Vyama vya upinzani mjifunze kutokana na makosa

mnyalilungulu

Senior Member
Sep 27, 2019
170
114
Vyama vya upinzani hasa vile saba mlivyojitoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa serikali za mtaa kwa mlichokifanya iwe funzo kwenu next time msirudie tena kwa sababu mmewanyima wananchi wenyu fursa ya kuchagua na kuchaguliwa.

Tatizo lenu mnapenda kufanya mambo kisiasa, basi kwa mlichokifanya mwaka huu tunaomba mwakani kisijirudie
ni hayo tu.
 
Unajua unachokiandika au unabwabwaja tu? wanafanya mambo kisiasa? he? kumbe uchaguzi ni jambo gani ? si suala la kisiasa? Ficheni ujinga wenu wakati mwingine
 
Labda unaishi kuzimu na hujui kilichokuwa kinatokea, huo uchaguzi uliitisha wewe? Ulikaa na ccm wakakuambia serious walitaka kushindana?
 
Upinzani ilikua hauna jinsi, wote tunajua atakama vyama vyote vingeshiriki CCM wangeshinda na upinzani unalijua ilo sasa walikua wanatafuta namna ya kukwepa aibu, na ilikua raisi kwa baadhi ya vyama kususia kwakua uchaguzi huu hauna maslai ya matumbo yao mojakwa moja.

Ingelikua Uchaguzi wa wabunge na Madiwani ivi vyama visinge susia kwakua wanahisi wanaweza kubahatika kupata viti ili waendelee kupata posho na ruzuku. Uchaguzi mkuu 2020 vitashiriki kwakua ikitokea wamebahatika kupata viti bungeni basi wataendelea kufaidika ila huu uchaguzi unao wahusu wananchi mojakwamoja wameamua kutimua mbio.
 
Mtindo huu vyama havitashiriki uchaguzi mwakani technically nchi inarudi kwenye chama kimoja kama Uganda itakuwa majina tu
 
Uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika tarehe 24 Novemba 2019 umeisha kwa idadi ndogo ya waliojitokeza, baada ya vyama sita vya upinzani kujitoa hii ni mwitikio mkubwa wa watanzania kwenu mkae mkijua watanzania wanawaunga mkono sana na wanawakubali sana kwa kila jambo tumieni vizuri kukubalika kwenu na watanzania Mungu awabariki sana.
 
Amina Amina

Ulitaka wajitokeze kwenda wapi wakati 98% wagombea walipita bila kupingwa?? Waambie wasithubutu kuugomea huo ujao labda wa kuziba pengo tu au dirisha dogo litakapofunguliwa January kwa wale mnaotaka kurudi kundini kabla ya uchaguzi mkuu
 
Mnalazimisha hii issue iendane na hisia zenu tu lakini mambo ni tofauti.

Kama wagombea wao wana uhakika ya ushindi, wakapige kura ya nini sasa?

Kama unadhani wanaungwa mkono to that extent waambie waitishe maandamano tuone idadi ya hao wanaowaunga mkono barabarani!
 
Mi nadhani upinzani tuelendelee na huu msimamo wetu wa kususia chaguzi. Nashauri hivi vyama vilivyosusia uchaguzi wa serikali za mtaa viendelee kususia hadi uchaguzi mkuu mwakani ili tuionyeshe CCM kwamba tuna mtaji wa watu wengi nyuma yetu. Hii itamfanya JPM na serikali yake kupita kiulani ili aendelee kuwaletea maendeleo watz wote tukiwemo na sisi wapinzani tuliosusia pamoja na wafuasi wetu. Kwa sababu kama vyama sita vikijitoa kwenye uchaguzi kuna vyama vilivyosalia vitashiriki tu tupende tusipende.
 
Sisi tunaangalia ushindi hizo idadi za wapiga kura wawe wachache au wengi sio ishu ya chama ,chama ishu yake ushindi

State agent
Uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika tarehe 24 Novemba 2019 umeisha kwa idadi ndogo ya waliojitokeza, baada ya vyama sita vya upinzani kujitoa hii ni mwitikio mkubwa wa watanzania kwenu mkae mkijua watanzania wanawaunga mkono sana na wanawakubali sana kwa kila jambo tumieni vizuri kukubalika kwenu na watanzania Mungu awabariki sana.
 
Uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika tarehe 24 Novemba 2019 umeisha kwa idadi ndogo ya waliojitokeza, baada ya vyama sita vya upinzani kujitoa hii ni mwitikio mkubwa wa watanzania kwenu mkae mkijua watanzania wanawaunga mkono sana na wanawakubali sana kwa kila jambo tumieni vizuri kukubalika kwenu na watanzania Mungu awabariki sana.
kuna kituo kimoja huko Songea waliojiandikisha walikuwa 166 , waliojitokeza kupiga kura walikuwa watatu tu , yaani mgombea wa ccm alishinda kwa kupata kura 3 , TLP 0
 
Mpaka wanaccm wenyewe wamekataa kushangilia uchafuzi hebu ona kijiji kizima wanajitokeza watu sita kushangilia ushindi mpaka aibu ccm.
IMG_20191126_150146.jpg
 
Hapo ni kijiji cha Mdega, wilaya ya Masasi Mtwara wakishangilia ushindi wa mwenyekiti wa mtaa alipita bila kupingwa, yaani mpaka wanaccm wamewaunga mkono wapinzani wamesusa kushangilia,
IMG_20191126_150146.jpg
 
Back
Top Bottom