Vyama vya siasa ni adui kwa mwananchi

nkumbison

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
2,219
2,969
Kwanza huwa vinadandia hoja za sisi wananchi nakujifanya wao ndio wanauchungu kuliko sisi huku kiuhalisia sio kweli maana hakuna kiongozi wala mpambe wa chama chochote cha siasa atakayeacha shughuri zake bila kuwa na uhakika wa kupata chakula eti akakipigie debe.

Swali ninalojiuliza hivi inawezekana mwenye shibe akamtetea mwenye njaa?

wanakuja kwetu kujisifu na wengine kulalamika kuonewa, wananchi tukiamua kuchukua hatua wanakuja tena nakututaka tuahirishe yale tunayoyaona yatatupeleka katika ustaarabu na kuheshimiana bila kuoneana.

Swali ninalojiuliza ina maan wanavyokuja kwetu kutulilia wanaonewa wengine kujisifu wanatekeleza mambo yao huwa wanataka sisi tufanye nini?

Kwakifupi hakuna chama cha siasa chenye lengo lakumkomboa Mwananchi kutoka katika changamoto zinazomkwamisha kufanya maendeleo ya hali na mali zaidi ya Vyama vinavyotaka kumtumia mwananchi ili kiingie madarakani.

Swali ninalojiuliza, kama uchaguzi huwa sio wa haki kutokana na tume kusimamiwa na refa aliyechaguliwa na kocha wa timu shindani, kuna haja gani yakupaniki au kuwashawishi watu wanaoijua hiyo hali na pengine ni kutokana na kuelezwa na vyama hivyo hivyo hali halisi so kosa la Mwananchi ni lipi akiamua kufanya maamuzi magumu ili Mambo yaje kukaa sawa.

Kiukweli nilitegemea vyama vya siasa kugomea shughuri za kisiasa ikiwa ni pamoja na kuwashawishi wananchi wasishiriki mpaka yale yatakayokuwa ya haki na halali yatakapotekelezwa ila wao ndio wa kwanza kututaka tuyapuuze waliyokua wanayapigia kelele.

Hapa napata jibu, vyovyote iwavyo vyama vinataka utawala tuu sio uongozi maan hawatuongozi kwenye kuidai haki yetu usawa na halali ya maamuzi yetu.

Hivi kwahutuba za raisi na wanachama wa chama tawala kuna mpinzani wakuthubutu kuwaambia watu wakajiandikishe?

Kwahotuba hizohizo na wapambe wanaotuaminisha wananchi tumeielewa hii awamu kiasi chakutaka hata uchaguzi usiwepo je hii watu kugomea kujiandikisha si ndio ishara ya ushindi waliokuwa wanaunadi, kwanini wasifurahi nakusema wamepita bila kupingwa maana wananchi tunayaelewa wayafanyalo lakini wao ndio imekua hadi vitisho, tatizo nini?

Kuna haja yakuanzisha Chama Cha Wananchi kinachounga mkono wayatakayo wananchi lama hivi sasa watu hawataki kuchagua matokeo wayajuayo iwe kwa kuonewa au kwakuukubali ushindi.

Vyama Vya Siasa Tuacheni Na Maamuzi Yetu.

Maana sijui ni kwanini

WANAOTAKA KUPIGIWA KURA NDIO WANAHAMASA KULIKO WANAOTAKIWA KUPIGA KURA.
 
Umechelewa sana kugundua ya kwamba Tanzania tuna wajasiriamali wa siasa na siyo wanasiasa. Kwao, siasa ni ajira. Miaka nenda miaka rudi, huendesha maisha yao kwa kutegemea siasa.

Nje ya ulingo wa siasa, hawana tofauti na samaki aliyevuliwa majini na kuachwa nchi kavu! Wanatapatapa kweli kweli! Na mwisho kabisa huishiwa pumzi na nguvu, na hivyo kujifia tu kifo cha mende.
 
Bahati mbaya zaidi mmekuja na lawama zaidi bila kuleta solution, ni namna gani mwananchi awe na sauti (nguvu) ktk mustkbali wa uongozi wa nchi. Watawala daima hawapendi wananchi wajielewe

Lakini Wananchi kote duniani hupitia vyama hivi kufikia malengo yao ya kujiongoza. Ukiondoa nchi zenye wafalme watendaji . Kwa hiyo unapopaumu vyama lete na solution ni njia ipi ya kupita. Kwani kwetu hapa serikali inajitahidi usiku na mchana kusiwe na mgombea binafsi.
 
Kama ulivyoelezea kwenye huo mstari wako wa mwisho, labda mgombea binafsi ndiyo suluhisho peke kwa sasa! Ila siyo hivyo vyama vya siasa ambavyo kimsingi vimegawanyika makundi mawili. Vyama maslahi na vyama mamluki.
 
Wananchi hawa unaowapigania hawawezi hata kujipigania kudai katiba nzuri inayowapa nguvu dhidi ya watawala. Wamebaki watu wa kupigwa propaganda na kufuata maelekezo ya vyama hasa watawala . Laiti wananchi wangekuwa na chembe ya ujasiri wa kuhoji na kukataa maelekezo potofu ya vyama na watawala usingeyasema haya . Lakini WaTz ni waoga na hata wawakilishi ambao wapo kikatiba nao ni waoga na wamekunja mikia kwa vyama.
 
Back
Top Bottom