Vyama vya siasa tushiriki uchaguzi jimbo la Muhambwe

Nguruka

Senior Member
Dec 6, 2006
180
124
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC jana ilitoa matangazo magazetini kubusiana na uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge Jimbo la Muhambwe huko Kibondo mkoani Kigoma.

Hivyo NEC wametoa fursa kwa vyama kutafuta Wagombea wa kuziba nafasi hiyo baada ya Mbunge aliyekua wa jimbo hilo kufariki Dunia Februari 12,2021 kwa ajali akiwa jijini Dodoma.

Hima sasa wanasiasa kupitia vyama mbalimbali kujitokeza na kuwania nafasi hiyo. Rai yangu ni kwa vyama tuhakikishe tunashiriki kinyang'anyiro hicho pasipo kuleta mambo ya kususia Uchaguzi.

Kusisia Uchaguzi kama huo kunaweza kuwa na matokeo mabaya huko mbele katika ulingo wa kisiasa kwani wananchi wanaweza chukulia mara zote Chama X ni wasusasi na hawanademokrasia kama Chama Z na F.

Hivyo basi ni vyema vyama vilivyo na usajili wa kudumu kujitokeza kwa mujibu wa kalenda ya Uchaguzi huo na kuwania nafasi hiyo na kuwawakilisha wananchi wa Muhambwe Bungeni. Kamwage sera kwa wananchi ambao ni wapiga kura na hakika sera zako zitakuwezesha kutwaa kiti hicho.

Kususia chaguzi yeyote ile ni kuwanyima Wanachama wako fursa ya kuongoza.


Screenshot_2021-03-28-10-45-05-97.jpg
 
Inatakikana Tume huru ya Uchaguzi,Mkurugenzi hawezi mtaja mpinzani kuwa mshindi wakati analipwa na serikali,anajaziwa mafuta na posho mbalimbali.

Watangaze mshindi ccm tuokoe fedha za umma.
 
Back
Top Bottom