Vyama vya siasa viachane na mtindo wa kujenga maofisi

Malata Junior

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
3,102
2,538
Heshima mbele wakuu.

Kumekuwa na utamaduni wa vyama vya siasa hasa CCM kuwa na majengo wanayoyaita ofisi nchi nzima kuanzia ngazi ya tawi hadi Taifa.Mfumo huu waliuchukua kutoka vyama vya kikomunisti ambayo na vyenyewe vimeshautupilia mbali!

Vyama vyote vikubwa vya siasa duniani hasa vya nchi za magharibi na Marekani huwezi kukuta eti ofisi ya tawi la chama cha Republican, Democrat,Labour, Conservative nk,au ukisikia wanachama wa vyama hivyo wakijenga ofisi ya tawi,kata,wilaya,mkoa nk.

Vyama vya siasa havitakiwi pia kuwa na watumishi wa kuajiriwa bali viongozi wote wa vyama wawe na shughuli zao za kujipatia kipato na si wanasiasa kukaa kwenye maofisi hayo wakijiita makatibu,waratibu,wakurugenzi nk wakati hawazalishi kitu!

Kwa kuwa teknolojia imekuwa vyama sasa vijiendeshe kidigitali kwa kusajili wanachama, wagombea, kutangaza Sera,ilani na kutoa taarifa muhimu kwa njia ya mtandao.Na hili katibu wa chama amaweza kulifanya baada ya shughuli zake za kawaida na si kukaa ofisini siku nzima!

Nakumbuka baada ya ubinafsishaji baadhi ya mabenki yaliuza majengo yote na kupanga kwa kuwa biashara yao haiitaji kumiliki majengo yao mwenyewe!

Ukipita maeneo mengi ya vijijini na mijini utakuta ofisi za CCM za matawi na kata zimefungwa muda mrefu,sasa huu upotevu wa rasilimali kwa kuweka majengo yasiyo na tija.

Kwa bahati mbaya vyama vya upinzani Tanzania navyo vimefuata mkumbo huo.Kwa mfano CHADEMA wamejitahidi kujenga ofisi za matawi na kata katika maeneo machache kwa nguvu za wanachama na sehemu nyingine wamepanga ofisi lakini mambo Ni kama yale yale ya CCM, ofisi zimefungwa muda mrefu,upotevu wa rasilimali!

Ushauri wangu kama vyama vinataka kuendelea kuwa na ofisi basi viwe na ofisi za majimbo tu,ofisi za matawi,kata,wilaya na mikoa zote zifutwe,ofisi za majimbo ziratibu shughuli zote za chama karaka vijiji, mitaa na kata.Kwa CHADEMA ambayo mimi Ni mwanachama wanaweza kubakiza ofisi za kanda na kufuta ile ya makao makuu. Shughuli za makao makuu zitafanyika ndani ya ofisi za Dar es salaam kuu (Greater Dar es salaam)
 
Back
Top Bottom