Kuna msemo unaosema kuwa Viongozi madikteta na vyama vya kidikteta kama cha Magamba huwa wana silaha moja tu ya kutawala nayo ni Kuwajaza wananchi wao uoga, lakini siku wananchi wakigundua kuwa viongozi hawa pamoja na vyama vyao hawana msaada wala umuhimu wowote katika maisha yao, mwisho wao huwa umetimia.
Watu wote wenye mapenzi mema na nchi yetu ambao tumeshajua kuwa chama cha magamba hakina manufaa yoyote kwa nchi yetu tuhubiri ukombozi kwa wale ambao bado akili zao zimetekwa. Ule mwisho uliotabiriwa umekaribia, wale wachache wanaofikiri walizaliwa wakakuta wazazi wao ni viongozi wakawarithisha na sasa wana ndoto za kututawala wasahau, hiyo chain haiwezi kuendelea. Waendelee kutumia vyombo vya habari kueneza uongo na kutisha wananchi lakini ule mwisho upo na umekaribia. Tumekuwa kwenye lindi la umasikini bila sababu za msingi wakati wao wakineemeka. Watu wa ajabu ajabu tu basi kwa sababu eti baba zao walikuwa mwanasiasa mashuhuri basi na wanaandaliwa kututawala! Wamejaa viburi na dharau, hawajui nguvu ya wananchi ilivyo kubwa, wakawaulize watoto wa Ghadaffi.
Kuna watu wa ajabu kweli siku hizi ati ni wanasiasa! hawajui lolote wala chochote, ukiwasikiliza wakiwa wanaongea unajiuliza hivi hii nchi ndio imefika hapa! Wana madaraka makubwa kweli ukijiuliza wameyatoa wapi huwezi kufahamu. Hivi jamani ndio tumefika hapa kweli? watu kwa uroho wao wanataka kututawala hata kama ni kwa kutuua?