Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,702
- 36,124
Kuna vitu vinatufanya sisi wananchi tufanye hitimisho kuwa viongozi wakuu wa upinzani ni wabinafsi wanaojali matumbo yao tu.
Twende kwenye swali husika ambalo linavijiswali vidogo ndani yake;
- Kwanini mliususia Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 na mkakubali kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu 2020?
Je, Uchaguzi Mkuu 2020 haukuwa na viashiria vya ukiukwaji wa kanuni za Uchaguzi kama mlivyodai kwenye local government election 2019?
Je, mliususia Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwakuwa haukugusa maslahi yenu(nafasi za ubunge mlizokuwa nazo)?.
NEC mliisema sio tume huru, ilikuwaje mliingia kwenye Uchaguzi Mkuu bila kuona maboresho ndani ya hii tume?.
Mlidhani mngeutwaa ubunge kwa umaarufu wenu?
Kutokuwapigania wagombea wa serikali za mitaa 2019 kwakuwa haukugusa maslahi yenu kumesababisha na nyie mpepetwe kama ngano.