pierre buyoya
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 476
- 163
Instagram @pierrebuyoya
Vyama vya siasa nchini ikiwa ni pamoja na chama tawala, Chama cha Mapinduzi CCM ni Majipu yaliofunika majipu, Ila sina mashaka sana na CCM kwa sababu hivi karibuni kinara wa kutumbua majipu nchini Mhe. Rais John Magufuli atakuwa mwenyekiti hivyo tatzo hlo litakuwa Historia . . .
Napata mashaka makubwa sana ni nani atajitoa kutumbua majipu ndani ya Vyama vya upinzani, ikiwa wafuasi wake wanaamini kuwa vyama vyao ni visafi ukiachilia mbali wale wanaoweka mbele maslahi ya Taifa . . .
Ripoti ya CAG iliyotolewa hivi karibuni inaonyesha mpaka sasa vyama 21 havijapeleka hesabu zao za fedha kukaguliwa. Ni chama kimoja tu ndiyo kimewasilisha ripoti ya ukaguzi kwa CAG, ambacho ni Chama cha Wananchi (CUF). . .
Rais Magufuli ana kazi kubwa sana ya kusafisha nchi na Chama chake CCM, Basi viongozi wa vyama vya upinzani tunaomba mtusaidie kusafisha vyama vyenu ili kuipa tumaini jipya Tanzania . . .