee wake basi inajulikana mwanzo kuwa hapo hakuna mechi na mshindi keshajulikana kabla ya pambano kuanza

na katika jambo hili hapa ndio tunapotilia shaka upinzani kuwa nao pia wamo katika kiini macho cha kuzingua watu,kwa sababu unakubalije kucheza mechi wakati mpinzani wako anakuja na referee wake,haya si mambo ya kitoto manake hata mambo ya mchezo timu za mpira hayakubali mambo haya lakini hapa wasomi na wataalamu wa nchi nzima wanaona ni mambo ya kawaida

nchi ikubali kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi chama kilicho madarakani hakiwezi kuwa na mamlaka ya kumiliki tume ya uchaguzi au sheria za uchaguzi na kama kitakuwa mamlaka hayo basi hapo hakuna mfumo wa vyama vingi ni kupotezea watu wakati tu
Hiyo imani tu mabadiliko yanawezekana kama wanainchi wakiamua na Upinzani kujipanga vizuri tu na kuwa focused.
 
oct 25 2015 wananchi wa zanzibar tuliamua na upinzani ukajipanga na ushindi ukapatikana lakini tazama tulipofika na maamuzi yalotolewa na tume ya uchaguzi,na ile ni njia moja ya kuitumia tume ya uchaguza kunaweza kuwa na njia mia moja za kila aina
 
Tatizo kuna mayuda au tumesahau jamani ukawa? Mtu kama Lipumba eti uungane nae au ACT?
 
oct 25 2015 wananchi wa zanzibar tuliamua na upinzani ukajipanga na ushindi ukapatikana lakini tazama tulipofika na maamuzi yalotolewa na tume ya uchaguzi,na ile ni njia moja ya kuitumia tume ya uchaguza kunaweza kuwa na njia mia moja za kila aina
Kama Seif alishinda kwanini aliogopa uchaguzi wa pili??

Angeshiriki tu tena angeshinda mchana kweupe
 
Si vizuri kuionesha hadhara kama hii jinsi ulivyo mtupu kichwani.

Unajuwa Mashood Abiola baada ya kushinda uchaguzi Nigeria ni nini kilifuata?

Kama watu humu mnatumia tundu la choo kufikiri na siyo ubongo.
 
kwa ufupi mfumo wetu wa vyama vingi ni kiini macho tu, mamlaka yote ya tume ya uchaguzi inatokana na kuteuliwa na mwenyekini wa chama kilichopo madarakani hiki ni kichekesho
Katika hili unashauri wapinzani watumie mbinu gani Ili Mwenyekiti wa Chama tawala asiwe na mamlaka ya kuteua tume?kwa sababu wapinzani wamelipigia Sana kelele jambo hili lakini Chama tawala hakiko tayari kuwasikiliza kwa kuwa hapo ndipo palipo na uhai wake wa kuendelea kutawala,pengine unaweza ukawa na mbinu mbadala ya kuwasaidia wapinzani nini wafanye Ili waweze kufanikiwa.
 
Vyama vya upinzani visipotafuta mbinu mbadala wa kujenga umoja imara na kuwa na hoja bora na zenye mashiko basi CCM itaendelea kushinda ktk uchaguzi kila uchaguzi mkuu unapofika.

Watanzania wana shida nyingi sana ambazo zinahitaji kutatuliwa ni wakati muafaka wa viongozi wa siasa kuja na mbinu tofauti na zilizo zoeleka na wengi toka siku nyingi.

Watanzania wanahitaji mabadiliko ya kweli kabisa toka kwa viongozi wazalendo wa siasa.

Wapinzani wasipokuwa wamoja kuelekea 2020 basi CCM itawasambaratisha
Swala sio kuungana swala ni katiba ya Warioba ili tuwe na tume huru Siyo hii tumeccm wakisaidiana na policcm. Ninaowaamini hawajawa ma ccm ni lile jasho la Wakurya tangu zamani
 
Na kuungana kwenyewe isiwe kipindi cha kukaribia uchaguzi. Waungane mapema na kujipambanua misimamo yao, wawatembelee wananchi, wazoeleke na iwe umoja wa kudumu.
Waungane kutengeneza uji gani , we unaona kuna kiongozi ndani ya ukawa ? Mzee mamvi, Zero, Mdee, Kubeena , sugu , hawa watawale nani ? CCM mpka 2070
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Ujinga wa wananchi hasa wa vijijini ndio unaoibeba CCM hata pale ambapo wapinzani wanaposhinda CCM wameshaapa kuwa hawako tayari kuwapa nchi wapinzani kwa Karatasi ya kura,hata kwa kutumia gori la mkono CCM wataendelea kutumia Ili waendelee kuwepo madarakani,mbinu hizo ndizo zinazowafanya CCM waendelee kuwepo madarakani na siyo kwamba tatizo ni la wapinzani.
 
Mimi naona ni ujinga wa vyama vya upinzani ndio mtaji wa CCM. Nakumbuka kabla ya uchaguzi viongozi wa UKAWA walienda ikulu kuongea na JK na wakasema wamekubaliana kubadili baadhi ya vifungu vya sheria ili kuipa tume nguvu. Wakapiga picha wakala wakanywa walipo toka kimyaaaaa. Au walitaka JK ndio awakumbushe?

Kingine huwezi jenga nyumba kwa kuanzia kwenye paa badala ya msingi. Upinzani ungeanza kujiwekeza zaidi kwenye ngazi za vijiji badala ya kuanzia ngazi ya taifa. Ni rahisi kupata wenyeviti madiwani na wabunge wengi kuliko Rais. Ila ukiwa na wawakilishi wengi bungeni unaweza kubadili sheria kwa kuzitoa sheria kandamizi. Halaf mkarudi kwenye uchaguz mkiwa na nguvu.

Huu ni mtazamo wangu tu
 
Back
Top Bottom