Vyama vya Siasa Tanzania na Watanzania Waishio Ughaibuni (Diaspora)

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na harakati nyingi za vyama vya siasa (hasa CHADEMA na CCM) kutafuta wanachama na kufungua matawi ya vyama husika huko ughaibuni.

Ningependa kufahamu siri iliyojificha katika harakati hizo kwani ninavyofahamu mimi mpaka sasa nchi yetu haina utaratibu wa kuwashirikisha wananchi waishio nje ya nchi katika kupiga kura. Pengine hoja yangu ya msingi ni kwamba ni kwa namna gani harakati hizo ni sehemu ya suluhisho la matatizo yaliyoko nyumbani (Tanzania)?
 
Tumeona CDM UK wamechanga magari mawili ya wagonjwa, CDM huchangishana wenyewe kuyafungua matawi yao.
Tumeona CCM ilivyotumia zaidi ya $30,000 kuwaleta Kinana na Diamond kufungua tawi Washington DC
Kwa kifupi hizo ni tofauti kidogo nilizozioona
 
Sababu hasa ni kuandaa mazingira ya kwenda mtoni kutembea siku za mbeleni kwa kisingizio wanaenda kukagua matawi.
.Kutoa ajira na deal za hapa na pale kwa watoto wao na malaya wao (ccm) kwa cdm ni njia ya kupata michango ili kitu m4c isonge mbele kumfikia babu yako na wajomba zako kule tandahimba, likuyufusi, mkanyageni na pale kiagata musoma.
 
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na harakati nyingi za vyama vya siasa (hasa CHADEMA na CCM) kutafuta wanachama na kufungua matawi ya vyama husika huko ughaibuni.

Ningependa kufahamu siri iliyojificha katika harakati hizo kwani ninavyofahamu mimi mpaka sasa nchi yetu haina utaratibu wa kuwashirikisha wananchi waishio nje ya nchi katika kupiga kura. Pengine hoja yangu ya msingi ni kwamba ni kwa namna gani harakati hizo ni sehemu ya suluhisho la matatizo yaliyoko nyumbani (Tanzania)?

1. Kupata michango inayoweza kusaidia kuendesha majukumu ya kichama (Kwa kuwauzia kadi kama ilivyo kwa wengine Tanzania na kuwashirikisha kwenye mikakati ya maendeleo)
2. Naamini watapiga kura 2015 kwa sababu tupo kwenye mchakato wa mabadiliko ya katiba (Hilo ni sehemu ya mapendekezo ya wengi)
 
katika siku za hivi karibuni kumekuwa na harakati nyingi za vyama vya siasa (hasa chadema na ccm) kutafuta wanachama na kufungua matawi ya vyama husika huko ughaibuni.
,
ningependa kufahamu siri iliyojificha katika harakati hizo kwani ninavyofahamu mimi mpaka sasa nchi yetu haina utaratibu wa kuwashirikisha wananchi waishio nje ya nchi katika kupiga kura. Pengine hoja yangu ya msingi ni kwamba ni kwa namna gani harakati hizo ni sehemu ya suluhisho la matatizo yaliyoko nyumbani (tanzania)?
sipendi maisha ya kukaa nje[ uk} ,nina hakika siku moja nitarudi nyumbani tz siku moja . Tukiangalia maisha ya watanzanzia kwa sasa hatustahili tuwe hivyo , rushwa na ubadhirifu kila kona na mikataba mibovu kila mahali. Walioko madarakani wamejisahao . Bila ya msukumo toka ndani na nje wataendelea kubaki madarakani milele. Ingawaje uwezo wa kubiga kura ugenini haupo mchango wetu wa hali na mali
unaweza kuleta mabadiliko. Mungu ibariki tz
 
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na harakati nyingi za vyama vya siasa (hasa CHADEMA na CCM) kutafuta wanachama na kufungua matawi ya vyama husika huko ughaibuni.

Ningependa kufahamu siri iliyojificha katika harakati hizo kwani ninavyofahamu mimi mpaka sasa nchi yetu haina utaratibu wa kuwashirikisha wananchi waishio nje ya nchi katika kupiga kura. Pengine hoja yangu ya msingi ni kwamba ni kwa namna gani harakati hizo ni sehemu ya suluhisho la matatizo yaliyoko nyumbani (Tanzania)?

I wouldn't worry so much kuhusu hayo matawi its only a few ambitious people dragging the lots into party politics for their own gains, particularly getting into politics through party acknowledgement. These people expect their efforts to recruit and promotions of the party to be rewarded in the future it has worked so far one or two have been given positions in the current gov, but those vying for parliament seats have along way to go on CCM side.

Wengine ni sherehe tu na soda ndio kikubwa kinachowapeleka lakini siasa wala haziwashughulishi maisha yanaboa wakati mwengine unajua. Hila viongozi wengine wa hivyo vyama 'mmmmmh' may be they should stick with their day jobs.
 
Dhumuni kubwa ni Kujitanua na Uhamasishaji wa siasa za kwetu kwa minajili unaweza ukakaa nje lakini unaweza kujua siasa za Nchi yako na kushiriki kwenye vikao vya chama chako Husika hata kama uko mbali..

Na Matawi haya yanajiendesha kwa Michango yao wenyewe ya wenye tawi husika labda kama kutakuwa na Mfuko ambayo wafadhil watatupia sarafu.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom