Vyama vya upinzani kubalini kugawana majimbo yaliyopo Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyama vya upinzani kubalini kugawana majimbo yaliyopo Dar

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by babayah67, Oct 12, 2010.

 1. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Zikiwa zimebaki siku kama 20 kabla ya uchaguzi mkuu, napendekeza vyama vya upinzani kugawana majimbo kama ifuatavyo: Ubungo (CHADEMA); Ilala (NCCR); Temeke (CUF); Kawe (NCCR); Kinondoni (CHADEMA); Kigamboni (CUF); Kinyerezi ( CHADEMA), Ukonga (CUF). Pia hata baada ya kufanya karibu nusu ya kampeni sehemu mbalimbali nchini, vyama vimeweza kujiona wazi majimbo gani mikoani wanakubalika na wapi chama gani hakina wafuasi ukilinganisha na chama kingine. Kwa lengo lile lile la kuitoa CCM madarakani nadhani vyama vya upinzani vinaweza kugawana majimbo hayo na kuitoa CCM madarakani. Kenya waliweza fanya hivi na wakaitoa KANU madarakani kwa nini sisi hapa tushindwe??? Wanachi tulio wengi tunataka kuitoa CCM madarakani lakini viongozi wa vyama vya upinzani mnatuangusha, kwanini hadi leo hii hamuoni haja ya kusimamisha mgombea mmoja majimboni????
   
 2. M

  Mzee Busara Senior Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni ngumu sana kujua agenda ya wapinzani. Hawataki kuungana lakini wanatoa ahadi ya kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania. Charity begin at home.
   
 3. M

  Mzee Busara Senior Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM ikishinda watadai imeiba kura kumbe ni wao wanaibiana kura kwa kuzitawanya kura kwa kila chama badala ya kujipanga kuunganisha nguvu. umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. huwezi kuwa dhaifu kisha utarajie kupata ushindi.
   
 4. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Yaani wee acha tu. Mimi huwa nafikiria hadi nakata tamaa kabisa ni kwa nini viongozi hawalioni hili suala. Toka 1995, 2000, 2005 na hivi sasa. Pamoja na kuwa wanakuja na hoja ya kuwa chaguzi zote za nyuma kura walizopata wapinzani ukizijumlisha zote hazikufikia japo nusu ya kura za CCM. Wananchi wa huko nyuma sio wa leo hii.
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Tafuta na panga uikate tamaa yako
   
 6. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mbona unataka kudidimiza demokrasia wewe,nani kakwambia demokrasia ya kweli ni ya vyama viwili,wananchi watachagua wanayempenda.Si kwamba CCM vs Upinzani,ni CCM vs Chadema vs CUF vs NCCR n.k.
   
 7. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chadema igaiwe jimbo dar kwa kazi gani waliyoifanya? Majimbo ya dar yote ni ya cuf huwa wananyan'ganywa tu.
   
 8. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kuchagua mgombea mmoja anayekubalika akiwakilisha upinzani si kuunganisha vyama. Kenya walifanya hivyo na leo bado vyama vyao tofauti vipo. Kama lengo la vyama vyote vya upinzani ni kuuondoa utawala wa CCM na kama vyote vinasimamia suala hilo, basi kwanini wasisaidiane kulifikia lengo hilo??? Toka kampeni zilipoanza na hasa baada ya kusoma na kuzisikiliza sera za vyama vya upinzani kama CUF, CHADEMA, na NCCR nimeona kuwa vyote sera zake zinawiana kwa njia moja au nyingine. Pia katika vyama hivyo vyote hakuna chama hata kimoja kinachoweza itoa CCM madarakani kwa nguvu yake chenyewe, ni katika kushirikiana pekee wataweza kupata Majority na kuipiku CCM.Vinginevyo sio siri CCM itaendelea tupende tusipende, maana BALLOT BOX WILL TELL!!!
   
 9. m

  mbea Member

  #9
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kondoo hanenepi siku ya mnada!
   
 10. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Mkuu hilo jimbo bolded lipo Dar kweli au ndo proposition? Naona Segerea huko vipi au ndo kinyerezi? Umetumia vigezo gani kuwapa NCCR Kawe? Unaamini Mbatia ananguvu kuliko Halima Mdee....
   
 11. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Yupo nje ya habari mzee.
   
 12. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kitu ambacho wadau mmesahau ni kwamba hakuna vyama vya upinzani. Neno "Upinzani" ni propaganda iliyokuzwa na chama cha mapinduzi kwa wananchi kwa kujiita chama tawala na vingine vinakipinga tu. Lakini ukweli ni kwamba vyama vyote ni vya siasa vinavyoshindana kupata uongozi kwa kunadi sera zao. Chama cha siasa kinachoshinda ndicho hupewa ridhaa ya kuongoza umma. Kila chama lengo lake ni kuongoza serikali na kuwatumikia wananchi. Kuita chama fulani tawala na vingine vya upinzani ni kuwaaminisha wananchi kuwa chama tawala ndicho chenye haki ya kuongoza dola, na vyama pinzani kazi yao ni kukosoa chama tawala tu. Hilo sio jambo la kweli vyama vyote vina haki ya kuongoza, ndio maana kila baada ya miaka mitano unafanyika uchaguzi kwa kushirikisha vyama vyote bila kubagua.
   
 13. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ni kweli mzee ni jimbo la Segerea sio Kinyerezi. Kigezo cha kuipa NCCR jimbo la kawe ni katika siasa za U-partsans tu, kwa kuwa Halima Mdee anaweza chaguliwa kupitia nafasi maalum za Chadema, basi si vibaya wakamwachia Mbatia apiganie ubunge wa kawe.
   
 14. S

  Sadi New Member

  #14
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chadema ni ccm b sasa unafikiri watakubali kuungana na wenzao? Mfano huko mbea vyama vyote vimeungana isipokuwa chademu!!!
   
 15. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Unataka kutuaminisha kwamba itikadi ya CUF na TLP ni sawa? Ama TPP Maendeleo ni sawa na UDP? DP wana itikadi sawa na CHADEMA? NCCR Mageuzi wana itikadi sawa na SAU?
  Mzee kila chama kina itikadi yake na kila chama ni mpinzani wa mwenzake. Kama unafuatilia michakato japo kidogo tu utakumbuka kuwa mwaka 2009 katika uchaguzi mdogo kule Tarime vyama vyote unavyoviita vya upinzani viliungana na CCM kuipinga CHADEMA. Sasa nani ni pandikizi wa CCM? Kumbuka Rev. Mtikila alipigwa mawe akimnadi nani?
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kwani sisi m kaungana na nani? Mashehe?
   
Loading...