Vyama vya siasa Tanzania longo longo tupu

gango2

JF-Expert Member
Aug 31, 2011
1,941
2,251
hakuna kubisha vyama vyetu vyote vya siasa tanzania vimejaa longolongo tupu, masilai binafsi ya viongozi wa vyama hivyo na UOGA KWA WANACHAMA...na ndo mana hatuendelei

leo hii akitokea mwanachama yeyote kutaka kugombea nafasi ya juu ya chama, basi matatizo tena anaishia kufukuzwa katika chama....sasa huku sio kukomaa kisiasa ni upumbavu...

watu kama kina Mrema, Cheyo, Maalim seif, LIPUMBA, Mbowe, SLAA, MBATIA wamekumbati madaraka ya chama kiasi kwamba haruhusiwi mtu kugombea nafasi hizo za juu. tumeshuhudia matukio mengi ambapo baadhi ya wanachama wanapojitokeza kugombea au wanapokuwa wanakubalika na kuwa tishio kwa wakubwa wa vyama vyao zinaibuka longo longo nyiiiiingi, kiasi kwamba tunakereka wanachama.

hebu waulizeni hawa watu wanavyopata/walivyopata shuruba...PROFESA SAFARI(CUF), HAMADI RASHID(CUF), MARANDO (Enzi hizo NCCR), KAFULILA (NCCR), SHIBUDA (ENZI HIZO CCM) na wengine wengi...


hebu tujifunzeni kwa wenzetu wanaopokezana madaraka, mfano mzuri ni REPUBLICAN na democratic part huko marekani.....

tunakereka sana wanasiasa wetu wanapojitokeza kutaka kuleta mabadiliko kunyanyaswa na kuchukuliwa hatua za kinidhamu....
 
Back
Top Bottom