Vyama vya siasa vyamvaa Waziri Muhongo vimempa siku 90 Rais Jakaya Kikwete kumwajibisha

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,571
[h=2] [/h] Jumatano, Novemba 28, 2012 04:52 Na Amina Omari, Tanga


VYAMA vya upinzani mkoani Tanga, vimempa siku 90 Rais Jakaya Kikwete kumwajibisha Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Vyama hivyo, vimefikia hatua hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa, Waziri Muhongo alitoa maneno ya kashfa dhidi ya wananchi wa Mkoa wa Tanga, kuwa hawapendi kazi.

Wakitoa tamko kwa waandishi jana, Katibu wa Chama cha PPT Maendeleo Mkoa wa Tanga, Ramadhani Manyeko alisema, Waziri Muhongo alitumia muda mwingi kutoa hotuba ya kukejeli, jambo lililowakwaza viongozi hao.

Alisema hatua ya kwanza ni kumtaka Waziri Muhongo kuomba radhi, lakini pia atafute mbinu na mikakati itakayosaidia kuwatoa watu wa Tanga katika umaskini walionao.

Naye, Mwakilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Jonathan Bahweje alisema kauli za Muhongo ni za kejeli hazipaswi kuvumiliwa.

“Muhongo amediriki kutuita sisi viongozi wa vyama vya siasa kuwa ni watu wa mitaani, wenye elimu duni tena ya ngumbalo,” alisema Bahweje.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Rashid Amir alisema kauli ya Waziri Muhongo imewaondolea heshima na utu wakazi wa mkoa wake.

“Huyu Muhongo aliwahi kuonywa na Spika wa Bunge, Anne Makinda na kutakiwa aache tabia ya kusema mambo ambayo hana nayo uhakika,” alisema Amiri.

Katika kikao hicho, Waziri Muhongo aliwahakikishia wadau waliyotaka kujua hatima ya mgawo wa umeme ambapo alipinga na kudai hakuna kitu kama hicho.

Wiki iliyopita, Waziri Muhongo katika mkutano wake na wadau wa madini uliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, anadaiwa kutoa maneno ya kejeli kwa wadau hao wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa ni watu wenye elimu duni, maskini, wapuuzi wapenda harusi na wavivu tegemezi.
 
R.B Mengine ni maneno ya kisiasa. mwonyesheni kuwa nyinyi sio watu wa mitaani, mna elimu-wanasiasa), sio wavivu-watu wa Tanga, basi mtamaliza ubishi. Hivi kweli Tanga hakuna umwinyi wa kutofanya kazi? Tusiwe na hasira bila kufanya critical assessment. Tanga kweli hakuna harusi za kuziba barabara. Turekebishe tamaduni/mila zingine bwana-
 
Last edited by a moderator:
Lusinde alishachukuliwa hatua gani kwa matusi aliyoyamwaga pale Arumeru Mashariki? Hizo ndizo sera za CCM!


Excellent....!!!!

Watu wa Tanga around 90% ni WAVIVU..... hili si tusi ni mjinga tu atasema tusi.... so kuwaambia ukweli imekuwa tatizo..? Umaskini wa watu wa Tanga ni kuacha UVIVU NA KUFANYAKAZI KWA BIDII..... wasome, walime, wafanye biashara kwa bidii na maarifaa.... kazi kukaa tu ....

Sasa Waziri katukana hapa ....!!!

Ila kwsbb wanapinga hii kauli ya waache uvivu.... Basi WAENDELEZE UVIVU wabakie walivyo.....

The world is moving too fast.... shauri yao...
 
Mh maneno haya makali wacha nipite kwanza .Tanga nadhani kuna madrasa nyingi kuliko madarasa .
 
A typical speech from a ccm cadre!! It reminds me of Kikwete's stupid speech to public servants!
 
haka ka mfano ka uvivu na watanga kukataa na kuona kuwa wametukanwa, ni sawa tu na kundi kubwa linaloamini kuwa maendeleo yanaletwa na watu fulani na wapo wamekaa wakilalama wakisubiria hilo.
Bila kujua na kutekeleza wajibu wao.
 
Huyu si mwanasiasa kwaiyo wanasiasa watofautishe. Hakuwahi kugombea ubunge na wala hatarajii ubunge wa kugombea. Ubunge wake ni wa kuteuliwa ili awe waziri.
 
excellent....!!!!

Watu wa tanga around 90% ni wavivu..... Hili si tusi ni mjinga tu atasema tusi.... So kuwaambia ukweli imekuwa tatizo..? Umaskini wa watu wa tanga ni kuacha uvivu na kufanyakazi kwa bidii..... Wasome, walime, wafanye biashara kwa bidii na maarifaa.... Kazi kukaa tu ....

Sasa waziri katukana hapa ....!!!

Ila kwsbb wanapinga hii kauli ya waache uvivu.... Basi waendeleze uvivu wabakie walivyo.....

The world is moving too fast.... Shauri yao...

ukweli unauma. Watu hawapendi ukweli. Acheni maneno mengi. Watu wa tanga tuchape kazi.
 
Aende na Moshi akawaambie Wachagga wezi, aende na Bukoba akawaambie Wahaya ..... Aende Mwanza na Shinyanga akawaambie Wasukuma washamba, aende Rukwa akawaambie Wafipa wachawi na wanga wakubwa, the list is endless, basi si atakuwa na kazi kubwa, na nyie mnaokubaliana nae si ndio Wapumbavu wakubwa wa nchi hii!
 
Na ikithibitika kuwa kweli wenyeji wa Tanga hawapendi kufanya kazi mtafanyaje?
 
Aende na Moshi akawaambie Wachagga wezi, aende na Bukoba akawaambie Wahaya .....Aende Mwanza na Shinyanga akawaambie Wasukuma washamba, aende Rukwa akawaambie Wafipa wachawi na wanga wakubwa, the list is endless, basi si atakuwa na kazi kubwa, na nyie mnaokubaliana nae si ndio Wapumbavu wakubwa wa nchi hii!

Bukoba akawaambie Wahaya .....???????????????????????
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom