Vyama vya siasa Tanzania vina brand strategists? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyama vya siasa Tanzania vina brand strategists?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kafara, Apr 11, 2009.

 1. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  cocacola, ibm, nokia, nk zinahesabika kwamba ni "brands" zenye thamani sana. kwa maana nyingine "brands" hizi zinaheshimika kwa nguvu zake sokoni. makampuni yenye brands hizi yanawivu sana na brands zake na siku zote yapo makini na tayari kuzilinda brands hizo. kuondoka kwa meneja mkuu au mtendaji yeyote yule katika hizi kampuni kunaweza kutikisa kampuni lakini ni vigumu kuvunja nguvu za brand hizi. brand hizi zinaweza kushuka thamani pale ambapo bidhaa zake zitakapoacha kukidhi ahadi kwa mteja zinazozizunguka brand hizi, jina la brand litakapokuwa diluted kwa bidhaa hafifu (zinazotengenezwa na makampuni mengine) zinazotumia brand za haya makampuni. aidha brand hizi zinaweza shuka thamani pale ambapo bidhaa mpya shindani yenye ubora kuliko bidhaa za makampuni haya itakapojitokeza sokoni.

  kwa mtazamo wangu kutokana na historia yetu ccm imeweza kujitengenezea "brand" imara sana. sifahamu kama ndani ya ccm wapo wataalamu wa mkakati wa kuimarisha "brand ccm". aidha ccm kwa muda mrefu imeweza kuwaaminisha watanzania kwamba bidhaa inazotengeneza ni bora na hakuna chama (brand) kingine cha siasa kinachoweza kutoa bidha bora kama zao (yaani siasa safi, amani, uongozi bora nk). kwa kiasi kikubwa hili limefanikiwa.

  wakati tukielekea kwenye uchaguzi 2010 ni vyema vyama vya upinzani vikajipima ni kwa kiasi gani nao brand (mfano chadema, cuf, tlp, nccr-mageuzi nk) zao ziko imara. je wao wanawaahidi watanzania bidhaa gani zaidi ya zile zinazouzwa na ccm. na kama watauza bidhaa sawa na ccm je zitakuwa na ubora gani kuliko hizi bidhaa zinazobebwa na brand ccm?

  katika vita dhidi ya ufisadi naona ccm imekuwa ikijitahidi sana kuhakikisha kwamba ufisadi hauunganishwi moja kwa moja na brand ccm. kwa mfano masuala ya epa hususan kagoda. ccm imekuwa tayari na kwa mtazamo wangu imeachia majina ya wanachama wake yatajwe kama watu binafsi na sio kama sehemu ya ccm. hivyo brand ccm inaendelea kuwa imara. nionavyo mimi wanachama waliomo ccm na ambao hawakubaliani na mambo ya serikali ya ccm wanashindwa kutoka kwani nao wanaamini nje ya brand ccm hakuna chama chenye brand yenye nguvu kama ccm. katika mpambano wa kisiasa tunaona mashambulizi yanayofanywa ili kuua/kuzuia ukuaji wa brand za vyama vya upinzani (mfano ukabila na udini unaohusishwa na baadhi ya vyama vya upinzani)

  upande wa vyama vya upinzani naona zaidi mafanikio yanahusishwa zaidi na viongozi na sio chama (brand) hivyo watu binafsi mf. mrema, sheriff, zitto, slaa, wangwe (rip) nk ndio wanaonekana zaidi ya brands za vyama vyao na kwa hali hii brand haikui bali watu.

  hata hivyo natambua yaliyotokea tarime kule uwezekano mkubwa brand chadema ilikuwa imara na inaelekea wapinzani wa chadema hawakuliona hilo. labda operation sangara inaweza kuimarisha brand chadema sehemu nyingine.

  swali ni jee vyama vyetu vya kisiasa vinamikakati ya makusudi ya kuimarisha brands zao au ndio mambo ni kibahatibahati tu?
   
 2. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kafara,

  UDP walikuwa na Mapesa, CUF ni Utajirisho, sina uhakika kuhusu Chadema, TLP, DP au NCCR!

  Lakini pamoja na mahubiri ya Mapesa au Utajirisho, hakuna hata mmoja wao ambaye ameweza kujijenga kwa brand name zaidi ya kudai tunataka tuing'oe CCM kwanza!

  Je wanawezaje kutuuzia sisi bidhaa tuiamini ikiwa wnasema hawawezi kutuonyesha ubora wa bidhaa zao mpaka waingie Ikulu?

  Ndio maana CCM wanabakia kutawala!
   
 3. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  rev.

  naona hapo ndio walikosea zaidi kwani wao wamekuja na "slogans" wakidhani ni brands. brands ni kitu kikubwa zaidi misemo. si unaona misemo ya ari mpya imepwaya na ccm wala hawaikumbushii siku hizi kwa hofu ya kudhoofisha brand ccm.
   
Loading...