Vyama vya kimapinduzi huteka haki za Raia

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,883
35,165
Wakati fulani nilikuwa nashangazwa ni kwa nini mpaka sasa Zanzibar kuna kitu kinachoitwa "Baraza la Mapinduzi" miaka zaidi ya 55 tangu Mapinduzi ya Zanzibar kutokea. Hivi ni watu wangapi waliokuwepo kwenye mapinduzi yale ambao mpaka leo bado wamo kwenye hilo linaloitwa Baraza la Mapinduzi.

Lakini pia nikikumbuka jinsi watu wa ASP walivyong'ang'ania kwamba ni lazima neno "Mapinduzi" liwemo kwenye jina la chama kitakachotokea baada ya ASP na TANU kuungana, naona ni kwa nini vyama vya kimapinduzi huamini kwenye mapinduzi maisha yao yote.

Leo ukiiangalia CCM utaelewa ni kwa nini chama hicho kinaamini kitatawala Tanzania milele. CCM inaamini hivyo kwa sababu ni kawaida kwa vyama vya kimapinduzi kuamini vyenyewe ndivyo nchi na wananchi na vyama vingine siyo wananchi wala si watu wenye haki ambayo chama cha kimapinduzi inaamini inacho.

Chama kilichowaondoa wakoloni kwa mapambano ama kwa aina yoyote ile ya kiukombozi, kwa kawaida hupora haki za wananchi wenzao na chenyewe hujifanya ndiyo kisemaji cha kila jambo la nchi na wenye mawazo tofauti na chama hicho huonekana ni wasaliti.

Leo Afrika ya Kusini Julius Malema anaonekana ni Kibaraka wa Makaburu na wanasiasa wenzake wa ANC kwa kuwa tu amekuwa kinyume na ANC.

Huwezi kuwa Rwanda ukaanza kuwa kinyume na uongozi wa Rwanda Patriotic Front (RPF) halafu bado ukaonekana ni mzalendo.

Robert Mugabe ameondolewa kwenye uongozi wa chama cha ZANU-PF na serikali ya Zimbabwe lakini bado ZANU - PF wanaamini kwamba wao peke yao ndiyo wenye haki ya kutawala Zimbabwe. Mugabe hayupo lakini ZANU - PF inajiona yenyewe ndiyo Zimbabwe na Zimbabwe ndiyo ZANU - PF.

Watu wanashangaa ni kwa nini Korea ni nchi mbili zinazofanana kwa kila kitu linapokuja asili ya watu wake, lakini Korea ya Kaskazini inaendeshwa kama ni mali binafsi ya Familia ya kina Kim Un. Tatizo ni chama cha kimapinduzi.

Nchi yoyote yenye kuongozwa na chama kinachojifanya ni cha kimapinduzi ni lazima wananchi wa nchi hiyo waishi maisha kama ya watumwa kwa kuwa vyama vya kimapinduzi vina tabia ya kupora haki za raia wake.
 
Sasa na wewe si ufanye mapinduzi ili uturudishie HAKI wananchi

Mzalendo wa kweli halalamiki (jonas savimbi)

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Na vyama hivyo hujitahidi sana kuwafanya wananchi wawe wajinga na masikini ili viendelee kuwatawala bila shida! Mfano ni serikali ya awamu ya tano kutopenda biashara na wafanyaɓiashara kwa kukumbatia unyonge kama sifa nzuri kwa wananchi kuwa nayo!

Kutopenda wananchi kupata taarifa mbambali zinazowaelisha na badala yake kuwafungia kwenye kasha la propaganda za uongo za kusifu na kuabudu watawala!

Njia mwafaka ya kuviong'oa vyama hivi ni kwa njia ya mapinduzi tena. Baaɗa ya hapo masalia ya wenye fikra mgando za kimapinduzi watakuwa wameisha ama wameshatambua ni maana ya demokrasia katika jamii iliyostaarabika!

Tofauti na hapo wataendelea kutufugia makundi ya wasiojulikana ili tuendelee kuwapigie magoti!
 
Ni nadharia tu Lkn ukisoma history ya vyama vikongwe vilivokufa mfano KANU, Zambia, Malawi, nk unakuta vilikufa sababu ya kubebwa na dola na si mioyoni mwa wananchi. Chama chochote kinachotegemea kubebwa na dola lzm kitakufa ni suala LA mda tu pale kosa LA kiufundi likijitokeza,
 
Na vyama hivyo hujitahidi sana kuwafanya wananchi wawe wajinga na masikini ili viendelee kuwatawala bila shida!
Ukiangalia hata kwa Tanzania utaona yale maeneo ya mijini kwenye elimu na hali bora kiasi ya maisha ndiko ambako CCM inapingwa.

Ukikuta kijiji kina maendeleo ya aina fulani inakuwa ni rahisi sana kwa chama cha upinzani kupata uungwaji mkono. Huwezi kuona mijini kwenye maeneo maskini wakiunga mkono wapinzani.
 
Kaulia mbiu yao ni tishio tosha,(kidumu chama cha mapinduzi).

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukitaka kuwatawala watu wanyime elimu wafanye kuwa masikini, wakomoe kwenye kodi ,watungie Sheria Kali za kuwatawala ,nk ila don't try this at home wakikugeuka utaukumbuka msemo usemao heshima ya dikteta ni kuondolewa madarakani kwa aibu,watu hawatokuwa wajinga siku zote njaa ikizidi.
 
Huyu jamaa huwa namuweka kwa sababu ya uthubutu wake wa kuingia forest
Inawezekana akawa ni mwanamapinduzi lakini akawa siyo Mzalendo.

Yaani wanamapinduzi wengi wa Afrika huwa na makando kando ya kufadhiliwa kutimiza uanamapinduzi wao na mwisho wa siku huwa vibaraka wa hao waliowafadhili. Leo hii ndiyo inajulikana kuwa ugomvi wa "mwanamapinduzi" Idd Amin na "Mzalendo" Milton Obote ulitokana na kugombania madini yaliyokuwa yanachimbwa kiharamu toka Kongo.
 
Alivuna alichopanda akazikwa kama mzoga wamarekani walipomtumia wakamtupa km Le profu alivotupwa na chakavu
Ndiyo maana mimi huwa nasema mtu asiye na mwelekeo labda aniteke, lakini siwezi kuunga mkono harakati za kijinga kwa furaha ya muda mfupi. Hivi wale Askari zaidi ya 100 wa Marekani waliokuwa "wanasaidia" kumpata Joseph Kony wa Lord Resistance Army (LRA) unadhani walikuwa wanafanya vile kwa maslahi ya Uganda?
 
Chama chochote kikibebwa kwa misingi ya dola kitakufa tofauti na chama kitakachojengwa kwenye misingi ya watu,yaani kiishi moyoni mwa watu.Mfano slow anakiishi chama sababu ananufaika,akikatiwa mfumo wa kula hawezi kukiishi chama.Ili chama kiishi ni lzm wananchi wanufaike na kuwepo wa chama hicho
 
Back
Top Bottom