Vyama Vya Siasa Msingi Wa Ujenzi Wa Vijana Wenye Uchungu Wa Kuchuma? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyama Vya Siasa Msingi Wa Ujenzi Wa Vijana Wenye Uchungu Wa Kuchuma?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Jul 11, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145

  Vyama Vya Siasa Msingi Wa Ujenzi Wa Vijana Wenye Uchungu Wa Kuchuma?


  Vyama vya Siasa ndio msingi wa ujenzi wa vijana ambao ndio viongozi wa Taifa la leo na kesho.Kwa mfumo wa mbio za vijiti vijana wanachukua uzoefu toka kwa watangulizi wao kisha,kupitia busara na maelekezo ya waliowatangulia vijana wanajifunza mazuri kisha kwa kupitia hayo mazuri wanatumia karama ya mapaji ya muumba kuweza kuendesha maisha ya wanajamii wenzao na hivyo Taifa kusonga mbele kupitia zama na vitabu vya wakati husika.

  Napata shida sana,kila ninapowaona vijana, walioko kwenye vyama vya siasa,kama alama ya viongozi wa kesho wa Taifa la kesho.Hakika viongozi vijana wanaotawala majukwaa yetu kisiasa kwa vyama vyote vya siasa,hakika ni tishio kubwa sana kwa Taifa.

  Kupitia ujana ni mategemeo ya Taifa kupata nyakati mpya zikiwa na matarajio mapya ya ujenzi wa Taifa letu.Je vijana hawa walio kwenye siasa za sasa zenye ukakasi wa ufisadi ni alama ya anguko la kizazi kilichotakiwa kulithi changamoto zenye fikra mpya,kimeelemewa na kuwa kizazi cha vijana walioingia kwenye siasa wakiwa na kiu si kuweka mchango wa kujenga na kukuza Taifa,bali KUCHUMA NA KUPATA HESHIMA JINA [Popularity].

  Ni mbaya sana kwa viijana,kufilisika akili,kwa kuwa vijana ni tegemeo na nguzo ya Taifa,Taifa lolote lile linategemea vijana kuwa walithi wa jamii tanagulizi katika ujenzi wa Taifa,katika kada mbalimbali kama viongozi wa kisiasa,taasisi,biashara,na kazi zingine ili kuleta ustawi wa Taifa.

  Kwa sababu vijana ambao ndio nguzo kuu ya Taifa,wanatoa ishara ya kuwa mwenendo huu,Taifa linajiundia Taifa TEKETEKE [Instability] lenye viongozi maslahi binafsi zaidi,kuliko vijana ambao wao ndio kiu ya ujenzi.

  Lawama ziende kwa nani dhidi ya viongozi vijana tulionao sasa wenye kujali maslahi na umaarufu kuliko dhumuni kuu la kuwatumikia wananchi?
  1: Vyama Siasa 2: Wananchi 3: Serikali 4: Mfumo 5: Viongozi wa vyama vya siasa au 6: Nguvu toka nje.
   
Loading...