Vyama visivyo na wawakilishi bungeni kuanza kampain kesho

state agent

JF-Expert Member
Jul 1, 2019
1,764
2,511
Wametangaza kuwa kesho wanakiwasha wanaanza mapambano mkali dhidi ya CCM ,Wamesema hawatakata tamaa kwani hata waliopo bungeni walipata nafasi bila hiyo tume huru kwani siasa ni mpambano.Wapo vema kuwatumikia watanzania ngazi za serkali za mitaa na kusema hao ndio wananchi wanyonge na kujitoa ni kuwadharau na kuwatelekezaWanatuma salamu kwa vyama vyote vinavyojiona viko juu kuacha kudharau chaguzi za chini kuwa ndio hasa watanzania maskini walipo na kupambana sana 2020 wapate majimbo

State agent

===

Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema akifungua mkutano mkuu.
VYAMA visivyokuwa na uwakilishi bungeni, TLP, UMD na DP, kesho tarehe 17 Novemba 2019 vitaanza kufanya kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Hayo wamesema viongozi wa vyama hivyo, katika nyakati tofauti leo tarehe 16 Novemba, 2019, wakati wakizungumza na mtandao wa MwanaHALISI ONLINE, kwa njia ya simu

“Mimi kesho nitazindua kampeni za chama changu kwenye kijiji changu cha Kiraracha, Marangu Magharibi, jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro,” amesema Mrema.

Abdul Mluya, Katibu Mkuu wa chama cha DP, amesema chama chake kitazindua kampeni za uchaguzi huo, katika wilayani Buhingwe, mkoani Kigoma.

Hata hivyo, Mluya amedai kuwa, wagombea wake wengi wanashawishiwa na baadhi ya wananchi kujitoa katika uchaguzi huo.

Kamana Mrenda, Mwenyekiti wa Chama cha UMD, ameeleza kuwa, wamejipanga vyema kufanya kampeni katika maeneo waliyosimamisha wagombea. Na kwamba, chama chake kitazindua katika wilayani Kabondo mkoani Kigoma.
Kampeni za uchaguzi huo zinatarajia kuanza kesho, na kumalizika tarehe 23 Novemba mwaka huu. Kisha uchaguzi utafanyika tarehe 24 Nove,ba 2019.


CHANZO: Mwanahalisi online
 

Attachments

  • IMG-20191116-WA0045.jpeg
    IMG-20191116-WA0045.jpeg
    83.3 KB · Views: 1
Hivi vyama vilete ushahidi kuwa vina wagombea hata kwenye kijiji kimoja.

Hii ni habari inayoonyesha kuwa ujinga umetamalaki nchini.
 
Daah hii kweli kali..!!

So wagombea wao wamewasimamisha kwenye mitaa gani hawa jamaa?? Mbona wanaamua kutuchekesha bila malipo!! Tipumzisheni guys watu wenyewe hatujala sisi..!!

BACK TANGANYIKA
Wewe una maana hujui kitabu chenye majina ya wagombea anamiliki nani?Kesho ukikuta wagombea wa TLP wapo nchi pote utabisha? Subiri yajayo ndio utajua Who is Slow Slow na hekaya zake za Abunwasi
 
Back
Top Bottom