VYAMA VYA UKOMBOZI AFRIKA VIJITATHIMINI KURUDISHA IMANI KWA WANANCHI

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
183
ed24b84a35b8c8ea212a1a0779c2ccc3.jpg


Hatua ya Kushinda Dola kwa vyama vya Upinzani barani Afrika ni ishara mbaya sana kwa Vyama vya ukombozi barani Afrika inaonesha zinahitajika nguvu za ziada ili kuwaaminisha tena wananchi nia thabiti ya Vyama vya Ukombozi kuhusiana na kuwakomboa wananchi na kwa namna. Ipi.

Anguko la Vyama tawala hususani kwa miaka hii ya karibuni mfano Gambia, Nigeria Ghana no ishara kuwa wananchi hawwna Imani tena na vyama hivo licha ya kuwasaidia kutoka kipindi kigumu cha umwagaji Damu na mateso kutoka kwa wakoloni wa Zamani ambao walisambaza mfumo wao wa kibepari na Unyonyaji Afrika.

Sababu kubwa ya Vyama vingi vya ukombozi kudondokea Pua katika Chaguzi nyingi Afrika ni kurejesha mifumo ya kibepari kama ilivuokuwa wakati wa Ukoloni ambapo Viongozi wake hushindwa kiwaheshimu wanaowaongoza, kwa kufanya maamuzi kwa Maslahi ya Taifa. Badala yake hutumia njia walizopatia uhuru kutawala wananchi katika Karne ya sasa ambayo ni Uwazi na uhuru wa maoni ndio sera ya Dunia

Sasa hali imebadilika barani Afrika wananchi wengi wamechange Upepo wameanza kuvidhania Vyama vya Upinzani ndio vyama vipya vya ukombozi katika karne hii 21 sababu zikiwa vyama vya Ukombozi wanaendeleza waliyokuwa wskiyapiga vita na kupinga vikali katika karne ya 15 na 14, Kuna haja kubwa kwa vyama vya Ukombozi Afrika kujitathmini upya na kujua wapi viliteeleza ili virejeshe imani mpya kwa Wananchi naamini bado vinapendwa.

[HASHTAG]#kijanamzalendo[/HASHTAG] [HASHTAG]#ilovetz[/HASHTAG] [HASHTAG]#maoniyangu[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom