Vyama vingi marufuku Tanzania

Varbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
1,117
856
UKWELI KUHUSU HALI YA KIUSALAMA NCHINI, Ndugu zangu Watanzania na wapenda Aman kwa ujumla Haya ni mawazo yangu kutokana na Hali ya Usalama inavozidi kuzorota siku hadi siku! Kuanzia miaka ya 1990-2013 nchi yetu imeshuhidia vifo vingi vinavyoletwa na vurugu hasa za kisiasa, Matukio ni mengi ya kiwa ya wale wanachama wa CUF Kule Zbar, mauaji ya wachimbaji Kule Mara, mauaji ya Mara kwa Mara Kule Arusha!, Mauaji yote haya yanafanywa na polisi waliotayari kuua wakati wowote kwa waandamanaji au kwenye Mikutano ya wapinzani ambao hawana hata Fimbo mkononi! Wao wakiwa na SMG na risasi za moto! Mauaji hayo mengi ilikua sio rahisi kubaini nani anahusika moja kwa moja Lkn mengine imeinekanawazi kabisa polisi wanaua wazi wazi, KIINI CHA HAYA, chanzo cha yote ni CCM kutokubali chama kingine kichukue uongozi wa eneo Fulani iwe Udiwani, ubunge au uwenyeviti wa vijiji! Tabia hio ya chama tawala ndio inayo ongeza wimbi la vifo Kila uchao! Hata Kama ushahidi upo wazi hukataa na kutumia madaraka Yao kughilibu na kuficha UKWELI, mfano mauaji ya Mwangosi, kipigo cha Dr Ulimboka japo ushahidi upo wazi bado waliendelea kukanusha, Tanzania ni moja ya nchi ambayo inaweza kuzalisha vikundi vya waasi Kama tabia Kama hizi haziwezi kuzibitiwa! Kama tumechagua vyama vingi kuwe na uwanja sawa na sio kudidimiza upande mmoja! Urushwaji wa Bomu Arusha Polisi wamehusika baadhi ya majeruhi walimuona muuaji akiwa na sare za polisi na akitoweka ndani ya gari la polisi! Kwa kuona watanzania hawaelewi Serikali inatoa 100mil kwa atakae fanikisha upatikanaji wa mlipuzi! Ukichunguza haya yote utagundua kua CCM haipotayari na Siasa za vyama vingi! Pamoja na ufisadi na kushindwa kusimamia Rasilimali za Taifa hili hiki chama kimeonyeaha kipo tayari kuua yeyote ili kuendelea kukaa madarakani!! Wito wangu muda umefika wa kukusanya ushahidi na kuipeleka kwenye mahakama za kimataifa hii serikali dhalimu kabla hatujaanza kuuana wenyewe kwa wenyewe!!
 
Ulimbukeni tuu unatusumbua hatujui namna ya kuendesha siasa
 
wazo ni zuri mzee na ikumbukwe dhana ya mfumo wa vyama vingi tumerith toka nje kama dini tulivofanya lakini tumevibadili maana toka tulolengea na kuwa ya faida binafs za watu wachache
ningependekeza vyama vyote vilivopo vifutwe na kwa kutumia itikadi mpya na visheria vipya vya uundaji vyama hivo ungetumika kuunda upya
 
CCM hawana hati miliki na hii nchi, hii nchi ni yetu sote wasitutishe. Hao polisi inaowategemea hadi kufikia 2015 tutakuwa tumeishazoeana nao tu na watakuwa wamenusa uelekeo wa upepo kwa wananchi tumeikataa CCM na wao wako 10,000 tu hivyo kura za mapolisi hazitaibakiza CCM madarakani.
 
Mimi nina mawazo tofauti na yako.Tatizo hapa sio vyama vingi.Lakini pia tatizo sio kurithi vyama vingi kutoka ughaibuni.Kwa sababu hata kama tutabaki na chama kimoja,bado tutahitaji mabadiliko ya kiutawala.Sasa ikiwa walioko madarakani hawatakuwa tayari kuwapisha wengine bado tutaendelea kushuhudia mauaji tu.Pia tusisahau iwe ni chama kimoja au vyama vingi hiyo ni mifumo tuliyorithi kutoka ughaibuni.

Mimi nadhani jamii nzima tunatakiwa kujitathmini upya.Matatizo tunayoyaona,iwe ni ya kiutawala au hao wanasiasa tusiokuwa na imani nao,yanatokana na mabadiliko ya kiujumla katika jamii yetu.Sio rahisi jamii iliyoporomoka ikatoa watu wema.Tunawaonea tu hao wanasiasa,maana wanatokana na jamii hii hii tunayoishi.Hatutegemei jamii corupt itoe viongozi/wanasiasa malaika,never.Kwa hiyo tunapokuwa tunawalaumu wanasiasa/viongozi lazima kuangalia na upande wa pili ambao ndiyo hii jamii yetu tunamoishi.
 
Back
Top Bottom