mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,050
- 4,904
Ndugu wana JF kupitia jukwaa la siasa, nawasalimu Kwa jina la Demokrasia jibuni 'kwa pamoja tuipiganie'
Ndugu wana JF, Naomba nianze kwa kunukuu maneno machache toka katika katiba ya JMT (1977) sura ya Kwanza, ibara ndogo ya kwanza katika ibara ya 8
"(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao"
Mwisho wa kunukuu!
Ndugu wana JF, Katiba yetu ya JMT inatambua na inaelekeza vyema kabisa ya kuwa nchi yetu imepaswa kufuata misingi ya Demokrasia na haki ya jamii, Madaraka na Mamlaka yote itoke kwa wananchi, lakini ukijaribu kupima ili upate uharisia wa kile kinachoelekezwa na Katiba na kile kinachofanyika sometimes n tofauti kabisa, kwa mfano, uchaguzi uliofanyika mwaka 2020 mwezi wa 10, uligubikwa na janga kubwa liitwalo KUPITA BILA KUPINGWA, hili janga lilileta Mshangao na taharuki kubwa Sana katika jamii zetu kwani upande mmoja wa karata ulipita kwa kwa asilimia kadhaa kupitia mfumo huo lakini upande wa pili ulibaki kulalama hku ukikosa sehemu ya kwenda, hili swala liliwanyima watu haki yao ya kidemokrasia kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
Ni kwa nini hali hii ilijitokeza?
Ukifuatilia vizur viongozi wa Vyama pinzani watakwambia ni kwa sababu ya sheria mbaya za uchaguzi kitu ambacho hata Mimi nakubaliana nao,
LAKINI binafsi Mimi Nina mtazamo mwingine tofauti nikiwatazama wao nao wanamchango mkubwa katika kuididimiza Demokrasia nchini! Kwa nini nasema hivi?
1) yalipofanyika makubaliano ya kuanzishwa kwa Vyama vingi vya siasa, je viongozi hamkusoma vizur sheria zinazohusu tume ya uchaguzi ambayo wasimazi wake ( Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe) wote wanateuliwa na Raisi? Kama mlisoma mlizielewa? Kama mlizielewa mlichukua hatua gani kabla ya kuanzisha vyama vyenu? Au mlifunika kombe mwanaharamu apite ili muwe na namna ya kupiga noti? Kama ndivyo, nani alaumiwe Sasa?
2); kwa Sasa mnajukumu kubwa la kuhakikisha Yale yaliyotokea mwaka Jana yasijitokeze tena! Lakini kinachoshangaza mko unorganized! Yan chama hiki kinashiriki uchaguzi lakin kingine hakishiri kwa madai tuwe sio huru, kinachoshiriki kinaonesha wazi kina imani na tume, kwa mwendo huu mtafika kweli? Kwa nini msiwe na organization ya kisheria pasipo kuingiliana kiitikadi lakin muwe na msimamo mmoja hasa mnapotaka kushinikiza mabadiliko ya sheria? Huitaji ufunuo kutoka mbinguni ili ujulushwe kuwa hapa mnakwama mnakwama, na bila kumung'unya maneno msipo lisimamia hili naomba niwaambie CCM itatawala milele, msidhani kuwa kuwa Kuna mwana CCM atabadili sheria za uchaguzi kirahisi, thubutu..…!!! Hilo halipo maana nao wanaombea sheria zibak hivyohivyo ili wapite bila kupingwa, ili tume iwe upande wao