Vyama vya siasa visiuteke mchakato wa katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyama vya siasa visiuteke mchakato wa katiba mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Nov 28, 2011.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  katiba ya nchi si katiba ya vyama vya siasa,
  vyama vya siasa visi "take" advantage kujitafutia umaarufu kwenye suala la katiba mpya,
  hapa watanzania wote tuna nafasi sawa ya kuandaa tanzania yetu ya kesho,si jukumu la yule.
  nawajua sana wana siasa kwa kuteka hoja kwa maslahi ya kisiasa,wanatabia ya kuteka hata misiba...
  kila anayejiita mtanzania ashiriki mchakato huu ipasavyo ili tupate katiba ya wananchi inayotokana na wananchi wenyewe na si katiba kwa ajili ya wananchi.
  Nawasilisha.
   
 2. i

  iwensato Member

  #2
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Suala la katiba ni suala la watu wote na makundi mbalimbali. Linapotokea kundi fulani linazungumzia katIba na kundi lingine likakaa kimya kundi linalokaa kimya lisipige kelele eti kundi fulani linateka mjadala wa katiba ni upuuzi; nani kakukataza kushiriki ukiwa kama kikundi au mtu binafsi?

  Wenye hoja acheni wajenge hoja na wanaokaa kmya waache wakae kimya. HAPANA KULAUMU.
   
 3. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #3
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoa hoja hujaweka hoja yako sawa usikurupuke. Weka wazi ni vyama gani vya siasa unavyovilenga kwa maana kama ni kutekwa hoja, ilishatekwa na vyama vya CCM na CUF pale walipopitisha muswada kabla ya wananchi kuujadili jambo ambalo CDM hawakubaliani nalo. Weka hoja yako vizuri ueleweke ingawa kimsingi ilishapitwa na wakati.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Naunga mkono hoja.... Naona chadema na ccm wanataka kutupigisha siasa wakati katiba iko kisheria na utawala zaidi

  naanza kuhisi ngiri na nguruwe lao ni moja
   
Loading...